Je, Rais Magufuli atahudhuria kikao cha UN General Assembly cha mwaka huu?

Kwa maoni yangu,naunga mkono msimamo wa Rais Magufuli wa kukataa 'kupigia magoti' hao chui wenye ngozi ya kondoo.Namuunga mkono kwa kukataa kuwanyenyekea hao 'wajomba' wanafiki.Namuunga mkono kukataa kuwa 'mtumwa wa hiari' kwa mabeberu na taasisi zao kimumiani,hasa zile za Brettonwoods.Namuunga mkono kwa kukataa kujipendekeza kwa hao wakubwa wenye sura mbili;sura moja imejaa huruma 1% na sura nyingine imejaa wingu jeusi la uporaji kwa 99%.
Mabeberu hawawapendi Waafrika ila wanaipenda Afrika kwa wingi wa rasilimali.
 
Ndio kitu mnachokumbuka na kupigania kirudi tena. Zile safari za kila mwezi za Ulaya na Marekani. Kuhudhuria kuanzia mkutano wa kunguni, nzi, mbu na hata viroboto. Mnaweza kutuonyesha kitu gani kikubwa kilifanyika mpaka muanze kutuaminisha kwamba bila kwenda huko kwenye hiyo mikutano tunakosa kitu kikubwa?
Falasana wewe
 
Siamini kama UN General Assembly kama ni muarobaini wa mahitaji ama matatizo uliyoolozesha.
UN haina meno,wenye meno ni mataifa makubwa machache tajiri.nchi kama zetu bila juhudi binafsi hazitasonga mbele,ni kazi za wasaidizi wa rais kuyafanya hayo usemayo,wakiwemo mabalozi
Endelezeni ujeuri
 
Kikao cha UN General assembly kinafanyika tena mwezi wa tisa mwaka huu kama ilivyo ada

Ni mwaka wa nne huu wa utawala wa Rais Magufuli hajawahi kusafiri kutoka nje ya Afrika, tofauti na watangulizi wake, Mheshimiwa Magufuli hajahudhuria kikao hata kimoja cha UN General assembly.
Kikawaida vikao vya General assmebly ni vikao vyenye hadhi ya wakuu wa nchi ambapo mambo mengi huzungumzwa pale lakini ukiacha mbali na hapo huwa ni nafasi nzuri kwa mkuu wa nchi mmoja kupata nafasi ya kuongea na kukubaliana mambo mengi ya maendeleo na wakuu wenzie wa nchi mbalimbali.

Kwa sasa mathalani zao letu la korosho limeyumba, huu ulikuwa ni muda muafaka wa raisi Magufuli kuongea na wakuu wenzie wenye viwanda na masoko ya korosho kuona Tanzania inaweza kunufaika vipi na fursa zilizoko kwao.

Lakini pia nchi yetu inahitaji uwekezaji mbalimbali wa mitaji, hii ni nafasi ya kukutana na wafanyabiashara wakubwa ambao hufunga safari kipindi hiki ili waweze kukutana na viongozi wa nchi mbalimbali kuzungumza masuala ya uwekezaji.

Pia kwa kuwa nchi yetu ina utalii basi hiyo pia ni fursa nzuri ya kuongea na wadau wa utalii na kuona namna gani tunaweza kuleta watalii wengi zaidi.

Swali langu ni kwamba Miaka minne Mheshimiwa Raisi hajaenda kukutana na Kiongozi yeyote wa Taifa kubwa na wala hajahudhuria kikao chochote cha UN General assembly.

Je safari hii itaenda?

Kwa uelewa wangu mdogo nadhani ukiondoa nchi zile kubwa wakuu wa nchi ndogo wanaopewa nafasi ni wale walioshika madaraka baada ya mkutano uliopita wa General Assembly. Rais wetu alitakiwa kuhutubia Baraza hilo mwaka 2016. Maadam hakufanya hivyo wakati ule wala mwaka uliofuata his chance is gone until may be after the 2020 elections.
 
Ndio kitu mnachokumbuka na kupigania kirudi tena. Zile safari za kila mwezi za Ulaya na Marekani. Kuhudhuria kuanzia mkutano wa kunguni, nzi, mbu na hata viroboto. Mnaweza kutuonyesha kitu gani kikubwa kilifanyika mpaka muanze kutuaminisha kwamba bila kwenda huko kwenye hiyo mikutano tunakosa kitu kikubwa?
Bila hizo safari leo hii tusingekuwa na uwezo wa kupata hata ARV
 
Mkuu, hata Nyerere alikuwa akienda hizi safari za UN, si mnasema Magufuri kama Nyerere, vipi tena basi kwenye nyanja hii muhimu ya Diplomasia mbona hafuati nyayo?
Nyerere aliandika "TUJISAHIHISHE"
JPM ana kazi saaana.
Hizi zingine VP mama Samia anatosha kabisa kuzihandle.
 
Ndio usomi wetu ulipofika ukomo. Kuongea kiingereza, hata kama unachoongea ni shit tupu. Nchi yetu ni Zaidi ya mtu mmoja ambaye tunapenda kuona kama ndio sababu ya kila tatizo letu. Matatizo yetu hayapo mbali na sisi. yapo ndani ya kila mmoja wetu kwa nafasi yake. Unless tunayaanza hayo, kiingereza tutaongea lakini hakitupi status yoyote popote pale.
Hizi kelele ambazo ndani ni empty, hazimzuii tembo kunywa maji. Tuwe strategic
Mkuu Rogojin humu ndani kuna baadhi ya watu wanaandika kejeli kwa makusudi, wanajifanya wajinga lakini ni mbinu tu za kimajadiliano.

Tuna wasomi wangapi wenye kujua kingereza ambao waliishia kwenda Uingereza na kusaini mikataba kwa matakwa ya wazungu?.

Tuna makuwadi wangapi wa wazungu ambao wameiuza nchi yetu huko nyuma kwa kulipwa fedha mbuzi tu?.

Ujinga haushii kutolewa shuleni tu, mpaka humu jukwaani wapo wajinga wengi wenye kuhitaji darasa pana.
 
Mkuu, hata Nyerere alikuwa akienda hizi safari za UN, si mnasema Magufuri kama Nyerere, vipi tena basi kwenye nyanja hii muhimu ya Diplomasia mbona hafuati nyayo?
Huyu wa sasa azihitaji sana hizo safari za nje kama ambavyo mnajaribu kujenga hoja, huyu anayaishi maisha halisi ya kiuchumi. Kilichopo kinatumika kadri ya mahitaji yaliyopo.

Hao wazungu wanaipenda sana hiyo tabia, achana na haya majungu ya humu JF kwamba wazungu hawamkubali JPM. Wazungu ukiishi nao wanapenda kukuona ukiwa ni mtu mwenye kutumia kinachopatikana kiakili, hawapendi matanuzi ya kipuuzi.

Wazungu hawapendi na hawafurahishwi na tabia ya mtu kula bata wakati watoto wanapiga mihayo vijijini, media za kitanzania zinanunuliwa sana, matokeo yake malengo ya kishenzi ya wapigaji yanaonekana kama ndilo wazo la watawala.
 
Ndio kitu mnachokumbuka na kupigania kirudi tena. Zile safari za kila mwezi za Ulaya na Marekani. Kuhudhuria kuanzia mkutano wa kunguni, nzi, mbu na hata viroboto. Mnaweza kutuonyesha kitu gani kikubwa kilifanyika mpaka muanze kutuaminisha kwamba bila kwenda huko kwenye hiyo mikutano tunakosa kitu kikubwa?
Hoja ya kipuuzi. Mtu kula sana ni ulafi. Na ulafi ni muhimu kupingwa. Lakini huwezi kuacha kula kwa kisingizio kuwa umeambiwa usiwe mlafi. Utakuwa huna akili.
 
Nimuogope nani? Kuna lugha mtu akiongea unajua anasema kutokea nafasi gani. Uko shimoni. Hizi ni lugha za mkosaji. Toka lini kiingereza kimekuwa issue ya muhimu kwa political leaders?
Hata kama anajua kiingereza, akienda Russia na Ufaransa au China anafanyaje? Tunajua nguvi dola iliyonayo kwenye mambo ya diplomasia?
Usitoe hoja za kipuuzi.

UN kuna lugha zilizoidhinishwa kama lugha rasmi za Umoja huo. Kiswahili hakimo lakini sisi tuna official languages 2. Ya kwanza ni Kiingereza na ya pili ni Kiswahili. Hivyo inafahamika kuwa kwa vile English ni official language no. 1 kwetu, kwenye mawasiliano ya kimataifa tuna lugha yetu tayari ambayo ni English.

Warusi, Wajerumani, Wachina, Wafaransa, Wasenegali, n.k. wanatumia lugha za Kirusi, Kijerumani Kichina, Kifaransa, Kifaransa, n.k. kwa sababu ndiyo official languages zao katika mataifa yao, na hata UN wanazitumia lugha hizo.

Na hata ukifika kwenye mataifa niliyoyataja, utawekewa vitafsiria lugha toka kwenye lugha hizo kwenda kwenye lugha yako official ya Kiingereza.

Watanzania tuache ujinga. Kwetu lugha rasmi namba 1 ni English. Ndiyo maana hata sheria zetu zinatungwa kwa Kiingereza na kutafsiriwa kwa Kiswahili na siyo kinyume chake.

Lugha yetu ya kufundishia masomo ni English. Kiongozi kutojua official language ya Taifa lako, lazima itakuwa ni kioja kikubwa. Mawasiliano ni jambo muhimu sana.

Udhaifu wa Watanzania kutomudu official language yetu ni upungufu mkubwa. Tuichukue hii kama ni challenge inayohitaji kufanyiwa kazi kwa umakini. Na wala siyo English tu, Watanzania wengi, na hata viongozi hawawezi kuongea Kiingereza kizuri wala Kiswahili kizuri. Yaani hawamudu lugha yoyote. Tunatazama zaidi makosa katika kuongea Kiingereza lakini wengi hata Kiswahili hawakimudu.
 
Jiwe kweli jiwe maana likirushwa kwenye kundi la mbwa kelele zake ndo hizi.
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom