Je tanzania ni taifa mfu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je tanzania ni taifa mfu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mnyikungu, Sep 23, 2009.

 1. mnyikungu

  mnyikungu JF-Expert Member

  #1
  Sep 23, 2009
  Joined: Jul 26, 2009
  Messages: 1,446
  Likes Received: 591
  Trophy Points: 280
  Nilipokuwa shule ya msingi darasa la tano mwalimu wetu alikuja na kutuuliza utamaduni ni nini? kwa kweli hakuna aliyejibu jibu lililomlizisha mwalimu mbaka mwenyewe alipotuambia kuwa utamadumi ni uhai na kielelezo cha kabila/nchi yoyote duniani,Hapa ndipo swali langu linapokuja je Tanzania ni ni nchi mfu? ni kielelezo gani kinachotutambulisha na kutuonyesha utaifa wetu?je tukisimama nje ya tanzania nani atajua kama sisi ni watanzania? au ndio utandawazi umetuharibu?
  Wenzetu hutumia nguvu nyingi sana kulinda tamaduni zao je Tanzania yetu inafanya hivyo? mimi nilifikiri labda lugha yetu ya kiswahili ndio inayoweza kutusaidia lakini mbona sijaona ikipewa umuhimu wake? nenda leo mahakamani utaona ni kichekesho mtu kutoka kijijini anapohukumiwa kwa kiingereza, yaani tumeshidwa kabisa kulinda utamaduni wetu! lugha za makabila yetu zinapotea lakini sijaona juhudi zozote za kuziokoa lugha hizo,Elimu ya sayansi haileti matokeo mazuri kwa sababu ya lugha, wanafunzi badala ya kuelewa wengi wanakariri,Tofauti na nchi kama japani au china ambao tamaduni zao wanazienzi,si ushirikina bali ni kwa tamaduni zao ndio maana leo wapo hapo walipo.
  uMEFIKA WAKATI TANZANIA INATAKIWA IBADILIKE KWA KUENZI NA KULINDA UHAI WAKE ILI LIENDELEE
   
 2. H

  Haruna Malima Member

  #2
  Sep 23, 2009
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tanzania ina utamaduni wake na inaulinda kwa dhati nao ni Kiswahili. Mfano wa mahakama ni mfu kwa sababu lugha ni optional nako ni Mahaka za juu tu. Mahakama za Mwanzo na Wilaya ni Kiswahili pia kwa Hakimu mkazi mkoa ni kiswahili. Mteja ana uhuru wa kuchagua lugha. Asilimia mia moja ya Wabongo wanaongea Kiswahili. Unataka ID gani? Chuo kikuu tunafundishwa kwa Kiingereza nk lakini tunafanya discussion kwa Kiswahili na kujibu kwa Kiingereza nk, hivyo lugha inatumika ngazi zote za Elimu, UPO! Je ni watu wangapi umewaona wanasoma magazeti ya Kiingereza kama si kiswahili hadi kwa graduates!
  Kitambulisho cha Mtanzania ambacho ni Peculiar ni Kiswahili.
   
 3. mnyikungu

  mnyikungu JF-Expert Member

  #3
  Sep 23, 2009
  Joined: Jul 26, 2009
  Messages: 1,446
  Likes Received: 591
  Trophy Points: 280
  bila shaka hujui unachokiongea,mi naliongelea kama taifa na nalinganisha na mataifa mengine kama afrika kusini ufaransa, libya,misrina nchi nyingine nyingi,angalia watawala wetu hata bungeni tu wanaingiza kiingereza,mikutano mingi ya hapa kama kuna kiongozi wa nje utaona wanatumia kiingereza.nakumbuka jack shirak wa ufaransa aliwahi kutoka nje ya mkutano wa umoja wa ulaya kisa waziri wake kaongea kiingereza na huu ndio mfano ninaotaka uigwe na watawala wetu,kama kweli tunaulinda utamaduni wetu kwanini lugha ya kufundishia tunapotaka iwe kiswahili liwe lina mjadara tena mrefu namna hii?
   
 4. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #4
  Sep 23, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Hapana!
   
 5. H

  Haruna Malima Member

  #5
  Sep 23, 2009
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mfano wa Afrika Kusini ondoa kabisa kwa vigezo hivyo kwani hao elimu yao ni kwa Kiingereza, Halfu wanamkoroganyo wa lugha za kikabila,Hawana ID kabisa!Bunge lao linaongea Kiingereza kwa kwenda mbele, ili hali wao si Waingereza UPO! Nami naongea kama taifa la Tanzania, Mahali popote tunajitambulisha kwa KISWAHILI na si vinginevyo. Umeanzisha mada ukiwa huijui.Kumbuka lugha inakuwa, inalelewa kwa kutohoa au kuingiza maneno mapya, usiwe lagard wa evolution of culture.
   
 6. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #6
  Sep 23, 2009
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Hapa USA nimekutana na Wacongo toka Goma wanapiga kiswahili saafi nao ni Watanzania?
  Kuna Waganda toka North Uganda wanaongea kiswahili kama wameishi Tanzania vile lakini bado si watanzania.
  Wako Wanyarwanda wanaongea kiswahili kizuri sana kwa kukipenda kama lugha nao ni Watanzania?
  Wakenya wa Mombasa na Lamu wanakirudi kiswahili kama kuria kata ya mbege.
  Wasomali toka visiwa vya kismayu wanaongea kiswahili safi kama wapemba, hata sura na tabia zao wanafanana na wapemba lakini bado si Watanzania.
  Kiswahili siyo Kitamburisho cha Mtanzania yeyote labda kwa kujidanganya tukiwa ndani ya mipaka ya Tanzania.
  Tukubali ukweli kwamba hicho kitamburisho hakikuwepo tangu zamani. Uongo namba moja, tulijidanganya kwamba tunacho kitambulicho cha kitaifa na sasa tunasema uongo namba
  mbili kwamba sijui utanda wazi au sijui tumeshindwa kukilinda!!!

  Ni lini tulitamka wazi kwamba Kiswahili ni Kitambulisho cha MTanzania?
  Tamko hilo lilitolewa au kupitishwa na nani na pia wapi huko lilipitishwa?

  Unaweza kulinda kitu kisichokuwepo???
   
 7. H

  Haruna Malima Member

  #7
  Sep 23, 2009
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  'bila shaka hujui unachokiongea,mi naliongelea kama taifa' Tafakali maelezo yangu ni Scientific to ur views. Sijarejea maamuzi ya kijiji ni ya kitaifa. "Mfano wa mahakama ni mfu kwa sababu lugha ni optional nako ni Mahaka za juu tu. Mahakama za Mwanzo na Wilaya ni Kiswahili pia kwa Hakimu mkazi mkoa ni kiswahili. Mteja ana uhuru wa kuchagua lugha" Tazama ulichoongea-"utaona ni kichekesho mtu kutoka kijijini anapohukumiwa kwa kiingereza, yaani tumeshidwa kabisa kulinda utamaduni wetu!" Au wewe ndo hujui ulichopresent kama mada??!! Umefanya research ngapi zinazoonyesha kuwa anayefikishwa/fika mahakamani akitokea kijijini hajui kiingereza? Au umekuwa myopic circumveted na kijiji cha kwenu utokako, ukazani Tanzania yote haina wanaojua kiingereza vijijini? Tanzania tunalinga na utamaduni wa lugha ya Kiswahili na Kimombo chamwagwa hadi VIJIJINI ambako kuna maafisa Ugani, walimu, waganga na wauguzi,maafisa wastaafu nk. Kuwa INTEGRATIVE ndugu!
   
 8. mnyikungu

  mnyikungu JF-Expert Member

  #8
  Sep 23, 2009
  Joined: Jul 26, 2009
  Messages: 1,446
  Likes Received: 591
  Trophy Points: 280
  nilihisi kuwa wanoosoma tovuti hii ni waelewa kumbe sivyo wengine wanabisha tu ili waonekane wanabisha haya mkubwa
   
 9. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #9
  Sep 23, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Ukweli ni kwamba kihistoria, kuna watu walikuwa wanaitwa Waswahili (ambao walikuwa wana lugha moja na utamaduni unaofanana). Territory ya hawa Waswahili ilikuwa inaanzia pwani ya kusini mwa Somalia hadi kaskazini ya Mozambique na pia visiwa vya Indian Ocean (Unguja, Mafia, Commoro. nk). Siku hizi utamaduni na lugha ya Waswahili hawa (yaani Kiswahili) imeenea hadi Congo, Rwanda, Uganda ...
   
 10. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #10
  Sep 24, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,598
  Likes Received: 3,890
  Trophy Points: 280
  Muanzisha maada, maada yako ni nzuri na very critical, ambayo, matatizo mengi sana yanayotokea hivi sasa ni kuwa hatuna utamaduni, hatuna maandiko, miiko, hatuna kitu.

  Je viongozi wetu wakila rushwa na kutuhumiwa wanaachia madaraka?
  nini adhabu ya wala rushwa?
  ....
  .....

  je tunalinda mali zetu?
  kwa kiasi gani mali zetu zinakuwa na wananchi na si za watu wachache?
  je elimu yetu inaendana na hali halisi ya taifa letu na mahitaji yetu..

  Swali lako ni basic, na msingi wa haya yoooote tunayoyapigia kelele hapa, to be honest, inahitaji greath thinkers to go to thoe basics, ama sivyo tutajaza post humu, kila mtu atatushangaa

  Je utamaduni wetu unasemaje kuhusu waliotuhumiwa na rushwa, tuwapokee kwa mazuri mekundu, ukieeenda mbali ungundua tatizo si viongozi tu bali hata wale wanaowaongoza,

  Ila title kidogo kali?

  Ni taifa hai lisilo na utamaduni , utamaduni unakuwa hai kwenye taifa linalopractise huo utamaduni.
   
 11. M

  Mkandara Verified User

  #11
  Sep 24, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu naona sasa wewe umekwenda mbali sana... hivi Marekani wanapozungumza kiingereza ina maana wao ni waingereza na hawana haki ya kudai kuwa lugha hiyo ni ID yao..Hivi nani kasema na imepitishwa wapi na lini?..Nani aliyepitisha hata kiingereza kuwa lugha ya mawasiliano duniani! wapi na lini maanake hata sikuelewi kwa sababu lugha hiyo inazungumzwa na watu kibao wa mataiufa kibao kama kiswahili unachokihoji hapa..

  Hata Mjamaika akizungumza Patwa, hicho kiingereza cha kuchonga hiyo ni ID yao kama vile wewe leo hii ukiamua kuvaa lubega wa Kimasai basi iondoe uhalali wa vazi hilo kuwa la kimasai. Mkuu kuna vitu vya jadi fulani na hakika kiswahili ni moja ya ID za Mtanzania kwa sababu Utanzania ni utaifa ulokuja miaka ya 60 na historia yetu kama Taifa inaanzia hapo.
  Sasa labda tukuulize wewe hilo vazi la kimasai lini ilitamkwa kuwa ndilo vazi lao, nani na wapi lilipitishwa...
  Maswali mengine jamani aaaagh!
   
  Last edited: Sep 24, 2009
 12. mnyikungu

  mnyikungu JF-Expert Member

  #12
  Mar 3, 2010
  Joined: Jul 26, 2009
  Messages: 1,446
  Likes Received: 591
  Trophy Points: 280
  lakini taifa haliwezi kuwa taifa bila utambulisho ambao ni utamaduni
   
Loading...