Je, Rwanda wanaweza kutusaidia kiteknolojia?

Cha Ajabu lipi wakitoka Rwanda?Hushangai au kuafiki mbegu ya mchikichi kuchukuliwa Tanzania kwenda Malaysia na Nchi hiyo ndiyo inaongoza uzalishaji Duniani.!Hebu acheni hizo hii ni AFRIKA MASHARIKI,Sie hadi pale tutabadili huyu VIRUS aliyetufamia Watanzania na kuacha Uaminifu na Uadilifu sehemu zetu za kazi.Na hili kama hatutajirekebisha kama Taifa itakuwa kila leo tunakosolewa na hayo mapungufu na tunalo kama luba.Tubadilike
 
Acha wanyarwanda waje tu, maana sisi tumezidi wizi wizi, ukipata nafasi badala ya kufaya kazi kwa weredi unakuwa unatafuta deal za kuiba tu ujitajirishe mwenyewe, hukuona kipindi kilichopita cheki moja ikilipwa bank inatoa makonteina na ya watu wengine, waliokua wanafanya haya hawakuwa watanzania?, sasa tunakuja kuonyeshwa njia ya kufanya kazi kwa weredi tunaanza kupiga kelele, je wizi uliokua unafanyika uendelee?
 
Labda kwa sababu huwa haitangazwi sana kwani mifumo ya IT, Umeme etc huwa inafungwa na nani Tanzania? Jibu ni kwamba mifumo na mitambo mingi Tanzania inafungwa na Wazungu, Wahindi, Wachina, etc na watanzania huwa tunabaki kusimamia hiyo mifumo/mitambo na ikiharibika tunawaita kuja kutengeneza, Mbona hatujawahi kulalamika? Au kwa sababu anakuja kufanya hiyo kazi ni Mwafrika mwenzetu? Rais angeomba Marekani watusaidi kufunga huo mfumo tungelalama humu?
Ndio maana napenda Donald Trump ashinde kwa sababu anaongea ukweli juu ya sisi waafrica tulivyo, Hili lilikuwa jambo la kujivunia kusaidiwa na Mwafrika mwenzetu yaani tumtegemee mchina ndio tumuamini sana,
Tuendelee kupiga bla bla tu na porojo maendeleo tutayasikia kwa majirani.
 
Lowassa wenye chama hatumtaki. Na suala la UDSM kuzalisha wezi watu hawasemi. Ila si mbaya kuchukuwa kizuri kutoka sehemu nyingine na si kuwa tunachukuwa watalaam bali utalaam wao.

Sawa na sera zetu huwa zinatumika nchi nyingi sana ingawa kwetu tunashindwa kuzifanyia kazi kwa sababu za wezi wale wale
unachama gani wewe booya labda chama cha wapiga puri.

swissme
 
Kwan tatizo lipo wapi mpaka Rwanda washindwe kutusaidia??Waje tu hakuna namna
 
Kwa wale ambao hamjasoma haya masomo ya Teknolojia ukweli ni kwamba hata ufundishwe na maprofessor elfu moja wazuri ukitoka huwezi kufanya kitu cha maana kama hujafanya training za kutosha specifically kwa kazi unayotaka kufanya specific kazi flani bado huwezi kujiita unajua kitu, ndio maana makampuni binafsi yana utaratibu wa kuwatrain wafanyakazi wake kila teknolojia mpya inapokuja, Kagame ana utaratibu wa kupeleka wanafunzi wake kusomea mambo flani kwenye nchi ambazo zimebobea kwenye mambo flani na wanarudi wanafanya walichotumwa, ila sisj huku mtu akimaliza elimu ya darasani UD labda IT au Telecom basi anadhani anaweza kufanya kazi lazima tuwe na utaratibu wa kuchukua vijana wakajifunze zaidi juu ya masuala tunayotaka kwenda mbele.
 
Kuna vingine ukivisikiliza kama una akili unaishia kucheka na kupuuza. Eti Rwanda itatusaidia wataalamu wa kufufua shirika letu la Air Tanzania, na kwamba Rwanda italeta jopo la wataalamu wa teknolojia ili tuweze kujifunza kwao. Yani Tanzania ijifunze "technology" Rwanda. Hahahah.!

Binafsi naipongeza Rwanda inavyojitahidi kupiga hatua za maendeleo kwa kasi tangu kumalizika kwa mauaji ya kimbari mwaka 1994. Imeweza "kurecorver" ktk kipindi kifupi na kuzipiku nchi nyingi za Afrika kwa maendeleo ya kiuchumi, ikiwa ni pamoja na kuimarisha sarafu yake. Hili ni jambo la kupongezwa.

Lakini kusema Rwanda inakuja kutusaidia kwenye maendeleo ya Sayansi na Teknolojia ni kichekesho kikubwa kuliko "comedy za Mr.Bean". Inakuja kusaidia nini kwa mfano?

Wataalamu wa kwanza wa TEKNOHAMA nchini Rwanda (hao ambao serikali ya CCM inawasifia) ni zao la mwaka 2001. Sijui kama unanielewa? Ni hivi; Rwanda kwa mara ya kwanza imezalisha wataalamu wa TEKNOHAMA kutoka nchini humo mwaka 2001. Idara ya Sayansi na Teknolojia ya Chuo Kikuu cha Rwanda ilianzishwa mwaka 1997, na ikaanza kuzalisha wataalamu miaka minne baadae.

Wakati Idara hiyo inaanzishwa mwaka 1997, Tanzania ilikua imeshazalisha maelfu ya wataalamu wa TEKNOHAMA wengi wakifanya kazi katika taasisi mbalimbali nje na ndani ya nchi.

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na vyuo vingine vya daraja la kati kama DIT, Mbeya Tech, na Arusha Tech vilikua vimeshazalisha wataalamu wengi sana wa Sayansi na Teknolojia. Yani wakati tukiwa na Maprofesa kadhaa wa mambo ya sayansi na Technolojia, Rwanda hawakua hata na chuo kimoja chenye hadhi ya VETA kinachofundisha technology. Leo tunaambiwa watakuja kutufundisha. Maajabu.!

Nadhani sisi ndio tunapaswa kuwafundisha wao, maana tuna wataalamu wengi kuliko wao. Tuna vyuo vingi vya sayansi kuliko wao, tuna "facilities" na "institutes" nyingi zaidi za technology kuliko wao. Hata Chuo kukuu cha sayansi na Technolojia cha Nelson Mandela kinachotegemewa na nchi zote za SADC kipo Arusha, Tanzania. Sasa Rwanda wanakuja kutufunza nini?

Hata aliyekua Mkuu wa chuo cha Teknolojia Rwanda (KIST), Professor Silas Lwakabamba inadaiwa ni mtanzania na amesoma Chuo Kikuu cha Dar (UDSM), kabla ya kuhamia Rwanda. Baadae Rais Kagame akampa Uraia wa Rwanda na akamteua kuwa waziri wa sayansi na teknolojia.

Wakati Tanzania inaanzisha Shirika la Ndege (Air Tanzania) mwaka 1977, Rwanda walikua wakipanda mabasi, na "matoroli". Walikua wakiona muujiza ndege zetu zikiruka kwenye ardhi yao zimeandikwa "Air Tanzania".

Iliwachukua miaka 25 kuanzisha Shirika lao la "Rwandan Air" (mwaka 2002).

Lakini kwa sasa Rwandan Air ina ndege 16 zinazoruka mataifa mbalimbali duniani, while Air Tanzania ina ndege moja mbovu isiyoweza hata kuruka kutoka "Mabibo hostel" hadi "Pugu Kajiungeni."

Ukweli ni kwamba tuliwatangulia Rwanda ktk maendeleo ya Sayansi na teknolojia lakini kwa sasa wametuacha nyuma. So ni vizuri kuangalia tumejikwaa wapi. Je, tatizo ni wataalamu? Ni fedha? Ni utaalamu au kitu kingine? Kujua chanzo cha tatizo kutasaidia kutafuta "solution" ya kudumu. Lakini tukijidanganya kwenye chanzo cha tatizo hata "solution" tutakayopata itatudanganya, na tutashindwa kuondokana na tatizo.

#Je_Tatizo_Ni_Teknolojia?
Katika ukanda wa Afrika Mashariki, Tanzania inaongoza kwa teknolojia ktk mambo mbalimbali. Hata ktk usafiri wa anga Tanzania ndio yenye "Radar" ya kisasa kuliko nchi nyingine za EAC.

Lakini hata kama shida ingekua technology bado isingekua tatizo kubwa kwa sababu teknolojia inanunulika. Tunaweza kununua teknolojia China, Israel, Marekani etc na tukaiadopt. Inategemea tunakaka technology ya nini.

#Je_Tatizo_ni_Wataalamu?
Tanzania ina wataalamu wengi sana wa masuala ya Sayansi na Teknolojia. However wataalamu wanaweza kutengenezwa. Tunaweza kuchukua raia wetu tukawapeleka nje ya nchi kujifunza na utaalamu watakaoupata wakaja kuutumia kuisaidia nchi.

#SWALI
Ikiwa tatizo si wataalamu, si fedha wala si technology je tatizo ni nini?

#JIBU
Tatizo letu kubwa ni utashi wa kisiasa (Political will). Bado hatujapata viongozi wenye utashi (nia ya dhati) ya kutaka kuiona Tanzania ikipiga hatua ktk sekta ya sayansi na teknolijia.

Either hatuna viongozi wenye utashi wa kisiasa, au wana utashi lakini hawajui njia gani watumie.

Nitakupa mifano michache. Mwaka 2013 kijana mmoja mkoani Arusha alitengeneza Helkopta kwa kutumia Injini ya pikipiki. Helkopta hiyo ilikua na uwezo wa kuruka mita 200 angani na kutua. Hakuna juhudi zozote zilizotumika kumuendeleza kijana huyu.

Mwaka 2014 kijana mwingine mkoani Geita baada ya kuhitimu kidato cha 4 aliweza kutengeneza mfumo wake wa masafa (waves) ambapo watu waliokua mita 500 waliweza "kumsearch" na kumpata kupitia radio zao. Kijana huyu hajulikali alipo kwa sasa.

Mwaka 2008 mmoja wa vijana walioingia "top ten" kitaifa kwenye matokeo ya kidato cha sita, akipata daraja la kwanza (points 3) mchepuo wa PCM, (jina nalihifadhi) kwa sasa anafanya biashara ya kununua na kuuza magari (chakavu). Licha ya ufaulu mzuri aliopata lakini serikali haikua na mpango wowote wa kumuendeleza ili aweze kuisaidia nchi baadae. Akaenda chuo kikuu kusomea "uhandisi" akamaliza akakaa mtaani bila kazi kwa muda mrefu, saivi kaamua kupiga "deiwaka" ya magari. Ananunua gari anakaa nalo anauza kwa bei ya juu kidogo (apate hela ya kula) ananunua jingine.

Haya ndio maisha ya mtu aliyepata alama "A" masomo yote kidato cha sita. Wakati Israel mtu kama huyu angekua ameendelezwa na serikali na kwa sasa angekua anatumika kwenye idara nyeti, lakini hapa kwetu tumeruhusu auze magari chakavu. Halafu bado tunadhani shida ya nchi yetu ni technology. Huu ni uzwazwa.

Bado hatujajua thamani ya wataalamu wetu. Hakuna utashi wa kisiasa wa kuwafanya wataalamu wetu kuwa "productive and potential" kwa nchi.

#Kwanini_Rwanda_wanafurahia_kutusaidia?

Rwanda wana akili sana. Wametusoma na wamejua shida yetu si teknolojia wala si wataalamu. Lakini wamekubali ombi la kutusaidia kuleta teknolojia na wataalamu. Kwanini?

#JIBU:
Rwanda wamegundua hatujui shida yetu ni nini. Tuna matatizo lakini hatujui "solution" yake. Tunadhani "solution" ni wataalamu au ni teknolojia. Tunatapatapa. Kwahiyo Rwanda wanaitumia fursa hiyo vzr.

Rwanda wanajua shida yetu si wataalamu wala si teknolojia. Lakini wamekubali kutusaidia kwa sababu wamegundua hatujui tatizo letu ni nini. Hivi kama kweli shida yetu ingekua technology tungeacha kwenda kutafuta technology China, Urusi, Marekani, Israel tukatafute Rwanda? Kwa technology ipi ya kina "Ndaizeye"?

So wanyarwanda wameshajua kwamba "hatujielewi" kwahiyo wanaweza tumia fursa hiyo kutuletea wataalamu wa kutufundisha technology "butu", wakati huo wakitumia fursa hiyo kupeleleza mambo mengine yatakayowanufaisha.

Maana yake ni kwamba "wataalamu wa Rwanda" watakuja lakini hatutaona changes zozote kwenye "technology" kwa sababu shida yetu si wataalamu. Tukija kushtutuka na kujua shida yetu, Rwanda watakua washatufaidi vya kutosha.

Ikumbukwe hata Rwanda shida yao haikua "technology" wala wataalamu. Shida ilikua "political will". Utashi wa kisiasa wenye nia ya dhati ya mabadikiko. Hatimaye wakampata Kagame mwenye utashi wa kisiasa, ambaye amewasaidia sana kukua kiuchumi.

Lakini Rwanda hata wangeleta wataalam wote wa teknolojia wa chuo kikuu cha "Havard" bado wasingepiga hatua yoyote kama wangekosa mtu mwenye "good political wiil" (utashi wa kisiasa).

Kwa hiyo Tanzania ili iweze kupiga hatua kiteknolojia na sekta nyingine hatuhitaji kuleta wataalamu kutoka Rwanda wala Congo DRC. Tunahitaji jambo moja kubwa. Utashi wa kisiasa.

Na utashi wa kisiasa wenye tija ni unaoletwa na mfumo, sio unaoletwa na kiongozi mmoja. Rais Obama aliwahi kusema Afrika haihitaji "watu imara" bali taasisi/mifumo imara." Nchi ikiwa na mfumo imara hata kiongozi akifa mfumo huo utaendelea kufanya kazi. Lakini ikiwa na kiongozi imara bila mfumo imara, siku akitoweka kila kitu kinatoweka. #Tafakari.!

Malisa G.J
Wazo zuri kazi kwenu viongozi
uko sahihi
 
Shida kubwa waliyo nayo watz ni altitude ukisoma vzr aliyoandika mleta mada hata wachangiaji wengine utabaini elements za bad atitude! unaweza kuwa vyuo vikuu hata kwny kila wilaya au hata many governance and civil society institutions lakin bado nchi ikawa maskini..lets look on hard things to detect, siyo habari ya uwingi wa vyuo na uwingi wa wasomi..maendeleo needs more than that!
 
Kwani hujui huo utaalam tuliwapa sisi? Unaanzaje kumfundisha mwalimu wake?
Fikira za kijinga sana hizi. Sina maana aliyeziandika ni mjinga bali kwa asili yake zinaujinga wa PHD. Hivi ukimfundisha mtu unakuwa umemkataza asijiendeleze!!! Hapo ulipo unayo maarifa kuliko mwalimu aliyekufundisha chekechea au hata shule ya msingi. Sasa unataka naye aendelee kukudharau kiasi cha kutohitaji taaluma yako imsaidie. Wanyarwanda wamejifunza kwetu kisha wamejiendeleza na kubobea kiasi cha kuunda mfumo wa kukusanya mapato wenye tija kwa serikali.
 
Huo utaalam rais aliwahi kuomba msaada kwa wataalamu wetu kama Stefano Mtangoo akaambiwa hawawezi kuunda mfumo huo?
Anaweza. Muda hauko upande wetu ndio maana unachukuliwa mfumo uliotayari unafanya kazi na changamoto zake kutatuliwa. Kwa kujua hili bado nchi inahitaji mifumo mingi tu wawe wamepata hii changamoto na kujibidisha kuunda mifumo mingine zaidi au hata kuuboresha huu uliopo ukaingiza vitu vingine ambavyo Wanyaruanda hawakuweka.
 
...Rwanda wanawasaidia sana...wakati wabongo mnahangaika na kufanya mambo manually....mithili ya hata kusitisha kabisa suala la kuwajali watumishi kimaslahi(kama kuwaandisha madaraja ama ajira mpya..ama kuwahamisha)...wenzenu Rwanda wameacha mambo ya manual work na sasa wanashughulika na kitu kinachoitwa..."Internet of things"...Nendeni Rwanda mkajifunze haya...
 
Tukichukua watalamu wa nje ya nchi ina maana kwamba sisi hatujui,hatuaminiki.....sasa najiuliza kama serikali haituamini nani atatuamini?.....
 
Unajipendekeza!!!
CQnPIquVAAEYPiY.jpg

swissme
 
Back
Top Bottom