Dalton elijah
JF-Expert Member
- Jul 19, 2022
- 780
- 1,831
Rais Samia!
Unateua makada wa CCM, waliotumikia serikali ya CCM, waliokuwa wateule wa Rais ambaye ni Mwenyekiti wa CCM, wanaolipwa pensheni na serikali ya CCM, ambao ni 'askari wa akiba wa CCM na serikali yake; unawafanya wajumbe wa tume uliyoiita Tume Huru ili ichunguze matukio ya uvunjifu wa amani kile kipindi cha Uchaguzi Mkuu wa 29 Oktoba 2025?
Unataka hiyo Tume ikachunguze matukio yale yaliyokuwa na baraka za Mwenyekiti wa CCM? Unataka hiyo Tume ikachunguze matukio yale yaliyokuwa na baraka za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania? Unataka Tume hiyo ikachunguze matukio ambayo CDF au Mkuu wa Majeshi alisema waliofanya matukio yale ni wahuni?
Unataka Jaji Mkuu mstaafu akachunguze yale matukio ambayo yamechangiwa na hasira za wananchi kutokana na mahakama ilipokuwa chini yake na chini ya majaji wakuu waliofuata kuhusu haki za kizchaguzi haikufanya?
Unataka Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu naye akachunguze mambo ambayo yamefanyika na huenda pia yakamgusa Katibu Mkuu Kiongozi aliyepo?
Unataka Luteni Jenerali akamchunguze CDF au Jenerali wake?
Unataka IGP (Mkuu wa Jeshi la Polisi) mstaafu akamchunguze IGP Wambura?
Unataka Dkt. Stergomena Tax, uliyemtoa huko nje na kumteua kuwa Waziri na baadaye waziri wa Ulinzi akachaichunguze Wizara ya Ulinzi?
Unafikiri kwa umri aliokuwa na Balozi Kapya (mzee wetu wa Kanisa wa zamani) akafanye nini katika hiyo Tume?
Ni kweli Mheshimiwa Rais unataka watu hao waje wakuchunguze wewe? Dada zangu enzi zile wakicheza 'rede' walikuwa wakisema 'po'!
Naomba nikuambie 'po' Mheshimiwa Rais, na baada ya kukuambia, 'po'; sasa naendelea!
Huku 'kitaani' watu wamekuchikia kupindukia! Hao waheshimiwa wanaokuzunguka hawawezi kukueleza usoni, lakini baadaye wakiwa katika vifua vya wapendwa wao hunong'ona! Wakija kwetu wachungaji, mapadri na maaskofu kwa ajili ya kupata vitubio wanaropoka yote! Ila sisi tuna viapo vya kutokutoa siri zao.
Ungetaka ushauri wetu, tungekushauri haya yafuatayo: Waite viongozi wa dini (wa Kanisa na Mskiti) wote wakiwemo hata ambayo wewe usingependa kuwaona. Sikiliza ushauri wao. Baada ya hapo, waite Marais wastaafu wa nchi zilizo na Urafiki wa muda mrefu na Tanzania na majirani kama Afrika Kusini, Msumbiji, Kenya, Nigeria, Ghana, Malawi, Namibia, nk. Sikiliza pia ushauri wao. Waite wazee wetu kama Warioba, Prof. Mwandosya, Askofu Sendoro, nk.
Wote hao wasikilize ushauri wao kabla ya kuipa majukumu hiyo Tume. Waite wakuu wa Idara ya Usalama wa awamu za nyuma walio hai na hao pia uwasikilize. Watanzania wakiona juhudi hizi na moyo wako wa kupondeka watakusamehe na watawasamehe pia wenzako. Watanzania wana orodha ya watu wanaowachukia - sio siri mheshimiwa!
Watanzania hawajamalizana na wewe kuhusu suala zima la uhalali wa uchaguzi. Tungejadili hilo kwanza ndipo tuanze haya mengine. Kwa hiyo, sisi Askofu Mwamakula tunashauri sana hilo suala la Tume aliyoiunda lisitishwe kwanza hata kama umelifanya kwa mujibu wa sheria na katiba. Lakini kinachogomba hata sio herufi za kwenye vitabu vyetu vya sheria, bali ni uhalali.
Tume hii ikianza kufanya kazi hata kama itatoa ripoti, ripoti hiyo haitakubaliwa na Watanzania. Sisi Askofu tumeona tukuambie haya yaliyopo katika 'moyo wa dhamiri' ya jamii na 'kifua cha dhamiri' iliyo kuu! Tunajua kuna uwezekano na tena mkubwa watu wako wakatusagia meno!
Lakini hata kama watatuua kama walivyowaua wengine, Kiti cha Urais wa Tanzania kitakuwa kimeambiwa ukweli. Hii ni dhamira ya kutaka kukiepusha au kukiokoa Kiti cha Urais kutoka katika hii 'najisi' iliyolikumba taifa. Lakini tunao uhakika kuwa 'kanzu' bado inaweza kushonwa upya hata viraka visionekane.
Sisi tulitarajia ya kuwa Tume ya Jumuiya ya Madola ungepewa muda huenda ndiyo ambayo ingefanya hayo majukumu kwa kuwa yenyewe haijalaumika ingawa na yenyewe inahitaji pia kujenga imani kwa Watanzania.
Sisi hatutaomba msamaha kwa kukusema pia hadharani wakati watu walio na heshima zaidi kuliko sisi wamejipanga kukusifia! Tuache sisi tunuke lakini tukijua ya kuwa tulisema yale yote ambayo Mkuu alitakiwa kujua kutoka kwa watu wake wengine walionuna (Ezekieli 33:1-20). Na sasa baada ya kuyasema hayo tunajimimina mbele ya Kiti cha Rehema cha Mungu kama ile sadaka ya kuteketezwa! Ikimpendeza yeye aliye juu atupokee sasa na ikiwa ni kwa mapenzi yake basi tuishi kuyaona yaliyo mbeleni! Amina
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Itunge, Dar es Salaam; 18 Novemba 2025; Saa 12:00 jioni.