Je Tanzania ina Uongozi Bora?

QUALITY

JF-Expert Member
Sep 27, 2010
853
115
wana JF na watanzania kwa ujumla,

Tumeona watawala wetu mbalimbali wakifanya madudu na hakuna anayechukua hatua au kutoa kauri kali kukemea. sasa tumefikia hatua ya mabomu kulipuka mara kwa mara na serikali kukaa kimya. Tumeshuhudia kamati/tume zikiundwa na kuleta majibu yasiyofaa halafu watawala wetu wanachekelea na kukejeli wananchi.

Yako maswali mengi ya kujiuliza kwa serikali yatu
1. Serikali imejifunza nini tangu mabomu ya mbagala kulipuka?
2. Waliosababisha uzembe huu wa Mbagala, walifanywa nini?
3. Wananchi waliopoteza majengo/nyumba zao mbagala mpaka leo kuna ambao hawajalipwa. watalipwa lini?
4. Kuna waliopoteza maisha, serikali imefanya nini kwa familia hizo?
5. Wao wataalamu wa mipango miji wanaopima na kutoa viwanja mpaka jirani na makambi ya jeshi, na hati kutolewa, wameshughulikiwa namna gani?

Tuanzishe vuguvugu la kupata viongozi bora kuepukana na mabalaa haya.
 
Swali: Je Tanzania ina uongozi bora?

Jibu: Ndio na hapana. Inategemea unajibu kwa kuzingatia nini na kutoka chama gani.
 
Uongozi bora wakati bunge limetawaliwa na ubabe wa Makimba na mikojo ya Pindapinda, Rais Fisadi wasaidizi wake je? Uongo bora utoke wapi kwenye Serikali ya Kifisadi :coffee:
 
Back
Top Bottom