Je Shirika Lako Linaaminiwa na Watu ?

Je Shirika Lako Linaaminiwa na Watu ?

Joined
Feb 5, 2022
Posts
44
Reaction score
65
1745450596009.png

Imani ya watu kwa Asasi za Kiraia imekuwa ikishuka siku hadi siku, si kwa Tanzania pekee, hata nje ya Tanzania. Tafiti iliyofanywa na Gallup and Wellcome mwaka 2022 inaonyesha kwamba asilimia 32 ya watu ulimwenguni wanakosa imani kwa Asasi za Kiraia nchini mwao. Sababu kubwa ya kushuka imani ya watu kwa Asasi za Kiraia ni ubadhirifu wa fedha zinazotolewa na wafadhili.

Tukio la 9/11, linatajwa kuwa ni miongoni mwa sababu kubwa iliyopelekea imani ya watu wengi ulimwenguni kushuka kwa Asasi za Kiraia. Hii ilitokana na kitendo cha Shirika la Msalaba Mwekundu (Red Cross) kutumia fedha zilizochangwa na watu mbalimbali kwa ajili ya wahanga wa shambulio la 9/11 kwa matumizi mengine, ijapokuwa baadae shirika la Red Cross lililazimika kuomba radhi, na kubadili matumizi ya fedha kwa kuzielekeza kwa wahanga kama wafadhili walivyotaka.

Sababu zingine zinazopelekea imani ya watu kushuka kwa Asasi za Kiarai ni;​
  • Kukosekana kwa Uwazi: Mapato na matumizi halisi ya Asasi za Kiraia yamegubikwa na usiri mkubwa. Ijapokuwa kwa mujibu wa sheria nchini Tanzania, Asasi zinapaswa kuwasilisha taarifa za utekelezaji wa miradi kwenye halmashauri na wizara,lakini taarifa nyingi zinazowasilishwa zinakosa uhalisia​
  • Kukosekana kwa Ufanisi: Asasi inaposhindwa kutumia kikamilifu rasimali zake katika kutekeleza shughuli zake, inapelekea kukosekana matokeo na mabadiliko ya kweli kwa jamii, hivyo kufanya watu kukosa imani nayo.​
Madhara ya kushuka kwa imani ya watu kwa Asasi za Kiraia
Imani ya watu inaposhuka kwa Asasi, madhara yake ni mengi na yanaweza kuharibu mustakabali mzima wa Asasi. Miongoni mwa madhara hayo ni kama ifutavyo;​
  • Kupungua kwa ufadhili. Mfadhili anapokosa imani na Asasi, anagubikwa na mashaka juu ya matumizi ya fedha zake kwa Asasi, hali hii inampelekea kupunguza kiasi cha fedha au kuondoa kabisa ufadhili wake kwa Asasi.​
  • Kukosa Washirika. Ushirika miongoni mwa Asasi ni nyenzo muhimu kwenye utafutaji wa rasilimali kwa ajili ya utekelezaji wa miradi na programu. Asasi inapokosa imani ya watu, taswira yake kwa jamii inaharibika kiasi cha kupelekea kukosa mshirika.​
  • Ukaguzi wa Asasi. Imani ya watu inaposhuka juu ya Asasi, ni rahisi mamlaka zinazohusika na usimamizi wa Asasi kuwa na mashaka na Asasi husika na hatimae kufanya ukaguzi.​

Nini kifanyike Ili Watu wawe na Imani na Asasi za Kiraia​
  • Uwazi na Uwajibikaji. Asasi zinapaswa kuwa wazi namna zinavyoendesha shughuli zao. Kwa mafano uwasilishaji wa taarifa za utekelezaji wa miradi kwa wadau, kufanya ukaguzi wa hesabu, kuwa na mfumo wa wazi wa kufanyaji maamuzi n.k.​
  • Kuwa na Bodi ya Wakurugenzi (yenye meno). Bodi ya wakurugenzi ina jukumu la kuisimamia “management” juu uendeshaji wa Asasi. Kunapokuwa na bodi yenye nguvu na iliyo huru, ni rahisi kuisimamia “management” na kupekelea Asasi kufanya shughuli zake kwa kufuata utaratibu.​
  • Ushiriki wa Wadau. Wadau ni watu walio na maslahi, ushawishi na umuhimu kwa Asasi. Kuwashirikisha wadau kwenye maamuzi kutapelekea Asasi kukidhi mahitaji ya wadau wake na hatimae kujenga imani ya watu kwa Asasi.​
  • Kujenga Uhusiano na Jamii: Asasi zinapaswa kujenga na kudumisha uhusiano mzuri na jamii.​
  • Elimu na uhamasishaji. Asasi zinapaswa kuendeleza kampeni za elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa asasi za kiraia na faida zake katika maendeleo ya jamii. Hii itaondoa mitazamo hasi na kwa kuwakumbusha watu kwamba asasi zina uwezo wa kutatua matatizo wanayokumbana nayo.​

Article By;
OMAR MSONGA
CONSULTANT
Project Management, Strategy, Fundraising & Training
For Consultation Service; Call +255 719 518 367 or
Email: msongatheconsultant@gmail.com
Dar es Salaam
TANZANIA​
 
View attachment 3313671

Hii kwa wajasiriamali itafaa
 
Back
Top Bottom