Je, Rais Magufuli atahudhuria kikao cha UN General Assembly cha mwaka huu?

Kwa maoni yangu,naunga mkono msimamo wa Rais Magufuli wa kukataa 'kupigia magoti' hao chui wenye ngozi ya kondoo.Namuunga mkono kwa kukataa kuwanyenyekea hao 'wajomba' wanafiki.Namuunga mkono kukataa kuwa 'mtumwa wa hiari' kwa mabeberu na taasisi zao kimumiani,hasa zile za Brettonwoods.Namuunga mkono kwa kukataa kujipendekeza kwa hao wakubwa wenye sura mbili;sura moja imejaa huruma 1% na sura nyingine imejaa wingu jeusi la uporaji kwa 99%.
Mabeberu hawawapendi Waafrika ila wanaipenda Afrika kwa wingi wa rasilimali.
 
Falasana wewe
 
Endelezeni ujeuri
 

Kwa uelewa wangu mdogo nadhani ukiondoa nchi zile kubwa wakuu wa nchi ndogo wanaopewa nafasi ni wale walioshika madaraka baada ya mkutano uliopita wa General Assembly. Rais wetu alitakiwa kuhutubia Baraza hilo mwaka 2016. Maadam hakufanya hivyo wakati ule wala mwaka uliofuata his chance is gone until may be after the 2020 elections.
 
Bila hizo safari leo hii tusingekuwa na uwezo wa kupata hata ARV
 
Mkuu, hata Nyerere alikuwa akienda hizi safari za UN, si mnasema Magufuri kama Nyerere, vipi tena basi kwenye nyanja hii muhimu ya Diplomasia mbona hafuati nyayo?
Nyerere aliandika "TUJISAHIHISHE"
JPM ana kazi saaana.
Hizi zingine VP mama Samia anatosha kabisa kuzihandle.
 
Mkuu Rogojin humu ndani kuna baadhi ya watu wanaandika kejeli kwa makusudi, wanajifanya wajinga lakini ni mbinu tu za kimajadiliano.

Tuna wasomi wangapi wenye kujua kingereza ambao waliishia kwenda Uingereza na kusaini mikataba kwa matakwa ya wazungu?.

Tuna makuwadi wangapi wa wazungu ambao wameiuza nchi yetu huko nyuma kwa kulipwa fedha mbuzi tu?.

Ujinga haushii kutolewa shuleni tu, mpaka humu jukwaani wapo wajinga wengi wenye kuhitaji darasa pana.
 
Mkuu, hata Nyerere alikuwa akienda hizi safari za UN, si mnasema Magufuri kama Nyerere, vipi tena basi kwenye nyanja hii muhimu ya Diplomasia mbona hafuati nyayo?
Huyu wa sasa azihitaji sana hizo safari za nje kama ambavyo mnajaribu kujenga hoja, huyu anayaishi maisha halisi ya kiuchumi. Kilichopo kinatumika kadri ya mahitaji yaliyopo.

Hao wazungu wanaipenda sana hiyo tabia, achana na haya majungu ya humu JF kwamba wazungu hawamkubali JPM. Wazungu ukiishi nao wanapenda kukuona ukiwa ni mtu mwenye kutumia kinachopatikana kiakili, hawapendi matanuzi ya kipuuzi.

Wazungu hawapendi na hawafurahishwi na tabia ya mtu kula bata wakati watoto wanapiga mihayo vijijini, media za kitanzania zinanunuliwa sana, matokeo yake malengo ya kishenzi ya wapigaji yanaonekana kama ndilo wazo la watawala.
 
Hoja ya kipuuzi. Mtu kula sana ni ulafi. Na ulafi ni muhimu kupingwa. Lakini huwezi kuacha kula kwa kisingizio kuwa umeambiwa usiwe mlafi. Utakuwa huna akili.
 
Usitoe hoja za kipuuzi.

UN kuna lugha zilizoidhinishwa kama lugha rasmi za Umoja huo. Kiswahili hakimo lakini sisi tuna official languages 2. Ya kwanza ni Kiingereza na ya pili ni Kiswahili. Hivyo inafahamika kuwa kwa vile English ni official language no. 1 kwetu, kwenye mawasiliano ya kimataifa tuna lugha yetu tayari ambayo ni English.

Warusi, Wajerumani, Wachina, Wafaransa, Wasenegali, n.k. wanatumia lugha za Kirusi, Kijerumani Kichina, Kifaransa, Kifaransa, n.k. kwa sababu ndiyo official languages zao katika mataifa yao, na hata UN wanazitumia lugha hizo.

Na hata ukifika kwenye mataifa niliyoyataja, utawekewa vitafsiria lugha toka kwenye lugha hizo kwenda kwenye lugha yako official ya Kiingereza.

Watanzania tuache ujinga. Kwetu lugha rasmi namba 1 ni English. Ndiyo maana hata sheria zetu zinatungwa kwa Kiingereza na kutafsiriwa kwa Kiswahili na siyo kinyume chake.

Lugha yetu ya kufundishia masomo ni English. Kiongozi kutojua official language ya Taifa lako, lazima itakuwa ni kioja kikubwa. Mawasiliano ni jambo muhimu sana.

Udhaifu wa Watanzania kutomudu official language yetu ni upungufu mkubwa. Tuichukue hii kama ni challenge inayohitaji kufanyiwa kazi kwa umakini. Na wala siyo English tu, Watanzania wengi, na hata viongozi hawawezi kuongea Kiingereza kizuri wala Kiswahili kizuri. Yaani hawamudu lugha yoyote. Tunatazama zaidi makosa katika kuongea Kiingereza lakini wengi hata Kiswahili hawakimudu.
 
Jiwe kweli jiwe maana likirushwa kwenye kundi la mbwa kelele zake ndo hizi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…