Testar
JF-Expert Member
- May 30, 2015
- 7,615
- 12,896
Naona serekali ya CCM imekusudia kuua upinzani Tanzania.Inatumia kila mbinu kuzuia mawasiliano kati ya wapinzani na wananchi, hakuna bunge Live, hakuna mikutano ya kisiasa wala uhuru wa habari wa kutosha.
Wakati CCM wakiwazuia wapinzani kuwafikia wananchi, wao ndio wanazidi kujitangaza zaidi.
Wanatumia vyombo vya habari vya umma na vya watu binafsi, ziara za kiserikali, mikutano ya siasa ili kujionesha zaidi kwa wananchi.
Itakapofika 2020 wapinzani wataonekana kama wageni kwa wananchi wakati CCM wakionekana kama watu waliozoeleka na kama chama pekee cha siasa.
Hii itasababisha ushindi wa kishindo kwa CCM na kupunguza nguvu ya upinzani nchini kwa kiasi kikubwa sana.
Baada ya 2020 kasi ya kuwafunga wapinzani na kuwazuia wasiwafikie tena wananchi itaongezwa.
Kufikia 2025 upinzani utakuwa umezikwa rasmi na kubakiwa na CCM pamoja na vyama vichache vya kusaini matokeo ya uchaguzi.
Hapa ndipo itakapokuwa rahisi zaidi kutindua katiba na kuifanya iseme jinsi watakavyo hata kama ni kujiongezea miaka mingine 10.
Kama udikteta utatokea Tanzania basi utaanza 2025 baada ya kuuzika upinzani.Hapo tutakuwa na Taifa la chama kimoja na ikiwezekana itakuwa la mtu mmoja.
Kama wapinzani wanaitakia mema Tanzania, ni lazima wasimame wakati huu kupigania haki zote hasa za kisiasa ili pawepo na fair ground. Wasibabaishwe na hizi kesi zenye nia ya kuwaweka busy mahakamani.
Kwa nchi za kiafrica upinzani ni harakati sawasawa na zile zilizotumika kudai uhuru.