Je shida ni wale tuliowapa mamlaka ya kuenforce na kusimamia sheria zetu kutojitambua au shida ni sisi wadanganyika?

Sijijui

JF-Expert Member
Jan 14, 2018
7,879
8,800
Wana jamvi,

Tangu awamu ya tano iingie madarakani, kumekuwa na malalamiko mengi ya wafanyakazi kuondolewa kwenye nafasi zao kinyume cha sheria na wengine kuteuliwa kushika nafasi mbalimbali kinyume cha sheria na taratibu pia.

Mambo haya kwa wengine inaonekana ni sawa tu. Sasa swali langu ni kuondolewa watu wengine kwenye nafasi zao kinyume cha sheria na taratibu inaonekana ni sawa, lakini kuondolewa au kutenda matendo kwa utaratibu huo huo wa kutokufuata sheria na taratibu yanayoweza kupelekea kumuondoa Rais madarakani. Rais anayevunja sheria na taratibu alizoapa kuzilinda inaonekana au kutofasiriwa kama ni uhaini?Je huu upendeleo wa kisheria unatokana na nini?

Je shinda ni wale tuliowapa mamlaka ya kuenforce na kusimamia sheria zetu kutojitambua au shida ni sisi wadanganyika?

Msaada tafadhari
 
Wee jamaa , asubuhi yote hiiii kweli, LEO ijumaa bnana, ngoja tukaswali kwanza.
Ni kweli mkuu ila hii issue inanisumbua sana mkichwa,unfortunately sheria ilinipita pembeni,najua tu definition ya law of tort
 
Mimi nalia na tiss tu, wanasema wako kwa maslahi ya nchi sasa sijui nchi gani hiyo, maana mi naona wapo kwa maslahi yao tu.
 
Back
Top Bottom