Je, tabia ya uongo kwa mwanamke ivumilike?

livewise1

JF-Expert Member
May 25, 2019
837
952
Habari!
Baadhi ya wanawake waongo waongo kwenye kutafta wenzi...baada ya kuwapata basi uhalisia wa mambo ukijulikana wanajitetea walitaka kupata huyo mpenzi ndio maana wakaongopa.
Lakini bado tabia za uongo uongo zinaendelea hata hivyo.
NB: huu uongo naozungumzia sio wa kupelekea usaliti.
Mfano anakuongopea babake anafanya kazi nje ya nchi...kumbe yupo hapo kariakoo anabiashara ya kuuza vifaa vya ujenzi...au yeye hana kazi kwa sababu hataki tu ila ana degree...badae unakuja kujua anayo kazi rasmi na alikuwa haombi pesa mpaka umtumie ukipenda...hata hivyo anaweza kukusapraizi na double ya pesa uliyompa ndani ya wiki hiyo hiyo!

-Hizi tabia zivumilike???
-haya hayawezi kuwa ni maandalizi ya matukio mengine makubwa???
Ushauri!!!
 
Bro vumilia tu km uchi anao ishi nae me mshikaji wangu kaongopewa mtoto ni wakishua kumbe kajamba nani na anaishi nae mambo yanaenda
 
Huo uongo unao uona wa kawaida jua ni maandaliz ya uongo mkubwa na wakutisha.

Maamuzi yapo juu yako
 
Bro vumilia tu km uchi anao ishi nae me mshikaji wangu kaongopewa mtoto ni wakishua kumbe kajamba nani na anaishi nae mambo yanaenda
Tatizo haijulikani ataacha lini uongo uongo.
Je, akija kuongopa mambo mengine ya hatari?
 
mbona na nyie mnatudanganyaga mnafanya kazi kwenye maofisi makubwa kumbe ni makuli tu.

tuvumiliane tu bro..

kama kakuotea na ww jitafte umuotee
Unajua uongo uongo [tabia] ndio shida.
Hujui utaongopewa dudu gani huko mbeleni.
Sisi wanaume tunaongopa mara moja tu ikibidi...lakini hatuna ile muendelezo wa kuongopa ongopa kila kitu.
Nyie wenyewe mkijuaga mwanaume muongo muongo mnaamsha popo.
 
Yaaan mkidanganya nyie ni kawaida, ila nyie mkidanganywa na uzi mnaanzisha. Kua mpole buddah
 
Habari!
Baadhi ya wanawake waongo waongo kwenye kutafta wenzi...baada ya kuwapata basi uhalisia wa mambo ukijulikana wanajitetea walitaka kupata huyo mpenzi ndio maana wakaongopa.
Lakini bado tabia za uongo uongo zinaendelea hata hivyo.
NB: huu uongo naozungumzia sio wa kupelekea usaliti.
Mfano anakuongopea babake anafanya kazi nje ya nchi...kumbe yupo hapo kariakoo anabiashara ya kuuza vifaa vya ujenzi...au yeye hana kazi kwa sababu hataki tu ila ana degree...badae unakuja kujua anayo kazi rasmi na alikuwa haombi pesa mpaka umtumie ukipenda...hata hivyo anaweza kukusapraizi na double ya pesa uliyompa ndani ya wiki hiyo hiyo!

-Hizi tabia zivumilike???
-haya hayawezi kuwa ni maandalizi ya matukio mengine makubwa???
Ushauri!!!
Mi nilidanganya alichaguliwa Harvard University kumbe ni form4 leaver aisee nilisikitika sana kujua ilo sema hawa viumbe ni waongo sana kuliko tunavyo thani.
 
mkuu seems unaumiza kichwa kwa mambo madogo mno.

hujatujua bado.

kitu kizito loading 🙊
 
Mi mwenyewe muongo mpka najiogopa nishawahi kuwa mlokole kuongozana kama kumbikumbi na mwanamke kisa mbususu nikipata muongo mjanja janja hata sishangai kikubwa najua nini nataka
 
Back
Top Bottom