Je Raisi asipotimiza wajibu wake anaweza kushtakiwa?

Gamba la Nyoka

JF-Expert Member
May 1, 2007
7,022
9,291
katiba inasema ,huwezi kumshitaki raisi kwa makosa aliyoyafanya wakati akitekeleza wajibu wake kama raisi, lakini je iwapo hatatekeleza wajibu wake kama raisi anaweza kushitakiwa?
mfano nchi imevamiwa na wananchi wanauawa lakini raisi akaacha kuamuru vyombo vya usalama kuwalinda wananchi je hapa raisi anaweza kushitakiwa?

au je raisi asipowachukulia hatua watu wanaohataisha uchumi wa Taifa(kwa sasa jina maarufu ni Mafisadi),je anaweza kushitakiwa kwa kutokutimiza wajibu wake?

je kwa hayo niliyoyataja hapo juu, ni makosa ya kuvunja katiba?. kwamba raisi asipotimiza wajibu wake wa (1):kuwalinda wananchi
(2):kulinda mali zao, atakuwa amevunja katiba na hivyo ashitakiwe?
 
Unaweza Kumshitaki Mtu Wowote Asiyetimiza Wajibu Wake Kama Mna Makubaliano Maalumu Ambayo Wote Wawili Mumesoma Makubaliano Hayo Na Kutiliana Sahihi Pamoja Na Mashahidi Au Kikundi Cha Watu

Kwa Jk Je Watanzania Wana Mkataba Gani Nae ? Ccm Wanamkataba Nae Gani ? Je Huo Mkataba Uko Wazi Kila Mtanzania Ausome Ili Wajue Wamemkabidhi Jk Majukumu Gani Ya Yapi Hajatekeleza ?

Hapo Ndipo Kulipowekwa Kofuli

Hakuna Kushitaki
 
Back
Top Bottom