mnyamiwono
JF-Expert Member
- Oct 7, 2012
- 708
- 71
Katika hali isiyokuwa ya kawaida mitandao ya kijamii hata magazeti pia, vyote vinazungumzia namna Chadema inavyohusika na swala la Ludovick anayedaiwa kuwa kada nguli wa chama, kuwa CDM wameshindwa au hawana nia ya kumsaidia atoke lupango pamoja na kuwa dhamana ya kijana huyu iko wazi, sasa ni vizuri tukajua ni kweli CDM wamemtelekeza? au mahusiano yake na chama yakoje? Nauliza haya kasababu imefikia wakati hata ludovick anaitwa kuwa alikuwa msaidizi wa Dr (matusi ya kisiasa) hii ni kweli jamani? Ushauri wangu ili kujenga sura endelevu ya chama inabidi mtu huyu aangaliwe ili asaidiwe na kama kuna kosa/sababu zozote zile zinazosababisha asisaidiwe basi watanzania wajulishwe ili kuondoa sintofahamu hizi na kukiokoa chama katika majungu ya wasiopenda amani na maendeleo ya demokrasia nchini kwetu.