Je, Tanzania hatuongozwi bali tunatawaliwa?

Je, Tanzania hatuongozwi bali tunatawaliwa?

Bob Manson

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2021
Posts
4,546
Reaction score
8,759
Huwezi kuwapa sifa ya uongozi watu ambao wanatuhumiwa kutumia madhaifu ya wananchi kuimarisha mamlaka na tawala zao. Zifuatazo ni sababu za kuamini kwamba hatuna viongozi bali watawala.

1. Inadaiwa Wananunua vituo vya matangazo (media) kubwa zote.

Lengo ni ku control mitazamo ya wananchi, kuwalisha drama na propaganda ili wazidi kuwa wajinga na wasijue nini hasa kinaendelea katika uhalisia wa taifa lao. Media Ni kiungo muhimu katika ustawi wa taifa, na wanajua umuhimu huo ndyomaana wanafaya juhudi kununua kama sio kuhonga media hizo ili zifanye yale yenye manufaa kwao.

2. Wanatuhumiwa kuteka, kutesa na kuuwa wakosoaji.

Wakosoaji ambao wanafanya juhudi kubwa kuwazindua wananchi na kuwatoa katika janga la ujinga, hugeuka kuwa adui wa utawala huu. Atateswa hata kupotezwa kabisa ili wananchi wasipate atakaye wafumbua macho.

3. Inadaiwa Wanarubuni wasomi kwa kuwaaminisha wakiungana na chama chao basi watapata nafasi za ajira.

Vyuoni tunaona wimbi kubwa la wanafunzi kujiunga na kuwa wanachama wa chama fulani kwasababu wameaminishwa pasipo kufanya hivyo basi hawatapata ajira hasa serikalini.

4. Wanatumia uwanja wa sanaa kama silaha yao ya kupata ushawishi wa wananchi ( Bread and circuses).

Tunaona pesa nyingi zinatumika kuandaa matamasha ya muziki na kuwalipa wasanii, lengo ni kuwapumbaza wananchi kwa muziki na maigizo ili wazidi kuzama katika kiza cha burudani na kusahau mambo ya muhimu katika taifa lao.

5. Wanatumia michezo kama njia ya kucheza na hisia za watu.

Badala ya kuimarisha sekta ya michezo kwa kubuni na kuanzisha programu zenye manufaa, wao wanaonunua magoli na kulipia mashabiki tiketi za ndege. Lengo ni kuwaaminisha mashabiki kwamba wapo nao pamoja na wanawajali.

Hawa sio viongozi bali ni watawala ambao lengo lao kuu ni kuhakikisha wanabaki madarakani kwa nguvu zote, lengo lao sio kusaidia na kuwaokoa wananchi bali ni kuwatawala na kuwafanya wawe wajinga zaidi.

NOTE: Ujinga wetu ndyo mtaji wao mkubwa.
 
Huwezi kuwapa sifa ya uongozi watu ambao wanatumia madhaifu ya wananchi kuimarisha mamlaka na tawala zao. Zifuatazo ni sababu za kuamini kwamba hatuna viongozi bali watawala.

1. Wananunua vituo vya matangazo (media) kubwa zote.

Lengo ni ku control mitazamo ya wananchi, kuwalisha drama na propaganda ili wazidi kuwa wajinga na wasijue nini hasa kinaendelea katika uhalisia wa taifa lao. Media Ni kiungo muhimu katika ustawi wa taifa, na wanajua umuhimu huo ndyomaana wanafaya juhudi kununua kama sio kuhonga media hizo ili zifanye yale yenye manufaa kwao.

2. Wanateka, wanatesa na kuuwa wakosoaji.

Wakosoaji ambao wanafanya juhudi kubwa kuwazindua wananchi na kuwatoa katika janga la ujinga, hugeuka kuwa adui wa utawala huu. Atateswa hata kupotezwa kabisa ili wananchi wasipate atakaye wafumbua macho.

3. Wanarubuni wasomi kwa kuwaaminisha wakiungana na chama chao basi watapata nafasi za ajira.

Vyuoni tunaona wimbi kubwa la wanafunzi kujiunga na kuwa wanachama wa chama fulani kwasababu wameaminishwa pasipo kufanya hivyo basi hawatapata ajira hasa serikalini.

4. Wanatumia uwanja wa sanaa kama silaha yao ya kupata ushawishi wa wananchi ( Bread and circuses).

Tunaona pesa nyingi zinatumika kuandaa matamasha ya muziki na kuwalipa wasanii, lengo ni kuwapumbaza wananchi kwa muziki na maigizo ili wazidi kuzama katika kiza cha burudani na kusahau mambo ya muhimu katika taifa lao.

5. Wanatumia michezo kama njia ya kucheza na hisia za watu.

Badala ya kuimarisha sekta ya michezo kwa kubuni na kuanzisha programu zenye manufaa, wao wanaonunua magoli na kulipia mashabiki tiketi za ndege. Lengo ni kuwaaminisha mashabiki kwamba wapo nao pamoja na wanawajali.

Hawa sio viongozi bali ni watawala ambao lengo lao kuu ni kuhakikisha wanabaki madarakani kwa nguvu zote, lengo lao sio kusaidia na kuwaokoa wananchi bali ni kuwatawala na kuwafanya wawe wajinga zaidi.

NOTE: Ujinga wetu ndyo mtaji wao mkubwa.
Umasikini husababishwa na udumavu wa akili zetu hata hayo yote uliyo yataja yanasabishwa na jamii zetu kudumazwa akili tumeandaliwa kuto kuhoji na tatizo la kuhoji linaanza kwenye ngazi ya familia kuna vitu ukivihoji utaambiwa kama umekua uondoke ama kujibiwa bila hoja zenye mashiko, je tutaishi kwa bora liende hadi lini? yaani kuishi kwa matumaini ambayo hayatakuwa, (expecting results from what you know), kutegemea matokeo kwa mtu ambaye hawezi kukusaidia, ila hukupa matumaini anakuacha Solemba
 
Umasikini husababishwa na udumavu wa akili zetu hata hayo yote uliyo yataja yanasabishwa na jamii zetu kudumazwa akili tumeandaliwa kutoka kuhoji na tatizo la kuhoji linaanza kwenye ngazi ya familia kuna vitu ukivihoji utaambiwa kama umekua uondoke ama kujibiwa bila hoja zenye mashiko
Sasa kama hakuna uhuru wa kuhoji kuna tofauti gani na enzi za ukoloni, nadhani ile miaka ya uhuru ni uhuru wa kwenye makaratasi tu.
 
Waliochoka ni Watanganyika Katiba haina tatizo lolote

Kama mnawachagua akina Babu Tale hilo ni tatizo lenu Siyo Katiba 😀
Katiba ndyo inasema mbunge ajue kusoma na kuandika tu.

Matokeo yake ndiyo tunawapata hao wakina babu tale
 
Katiba ndyo inasema mbunge ajue kusoma na kuandika tu.

Matokeo yake ndiyo tunawapata hao wakina babu tale
Tatizo siyo elimu ni pale anaye pewa dhamana kuahirisha kufikiri kwa nafsi kwasababu ya kujipendekeza ama kutumikia kundi fulani kwa masilahi binafsi, na uoga kwa viongozi wake, a.k.a kujizima data, (unyumbu), human herding
 
Tatizo siyo elimu ni pale anaye pewa dhamana kuahirisha kufikiri kwa nafsi kwasababu ya kujipendekeza ama kutumikia kundi fulani kwa masilahi binafsi na uoga kwa viongozi wake
Kwa dunia ya sasa ni ngumu kupata kiongozi mzuri asiye na elimu, zama zimebadilika na dunia ni kama kijiji.
 
Katiba ndyo inasema mbunge ajue kusoma na kuandika tu.

Matokeo yake ndiyo tunawapata hao wakina babu tale
Kwani hao maprofesa huko Bungeni wamesaidia nini? 😄

Katiba imekupa upana mkubwa wa kumchagua Kiongozi
 
Kwani hao maprofesa huko Bungeni wamesaidia nini? 😄

Katiba imekupa upana mkubwa wa kumchagua Kiongozi
Maprofesa nao wamechagua kulinda matumbo yao na sio maslahi ya wananchi.

Katiba imetoa upana mkubwa bila kuzingatia kwamba kuna wakati utafika na dunia itabadilika, mambo mengi yatakuwa advanced.
 
Back
Top Bottom