Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 360,096
- 828,932
Refer mada ya kwanini watu wengi hufa usiku
Kuna maelezo na justifications za kisayansi kuhusu watu kufa usiku ambazo hata hivyo hazitoi majibu kwa asilimia mia moja.
Tunaishi katika dunia mbili (ulimwengu) tuna ulimwengu wa roho na ulimwengu unaoonekana... Ulimwengu wa roho ndio ulimwengu halisi na pumzi/uhai wa ulimwengu unaoonekana.
Chochote kinachotokea kwenye ulimwengu unaoonekana asili na chanzo chake ni ulimwengu wa roho.
Mwili kwenye ulimwengu wa roho hujilinda na chochote kibaya hasa pale inapotokea vita ya kiroho. Lakini kuna wakati mwili kupitia nafsi roho huamua kujidhuru yaani kufanya lolote lenye madhara kwa mwili mfano matumizi ya vilevi, ama kutouhudumia mwili na hata kujitoa uhai.
Kinachotokea kwenye ulimwengu unaoonekana ni replica ya ulimwengu wa roho! Mtu anapoamua kujinyonga, huyu anakuwa na utashi katika nafsi na ufahamu wake wa kile anachofanya!
Kwenye ile mada ya makutano ya kiroho , tunaona kwamba binadamu anapolala, utashi na ufahamu wake huenda mapumzikoni (dormancy/ muted state) ni kipindi hiki ambapo roho huchukua mikoba yote.
Ni kipindi hiki ambapo roho huivinjari dunia huko na huko, kwenye mabaya na mazuri, kwenye misitu yenye wanyama wakali, kwenye ajali, kwenye vita nk nk... Roho yako hukutana na kupambana na yote hayo.. Kumbuka ndoto nzuri au mbaya unazoota kila siku usingizini.
Roho inapokuwa huko na kupata ajali yoyote mbaya huwa hairudi mwilini.... Kinachotokea hapo ni kifo cha usingizini! Lakini pia roho huweza kujipeleka yenyewe kwenye shida ama vita isiyoweza kushinda na kujeruhiwa kabisa
Vile vile roho huamua yenyewe kuondoka na kutorejea tena mwilini (dhana ya kujinyonga).
Kwakuwa roho ni kitu kisichokufa, hivyo tunaposema kifo cha roho ni roho yenyewe kutorejea mwilini.
Kuna vichoo pia husababisha roho kujitenga na mwili na hapa ndio ushirikina na uchawi vinapoingia.
Kwamba unatumiwa roho nyingine iifukuze roho yako mwilini.... Matokeo yake ni kifo lakini daima kikiwa ni kifo chenye walakini.
Wafao usingizini ni matokeo ya roho zilizoenda kuvinjari dunia na zikashindwa kurejea ngamani.