Je, Tanzania bado inahitaji Rais kama Magufuli?

andoza

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
1,243
2,000
Kama ilivyo ada na kwa jinsi hali ya hewa ya siasa ilivyo kwa sasa ni wazi kabisa kwamba sasa ni Rasmi JPM ndiye mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM. Tunatambua kuwa JPM anayo nia, sababu na uwezo wa kuhakikisha kwamba anabaki madarakani katika kipindi kingine cha miaka mitano.

Mengi yamejitokeza katika kipindi cha miaka mitano iliopita ambayo kwa hakika yanatufanya Watanzania tujiulize tunataka Rais wa namna gani?

Kabla ya Magufuli kila mtu alitaka Rais kama Magufuli,kwa hakika tulitaka Rais ambaye ni mara mbili au tatu ya Magufuli,wengi walitaka Rais mwenye msimamo thabiti,mkali na anayesimamia haki na uwajibikaji. Kwa kiasi ametenda kwa kuzingatia matarajio hayo ingawa sio kwa kiwango tulichotarajia hakukaza ipasavyo,hakuwa na msimamo ipasavyo kuna maeneo ambayo bado alilega lega.

Kwa kuzingatia hatua iliyofikia katika maendeleo ya taifa letu na kwa kuzingatia changamoto tulizo nazo kama taifa na aina ya mabadiliko tunayotaka je Tanzania bado inahitaji Rais mwenye sifa kama za Magufuli?Kama jibu ni hapana je tunahitaji Rais mwenye sifa gani?Uwezo gani na haiba gani?

Ni maeneo gani ambayo tunahitaji mabadiliko ya kiongozi?Je, ni katika uhuru wa vyombo vya habari?Je ni katika siasa?Je, ni katika sera za uchumi, je ni katika huduma za kijamii?Je, ni katika miundo mbinu?Je, ni katika mahusiano ya kimataifa?Je, ni mabadiliko ya aina gani tunayotaka?Je, tunafikiri tunahitaji kiongozi mwenye sifa gani?

Tutoe maoni kwa uwazi kwa kuzingatia changamoto zilizopo,huku tukiwa na imani kwamba kiongozi atakayechaguliwa atazingatia hayo

Karibuni kwa mjadal
 

Kawe Alumni

JF-Expert Member
Mar 20, 2019
8,483
2,000
Watanzania 98% wanamuhitaji Rais Magufuli Wanaompinga Rais Magufuli ni mafisadi na majizi, wauza madawa ya kulevya na majangili.
 

fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
6,459
2,000
Kama ilivyo ada na kwa jinsi hali ya hewa ya siasa ilivyo kwa sasa ni wazi kabisa kwamba sasa ni Rasmi JPM ndiye mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM.Tunatambua kuwa JPM anayo nia.sababu na uwezo wa kuhakikisha kwamba anabaki madarakani katika kipindi kingine cha miaka mitano.

Mengi yamejitokeza katika kipindi cha miaka mitano iliopita ambayo kwa hakika yanatufanya watanzania tujiulize tunataka Rais wa namna gani?

Kabla ya Magufuli kila mtu alitaka Rais kama Magufuli,kwa hakika tulitaka Rais ambaye ni mara mbili au tatu ya Magufuli,wengi walitaka Rais mwenye msimamo thabiti,mkali na anayesimamia haki na uwajibikaji.Kwa kiasi ametenda kwa kuzingatia matarajio hayo ingawa sio kwa kiwango tulichotarajia,hakukaza ipasavyo,hakuwa na msimamo ipasavyo kuna maeneo ambayo bado alilega lega.

Kwa kuzingatia hatua iliyofikia katika maendeleo ya taifa letu na kwa kuzingatia changamoto tulizo nazo kama taifa na aina ya mabadiliko tunayotaka je Tanzania bado inahitaji Rais mwenye sifa kama za Magufuli?Kama jibu ni hapana je tunahitaji Rais mwenye sifa gani?Uwezo gani na haiba gani?Ni maeneo gani ambayo tunahitaji mabadiliko ya kiongozi?Je ni katika uhuru wa vyombo vya habari?Je ni katika siasa?Je ni katika sera za uchumi,je ni katika huduma za kijamii?Je ni katika miundo mbinu?Je ni katika mahusiano ya kimataifa?Je ni mabadiliko ya aina gani tunayotaka?Je tunafikiri tunahitaji kiongozi mwenye sifa gani?

Tutoe maoni kwa uwazi kwa kuzingatia changamoto zilizopo,huku tukiwa na imani kwamba kiongozi atakayechaguliwa atazingatia hayo

Karibuni kwa mjadal
Kamwe hatuhitaji rais mkabila, mbabe, dikteta, mbaguzi, muua demokrasia, mpenda mambo ya kienyeji na asiye na weledi wa uongozi. Tubadilishe October.
 

Kawe Alumni

JF-Expert Member
Mar 20, 2019
8,483
2,000
Tunapendekeza Rais ajaye awe na haiba km za Magufuli aendeleze ukuaji wa uchumi wa kati
 

mwayena

JF-Expert Member
Apr 21, 2016
2,878
2,000
Hatuhitaji kiongozi katili, muuaji, muongo,mnafiki, mwenye kufuru,mpenda sifa,mwizi na fisadi wa Mali ya uma ref..1.5 trl. Tunataka kiongozi mwenye sifa kinyume na hizo nilizoorodhesha
 

Edward Sambai

JF-Expert Member
Nov 16, 2013
2,459
2,000
Tunahitaji Rais anayeiheshimu na kuifuata katiba ya Jamuhuri ya Tanzania.
Tunahitaji Rais asiye mbaguzi kikabila, itikadi, kidini wala rangi.

Yeyote mwenye hizo sifa apewe kiti
 

VAPS

JF-Expert Member
Jul 10, 2012
4,043
2,000
Hali ya maisha ni ngumu sana mtaani. Sijui tunakosea wapi.Umoja na mshikamano wa taifa upo shakani. Hofu na mashaka vimetawala kada zote.
 

Fadhilim

Senior Member
Feb 3, 2013
173
225
Haihitaji tena Rais kama huyo, tunahitaji Rais ambaye ataheshimu mihimili mingine.
Sio kutoa kauli kwa mihimili mingine mfano kumwambia Spika wewe washughulikie huko bungeni, mimi nitawashughulikia huku nje.
 

sblandes

JF-Expert Member
Apr 25, 2010
5,098
2,000
Magufuli iwe isiwe,tunae hadi 2025.
Lakini ajifunze upendo, utu,na kuheshimu watu,ndio sifa kuu ya utanzania.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom