Je tanzania kuna demokrasia?

Njoka Ereguu

JF-Expert Member
Apr 7, 2012
821
335
Katika gazeti la mwananchi kuna makala iliyozungumzia demokrasia na kubainisha kuwa Demokrasia haina maana kama haiendi sambamba na kuwaletea wananchi maendeleo. Ukiangalia mwenendo wa siasa za Tazania neo demokrasia linatamkwa mara nyingi sana, na kuwa Tanzania ni moja ya nchi inayojivunia kuwa na demokrasia for the last 50 years.

Je wanasiasa wetu wanatumia neo demokrasia ili kuendelea kujiweka madarakani na kujineemesha badala ya kuwaletea maendeleo wananchi wake? Jinsi siku zinavyosonga mbele tunaona hali ya uchumi wa wananchi wa Tanzania inadidimia, elimu inashuka pamoaja na kuongezeka kwa idadi ya shule na wanafunzi wanaojiunga bado kiwango cha ufaulu kiko chini sana, huduma za afya ndiyo usiseme, usalama wa Tanzania umebaki ule wa mipaka ya nchi lakini mwananchi wa kawaida na jasho lake hana amani kabisa ilikinganishwa na tulikotoka. Haki ya msingi kwa watu, vyama vya siasa, asasi za kirai na mtu nazo zimetekwa na watu wachache ili kulinda maslahi yao.

Je tafsiri ya demokrasia Tanzania ni tofauti na nchi nyingine?
 
Back
Top Bottom