Je, Rais wa awamu ya 6 aje na mkakati gani kama waliomtangulia wamefanya haya.?

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,109
18,326
Julius Nyerere :
Kuwaunganisha watanzania kupitia kiswahili na ujamaa ili kuondoa matabaka na ubaguzi wa kikabila, dini na rangi.

Ali Hasani Mwinyi:
Biashara huria , Sekta binafsi zikapata uhuru wa kufanya biashara.

Benjamini Mkapa:
Ubinafshaji wa mashirika ya umma na kuruhusu uwazi katika utendaji wa serikali.

JAKAYA kikwete:
Uboreshaji wa demokrasia, Elimu na kuwaongezea wananchi kupata access za fedha, mawasiliano na kula bata.

Joseph Magufuli:
Ujenzi wa miundombinu na majengo ya Serikali.

Rais awamu ya sita? Kwa hali ilivyo sasa kamamitaendelea hadi 2025.. Je Rais wetu wa awamu ya sita atatakiwa kujikita kwenye agenda ipi ili nchi ifike inapo stahili kufika?

IMG_20200528_225250.jpeg
 

Attachments

  • FB_IMG_1590922168583.jpeg
    FB_IMG_1590922168583.jpeg
    16.6 KB · Views: 1
  • 20200530_145212.jpeg
    20200530_145212.jpeg
    71.7 KB · Views: 1
Uboreshaji wa demokrasia, Elimu na kuwaongezea wananchi kupata access za fedha, mawasiliano na kula bata.
Ningeondoa "Elimu" na kumpa "Miundombinu"- Barabara nyingi akiendeleza za Mkapa na kuongeza nyingine.

Lakini kama kawaida ya JF siku hizi, mada nyingi zinazoletwa hapa ni za kurashiarashia tu, wanaozileta hawaweki uzito unaostahiri kuziandaa vyema kabla ya kuziwasilisha.

Mwalimu Nyerere huwezi kumwandika kwa mstari mmoja huo kwa mambo mengi aliyofanya katika hali iliyokuwa ngumu sana.

Utamnyimaje "Elimu" na huku hata madaktari tu tulikuwa na wa kuhesabu kwenye mkono mmoja.

Ni mada mhimu sana hii, lakini kwa bahati mbaya, ndiyo hivyo tena..., tutarashia na kupita.

Kuhusu anayefuata, ngoja nisiondoke bila kuweka pendekezo hapo:
Ni, Elimu, Elimu, na elimu tena..., tumerudi nyuma mno katika eneo hili. Tulipashwa tuiwekee mkazo elimu yetu tokea tupate uhuru hadi sasa bila ya kupunguza mkazo huo.
"Kilimo" umemnyima Kikwete 'credits zake katika eneo hili _ Kilimo Kwanza ilianza kuonyesha matumaini, na ndiyo hiyo hiyo inayoendelea kutulisha na kujigamba kuwauzia wanaopenda kupigana vita.

"Viwanda" ni eneo la tatu linalotakiwa kuwekewa mkazo na yeyote atakayekuwa kwenye madaraka na kuendelea kuwa kipaumbele kwenda mbele.

Magufuli huwezi kumnyima credits zake kwa kupigania raslimali za nchi hii zinufaishe wananchi, pamoja na kwamba hili lilifanyika kwa kelele nyingi kama ilivyo kawaida yake ya kufanya mambo.
Katika eneo hili atagawana na Mwalimu Nyerere, yeye akichukua robo.
 
Back
Top Bottom