Je, Tanzania ina uhaba wa wawekezaji?

Je, Tanzania ina uhaba wa wawekezaji?

Traxtion

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2021
Posts
5,895
Reaction score
11,788
Wakuu, kwa maeneo niliyotembea hapa Tanzania naona kama uwekezaji upo haba sana, namaanisha uwekezaji wa makampuni makubwa.

Inaonekana miji yetu inakua kwa kasi ila maghorofa hamna, mfano ukisikia mji umekua kwa kasi basi jua tu ni wakazi ndio wameongezeka na wanaanza kufungua frame na kujenga nyumba, ila uongezekaji wa hotels, makampuni nk naona ni mdogo

Mfano Mwanza Jiji kuna watu zaidi ya milioni 1 lakini ukifananisha maghorofa na Mombasa au Kigali unaweza kujiuliza nini kinafanya Mombasa na Kigali ijengeke kuliko Mwanza licha ya kuwa na population zinazokaribiana

Mimi najiuliza kwa nini miji yetu ya Tanzania ipo hivi? Inakuaje Mbeya jiji la watu laki 7 maghorofa ya kuhesabika?

Mimi nilitegemea sehemu ikiwa na watu wengi basi na makampuni mengi yatakuja kuwekeza, yatajenga ofisi zao na mara nyingi huwa ni ghorofa, lakini la hasha. Sisi miji yetu ukuaji wake ni kuongezeka tu watu, na kupanuka ukubwa. Kwa nini?

Pia napenda kujua miji inayokua na kuongezeka maghorofa Tanzania ukiondoa majiji 6
Naongelea maghorofa kwa sababu najua kwenye sekta nyingine kama barabara, hospitali, shule nk miji ya Tanzania inajitahidi.

📷 Ruangwa, Lindi
1754561983946.jpg
Screenshot_2025-08-07-13-16-14-344_com.google.android.googlequicksearchbox.png
 
Purchasing power ya watanzania ni ndogo sana; vipato vya watanzania ni vya kula ubwabwa dagaa.

McDonalds ataenda kuwekeza mahali kama hapo kweli? Au KFC? Hiyo ni migahawa tu sembuse uwekezaji wa maana!
 
Purchasing power ya watanzania ni ndogo sana; vipato vya watanzania ni vya kula ubwabwa dagaa.

McDonalds ataenda kuwekeza mahali kama hapo kweli? Au KFC? Hiyo ni migahawa tu sembuse uwekezaji wa maana!
Ila hiyo ni point sahihi. Ili miji yetu ikue nahisi vijana wengi wanapaswa wapate ajira (kuajiriwa au kujiajiri) ili kuwe na mzunguko wa hela na purchasing power iongezeke, hapo uwekezaji utakuwepo
 
Wawekezaji uchwara wapigaji na wakwepa kodi tunao wengi sana
 
Ni karatu ndyo inaendana na ukuaji wake magorofa ni mengi inakizi hali ya mji tofouti na miji mengne tz
 
Back
Top Bottom