Je, Rais alikuwa sahihi kuwaomba msamaha wazee?

tzkwanza

JF-Expert Member
Dec 27, 2018
1,568
3,604
Jana kwenye mkutano kati ya Rais na wazee wa Dar es Salaam aliwaomba msamaha kwa kuwalazimisha wavae masks/barakoa.

Swali: Huo msamaha ni wa nini? Maana dunia inapitia janga la Corona hivyo kuwalinda na kujilinda ni jukumu la kila mtu sio suala la hiyari au kubembelezana.

Pia kama kamati ikimshauri mama Samia atoe chanjo kwa wazee ataweza kweli kuwaambia kama barakoa tu imebidi aombe msamaha?

Nchi ilichezewa na taarifa potofu kuhusu Corona zimejaa vichwani mwa watanzania.
 
Lugha za kiungwana tu mkuu. Za kubakia na mavi yao hazina nafasi katika awamu ya sita.

Serikali zinawajibu wa kuwajibika kwa wananchi. Si wananchi kuwajibika kwa serikali.

Utamaduni mpya huu wa awamu ya sita utawachanganya sana wasioupenda. Wapo tayari wana scavenge makopo majalalani.
 
Lugha za kiungwana tu mkuu. Za kubakia na mavi yao hazina nafasi katika awamu ya sita.

Serikali zinawajibu wa kuwajibika kwa wananchi. Si wananchi kuwajibika kwa serikali.

Utamaduni mpya huu wa awamu ya sita utawachanganya sana wasioupenda. Wapo tayari wana scavenge makopo majalalani.
Kweli kabisa. Je, wazee wataelewa?
 
SSH ni dhaifu, mbona kwenye mkutano wa CCM hakulazimisha masks ? Au kina Mwinyi na Mang’ula sio wazee wale? Auto pilot mode inaendelea, kituo ni 2025.
Kwani jana ndio leo? Kama taarifa za hali tofauti ya corona ilimfikia baada ya mkutano ule? Jamaa mbona umekuwa negative sana kwa Samia kwa kila alifanyalo shida nini hasa! Kubali matokeo Samia hakujichagua wala kujiteua wala kupindua. Ni mpendwa wako ndiye aliyemuona anafaa kuwa Naibu Rais huku katiba yako ndiyo imeamua hivyo punguza, chuki zisizo na mantiki.
 
Ni lugha za kiungwana, na haimaanishi kwamba anawaogopa, Samia ameonesha ana IQ kubwa sana ukilinganisha na JPM, amekuwa mara nyingi akitanguliza busara mbele kuliko ubabe wa kishamba aliokuwa nao yule alimtangulia, na amekuwa akisema mara kwa mara kwamba tulikuwa tunaelekea kubaya.

Lema na Msigwa waliwahi kuyasema haya ambayo amekuja kuyarudia na kuyatolea amri, kuwaomba mshamaha hakukosea, ni dalili ya Heshima kwa watu wengine bila kujali cheo chako
 
Mkuu kwa hadhi ya jukwaa kama hili leta mada ambazo ni strategic tofautisha nada za whatsapp group.
 
Back
Top Bottom