Je, Tanzania ihalalishe matumizi ya Bangi?

Je, Tanzania ihalalishe matumizi ya Bangi?

ShyaRuwa

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2015
Posts
8,448
Reaction score
15,374
Nimejaribu kuvuta picha ya mtu aliyehalalisha pombe na sigara na kuharamisha bangi lakini nimeshindwa. Nimetafakari juu yake kama alifanya utafiti wa kutathimini faida na hasara za pombe na sigara vs bangi lakini sikufikia mwisho wenye majibu. Sijui alifikiri nini.

Nikaingia mitaani kufanya mlinganisho wa maisha ya watu wanaotumia pombe+ sigara pekee V/s wanaotumia bangi pekee, ila niliambulia taharuki, idhaniwayo kuwa nyeupe ni nyeusi na kinyume chake pia. Uchunguzi wangu hauna nguvu ya kuuanika hapa jukwaani lakini ebu pambanisha watu wa hayo makundi mawili kwenye mbio za riadha alafu utuletee mrejesho.

Kila sarafu ina pande mbili, vivyo hivyo kila jambo lina faida na hasara zake, Hata kitu unachokiona cha faida zaidi nacho kina hasara zake. Bangi nayo ni moja wapo, ina faida na hasara zake. Licha ya kwamba imeharamishwa, matumizi yake yapo juu sana, na wanaotumia siyo vijana wa mitaani pekee wasio na kazi, bali kuna watu nimewashuhudia wakiitumia bangi kwa njia mbalimbali walionifanya niutafakari mtazamo wangu juu ya bangi.

Kwenye jamii zetu, bangi imefanywa kuwa sababu ya kila baya kama wizi, wehu, magonjwa ya kansa, uvivu na umasikini, n.k ndio maana mtu akionekana anamsimamo tofauti na ule unaotegemewa na jamii anabandikwa jina la 'mvuta bangi'.

Tukianza kutaja faida na hasara za bangi hatutazimaliza, zipo nyingi nyingine za kweli na za uongo zinazotolewa na watu ili upande wanaoegemea uonekane upo sahihi.

Ndugu wanajukwaa kwa mitazamo na dadisi zenu, je Tanzania ihalalishe matumizi ya bangi?
 
Isihalalishe bangi badala yake iharamishe sigara
 
Hii kitu bhange inaondoa ,aibu kabisa ,sio madem na vitu vingne unaviona vya kawaida sana bora ihalalshwe tu
 
Hii kitu bhange inaondoa ,aibu kabisa ,sio madem na vitu vingne unaviona vya kawaida sana bora ihalalshwe tu
Sasa mbona watu wanaipinga sana ili hali ina faida kedekede?...Mkuu huu sio uonevu kweli?
 
Napenda sana bangi...Haina madhara makubwa kama tunavyojengewa taswira ya kutisha
pombe na fegi ni hatari kuliko bangi, feg ina moshi mzito wakat bang ina moshi mwepesi,ni bora waihalalishe itumike sehem na sehem,
MAJANI YA KONDENI ...naipenda hii kitu
 
Aliyevumbua na kutuaminisha kua bangi ina madhara sasa kairusu kutumiwa hadi kitabibu, sasa sijui kwanini sisi bado tunasema ina madhara
 
Moshi wa bangi ni mwepesi sana, unapenya kwa urahisi kwenye mapafu kuliko wa sigara.Ndio maana wavuta bangi hawakohoi hovyo kama wala fegi.
 
Aliyevumbua na kutuaminisha kua bangi ina madhara sasa kairusu kutumiwa hadi kitabibu, sasa sijui kwanini sisi bado tunasema ina madhara
Mkuu licha ya kukatazwa, inalimwa, kusafirishwa, kuuzwa na kutumiwa kwa siri lakini kwa kiasi kikubwa sana.Kwa nini isiruhusiwe ili watumiaji wawe huru kwenye nchi yao?
 
Niwe mkweli bangi sitoacha, bangi ni tamu. Nikivuta harafu niangalie taarifa ya habari. Naona habari zaidi ya kumi kwenye kila Habari..
 
Mwaka 1933 huko ulaya.kuna mwanamke alikuwa mtumiaji wa bangi baada ya muda alifikia uamuzi wa kuolewa na mtu mweusi na apo ndipo kuhalamishwa kwa bangi kulipotokea.
 
Naunga hojaa. Waturuhusu tumoke mmea wetu Mungu aliuumba
 
Mwaka 1933 huko ulaya.kuna mwanamke alikuwa mtumiaji wa bangi baada ya muda alifikia uamuzi wa kuolewa na mtu mweusi na apo ndipo kuhalamishwa kwa bangi kulipotokea.
Hahahahaaa kwahiyo walihisi bangi ndo chanzo cha interracial marriage?...Kumbe watasha nao wanaimani za kishirikina Mkuu?
 
Mm navuta bangi pekee,sinywi pombe wala sivuti sigara,ila huwez kua kama navuta labda unione kwa nilivy hata nikikwambia huwez kuamin.Naamin bangi nzuri ila inategemea kichwa cha mtu.
 
Back
Top Bottom