Kuna mahali nimesema anayofanya JK kwa sasa ni mazuri??
Ulisema kuna sababu maalumu iliyomfanya afanye hayo na mimi nimekwambia wazi kuwa ulisema kuna motives nyuma yake.
Sikupenda utawala waJK uliojaa rushwa na utendaji kazi legelege wa wa wakati wa JK bali nilipenda yeye alivyoachia angalau uwanja mpana wa demokrasia
So mkuu
Kwako utawala wenye rushwa, ufisadi wa kutisha na ulaji wa mali za umma ni bora ikiwa tu democracy ipo open tu??
Kumbuka JK mwishoni mwa utawala wake ndio upinzani ulianza kupata nguvu kubwa kwahiyo wakati wake hakupata kash kash yoyote kama JPM aliyoikuta ambayo ni mbegu iliyopandwa na kikwete kwa hizo hizo rushwa, ufisadi na mengine mengi sasa kwanini wasilaumiwe?
hata hivyo nafahamu pia upinzani wa 2005 na 2010 haukuwa na nguvu kubwa kiasi cha kutishia urais wake na bunge la chama chake kwa hiyo huenda ni sababu mojawapo hatakuweza kuiona sura yake halisi pia)
Na huu ndio ukweli halisi uliosema JK aliona upepo mapema akaona inatosha na kuwapa mzigo wengine ambao aliupanda mwenyewe kwa mikono yake kwani JPM alipoingia madudu mangapi aliyakuta?? JK anatakiwa kulaumiwa kwa kutufikisha hapa hata iweje
Sikuukubali sana utawala wa jiwe kwa sababu mimi kwangu ujenzi wa miondombinu sio kipaumbele kikubwa zaidi mbele ya demokrasia na approach inayatomukia. Siamini miondombinu iliyojengwa na Hitler Ujerumani au Makaburu Africa Kusini ilikuwa ni gharama sahihi ya mateso kwa binadamu wengine, siamini miondombinu iliyojengwa Ethiopia wakati wa Zenawi ilihalilisha gharama kubwa ya mateso makubwa kwa binadamu wasio na hati.
Huenda upo sawa mkuu lakini let me say this
Kwako concept ya maendeleo ni unaitafsiri vipi??
Tukisema neno maendeleo unapata concepts ngapi humo ndani?
Huenda kwako maendeleo ni democracy tu mengine kwako sio sawa ila maendeleo tutayapima kwa
Uchumi wa taifa na mtu mmoja mmoja kitu ambacho hatujafikia
Kijamii pia kitu ambacho hatujafikia sawa sawa sababu kila siku jamii inaporomoka kimaadili
Politically..hapa ndipo unagusia wewe kwamba democracy pekee inatosha kuwavusha watu nchi ya ahadi kama ikifatwa vyema ila bado pia wakati wa kikwete tulikuwa na hali ya kawaida tu ya kiuchumi hakukuwa na tofauti kubwa mpaka sasa ya maisha
Yalikuwa yale yale tu tofauti nj kuwa JPM hakutaka democracy ya maridhiano na upinzani wakati kikwete aliruhusu..
Asante