MUKINGA MSANGI
Member
- Apr 20, 2013
- 12
- 1
Mimi napata wawasi sana kuhusu maendeleo ya nchi yangu miaka hii ya karibuni, kipindi cha nyuma nikimaanisha enzi za uongozi wa kwanza hadi wa tatu, kidogo tulikua tunajivunia kua na viwanda kama; viwanda vya magunia Morogoro, vya kusindika matunda, kiwanda cha tyres Arusha (gerneral tyre in Arusha), Kiwanda cha kutengeneza karatasi Mfindi (Mgololo)Iringa, hivyo inlivyotaja ni vichache,ongeza vingine unavyojua!Sasa swali ni hili; Nani ameviua viwanda hivi ambavyo vijana waliowengi wangeajiria katika viwanda hivi. Na kama vimekufa kuna vingine ambavyo vimeanzishwa au kufufuliwa kati ya vile ambavyo vimekufa?. Ili nchi iendelee lazima iwe na uongozi bora, siasa safi bila porojo, rasilimali watu na kingine cha muhimu ni viwanda.
Sasa kama viwanda vimekufa, uongozi niwakuungaunga na siasa ya nani mwanzilishi wa udini na kushikana uchawi kweli tutafika?. Nikionacho nchi yetu inarudi nyuma kimaendeleo kutokana kutokuweka vipaumbele vya maendeleo pia baadhi ya vyama kuangalia masilahi yao badala ya Taifa. Maendeleo ya nchi yanarudi nyuma au yanaendelea?