Maoni ya mdau juu ya hotuba ya Rais. Tumewadharau wataalamu wa Afya, Rais anatoa ushauri wa kisiasa

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,867
MAONI YANGU KUHUSU HOTUBA YA RAIS JPM.

#Kuhusu_Lockdown. Rais amesema uchumi wa nchi kwa kiasi kikubwa unategemea jiji la Dar. Japo ni kweli lakini apime kati ya uchumi na maisha ya wananchi wake kipi kina uzito zaidi. Let him choose the lesser evil. Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo aliwahi kusema “tutizame zaidi maisha ya watu kuliko uchumi, kwa sababu uchumi ukifa kuna njia nyingi za kuufufua, lakini watu wakifa hakuna namna ya kuwafufua”

#Kuhusu_Fumigation. Rais kasema ni jambo la kipuuzi kwa sababu hakuna fumigation inayoua virusi labda mende. Lakini je mbona mataifa makubwa yamefanya? Uchina, Uingereza, Marekani, Canada wote wanafanya fumigation. Je nao wanafanya upuuzi? Anyway tukubaliane na "mkuu" kwamba nao ni wapuuzi tu kama wapuuzi wengine. Lakini je nani ameleta upuuzi huo hapa nchini? JPM hamjui mkuu wa mkoa aliyezibatiza mashine za fumigation kuwa ni mashine zake? Sasa kwanini asimchukulie hatua?

#Kuhusu_Barakoa. Rais kasema wanaoweza kujishonea barakoa zao wajitengenezee wavae. Sidhani kama hii ni kauli sahihi kwa sababu barakoa si kitambaa tu cha kufunuika kinywa. Ni zaidi ya hapo. Wataalamu wanasema si kila barakoa inaweza kuzuia virusi vya Covid19. Ni zile zilizotengenezwa kitaalamu tu ambazo ni "Surgical mask" au N95. Sasa hii ya kuwaambia wananchi wajitengenezee za kwao, wengi watavaa matambara wakiamini wapo salama kumbe si kweli.

Pia Rais kasema kuna uwezekano tukaletewa barako za msaada kutoka nje zenye virusi vya Corona sidhani kama ni sahihi. Hizi ni story tulizozoea kuzisikia vijiweni ambazo mara nyingi hazina uthibitisho. Nijuavyyo mimi “mabepari” wangetaka kutuangamiza wasingesubiri hadi corona ije. Hebu fikiria tumetumia chanjo ngapi utotoni. Kuna vifaa tiba vingapi vimejaa mahospitalini mwetu vimetoka nje? Hata mabohari ya MSD yamejaza madawa kutoka nje. Wangetaka kutumaliza ingekuwa zamani sana.

#Kuhusu_Karantini. Rais ameshauri watu wasikae karantini siku 14 kama wanaonekana ni wazima. Nadhani hapa Rais hakushauriwa vizuri. Suala la siku 14 za karantini ni ushauri wa kitaalamu uliotolewa na shirika la afya duniani (WHO). Wataalamu wanaamini siku 14 zinatosha kumtizama mtu na kujua kama ana maambukizi ama lah. Otherwise tutawatoa watu karantini na kuwaruhusu kwenda uraiani lakini tujiandae kwa maafa makubwa. Mheshimiwa Rais akae na wataalamu wa afya wamweleweshe kwanini WHO inasisitiza siku 14 za karantini na si chini ya hapo.

#KuhusuUsahihiWaTakwimu. Rais amesema yeye anazo taarifa za waliopona wanakaribia 100 lakini Waziri Ummy anasema waliopona ni 11 tu. Hapa ni wazi kuna mkanganyiko wa taarifa. Kuna kundi moja linapotosha kwa makusudi. Either linalompa taarifa Rais JPM au linalompa taarifa Waziri Ummy. HAIWEZEKANI Rais na Waziri wake wakawa na takwimu zinazopingana kwenye suala nyeti nkama hili. Na kama kweli takwimu za Ummy zina kasoro, basi kasoro hiyo haiwezi kuwa kwa waliopona tu. Itahusu pia wagonjwa na waliokufa. Hii ina maanisha yale madai kwamba wagonjwa na waliokufa ni wengi kuliko takwimu zinazotolewa na Wizara ya afya huenda yakawa na ukweli.

#Kuhusu_Kujifukiza. Rais amesema watu waendelee kutumia njia za asili za kujilinda ikiwemo kujifukiza na kwamba virusi "vitapasukapasuka" kama nyuzi joto zikizidi 100. Lakini Naibu Waziri wa Afya Faustine Ndugulie alisema kuwa kujifukiza sio njia sahihi ya kupambana na virusi vya Corona. Akasema wanaojifukiza wana hatari ya kuunguza na kuharibu njia ya hewa.

Ndugulile ni daktari kitaaluma, na alizungumza kitaalamu. Hii ina maanisha kuwa Rais JPM hajashauriwa vizuri kuhusu hili suala la kujifukiza. Alipaswa "kuwaconsult" kwanza wataalamu kabla ya kuongea hadharani. Kupingana na Waziri wake hadharani ni kuleta mkanganyiko usiokuwa na lazima.

Malisa GJ
 
1587615533365.jpeg
 
Lengo la Rais lilikuwa Jema, alikuwa ana taka kupunguza hofu kwa Umma. Ila njia na maneno aliyo yatumia imefanya watu wapuuzie.
 
Ni kweli hofu imezidi lakini ninachokiona ni hofu ya kumuogopa Rais na kuogopa kuhitilafiana naye.Hofu hii itatuumiza zaidi.
Wanasayansi jitokezeni muendeshe vita hii.Waziri Ummy,Kamati ya kitaifa ya Corona,jifungieni na tokeni na maelekezo ya kitaalamu.
 
Wataalamu wa afya hawa si ndo hata hawajulikani kama wapo kipindi hiki?..wao wanajua kuandika dawa tu..
 
Doctor kasema, mnabisha nini? Tulichagua Doctor, Mwalimu, Hakimu, Mwanasheria, injinia, Mfugaji, Mkulima, Mvuvi , Mchungaji, Shehe, Rubani huyu mheshimiwa kila kitu anajua, Jopo la Madactari wa WHO alitumia vipimo sahihi kabisa kujua siku 14 ndio siku sahihi za kujua kuna maambukizi? Au hakuna, Doctor wetu kaita ni upuuzi,

Tuombe Mungu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo kwenye kujifukiza nimesoma mahala eti watu wajifukize mvuke wenye nyuzi joto 100 nikasema hiiiiiii.

Sent using Jamii Forums mobile app
atakuwa labda anamaanisha nyungu yaani chungu chenye mchanganyiko wa mimea yenye dawa kinachemshwa na baadaye mtu hujifunika shuka hufuniliwa na ule mvuke ndio unasambaa akiwa ndani ya hiyo shuka ni kama sauna ila nadhani joto lake huwa kali zaidi ila pengine kiangazi ugonjwa huu unaweza pungua kama wataalam hawa wanaovyosema ni hakika
Screen Shot 2020-04-18 at 10.45.31.png
 
Hostel za Magufuli zifungwe watu warejee majumban

Pia tujiandae kusikia Umati wa watu waliopona kuanzia leo kutekeleza maelekezo ya Amiri Jeshi kwa katibu Mkuu mpya, huenda Dr Zainab Chaula alipuuza Maelekezo ya Mwana Sayansi Maarufu Nchini Dr, Amiri jeshi n.k

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna maneno ukiwa Kama mimi unaweza ukayaongea mtaani au vijiweni na maisha yakaenda. Ila unapokuwa umekalia kiti kama kile, kila unalolisema lazima liwe limetafakariwa baada ya kupata maoni kutoka kwa wataalamu. Maana sauti ya kile kiti ni sauti ya taifa.
 
MAONI YANGU KUHUSU HOTUBA YA RAIS JPM.

#Kuhusu_Lockdown. Rais amesema uchumi wa nchi kwa kiasi kikubwa unategemea jiji la Dar. Japo ni kweli lakini apime kati ya uchumi na maisha ya wananchi wake kipi kina uzito zaidi. Let him choose the lesser evil. Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo aliwahi kusema “tutizame zaidi maisha ya watu kuliko uchumi, kwa sababu uchumi ukifa kuna njia nyingi za kuufufua, lakini watu wakifa hakuna namna ya kuwafufua”

#Kuhusu_Fumigation. Rais kasema ni jambo la kipuuzi kwa sababu hakuna fumigation inayoua virusi labda mende. Lakini je mbona mataifa makubwa yamefanya? Uchina, Uingereza, Marekani, Canada wote wanafanya fumigation. Je nao wanafanya upuuzi? Anyway tukubaliane na "mkuu" kwamba nao ni wapuuzi tu kama wapuuzi wengine. Lakini je nani ameleta upuuzi huo hapa nchini? JPM hamjui mkuu wa mkoa aliyezibatiza mashine za fumigation kuwa ni mashine zake? Sasa kwanini asimchukulie hatua?

#Kuhusu_Barakoa. Rais kasema wanaoweza kujishonea barakoa zao wajitengenezee wavae. Sidhani kama hii ni kauli sahihi kwa sababu barakoa si kitambaa tu cha kufunuika kinywa. Ni zaidi ya hapo. Wataalamu wanasema si kila barakoa inaweza kuzuia virusi vya Covid19. Ni zile zilizotengenezwa kitaalamu tu ambazo ni "Surgical mask" au N95. Sasa hii ya kuwaambia wananchi wajitengenezee za kwao, wengi watavaa matambara wakiamini wapo salama kumbe si kweli.

Pia Rais kasema kuna uwezekano tukaletewa barako za msaada kutoka nje zenye virusi vya Corona sidhani kama ni sahihi. Hizi ni story tulizozoea kuzisikia vijiweni ambazo mara nyingi hazina uthibitisho. Nijuavyyo mimi “mabepari” wangetaka kutuangamiza wasingesubiri hadi corona ije. Hebu fikiria tumetumia chanjo ngapi utotoni. Kuna vifaa tiba vingapi vimejaa mahospitalini mwetu vimetoka nje? Hata mabohari ya MSD yamejaza madawa kutoka nje. Wangetaka kutumaliza ingekuwa zamani sana.

#Kuhusu_Karantini. Rais ameshauri watu wasikae karantini siku 14 kama wanaonekana ni wazima. Nadhani hapa Rais hakushauriwa vizuri. Suala la siku 14 za karantini ni ushauri wa kitaalamu uliotolewa na shirika la afya duniani (WHO). Wataalamu wanaamini siku 14 zinatosha kumtizama mtu na kujua kama ana maambukizi ama lah. Otherwise tutawatoa watu karantini na kuwaruhusu kwenda uraiani lakini tujiandae kwa maafa makubwa. Mheshimiwa Rais akae na wataalamu wa afya wamweleweshe kwanini WHO inasisitiza siku 14 za karantini na si chini ya hapo.

#KuhusuUsahihiWaTakwimu. Rais amesema yeye anazo taarifa za waliopona wanakaribia 100 lakini Waziri Ummy anasema waliopona ni 11 tu. Hapa ni wazi kuna mkanganyiko wa taarifa. Kuna kundi moja linapotosha kwa makusudi. Either linalompa taarifa Rais JPM au linalompa taarifa Waziri Ummy. HAIWEZEKANI Rais na Waziri wake wakawa na takwimu zinazopingana kwenye suala nyeti nkama hili. Na kama kweli takwimu za Ummy zina kasoro, basi kasoro hiyo haiwezi kuwa kwa waliopona tu. Itahusu pia wagonjwa na waliokufa. Hii ina maanisha yale madai kwamba wagonjwa na waliokufa ni wengi kuliko takwimu zinazotolewa na Wizara ya afya huenda yakawa na ukweli.

#Kuhusu_Kujifukiza. Rais amesema watu waendelee kutumia njia za asili za kujilinda ikiwemo kujifukiza na kwamba virusi "vitapasukapasuka" kama nyuzi joto zikizidi 100. Lakini Naibu Waziri wa Afya Faustine Ndugulie alisema kuwa kujifukiza sio njia sahihi ya kupambana na virusi vya Corona. Akasema wanaojifukiza wana hatari ya kuunguza na kuharibu njia ya hewa.

Ndugulile ni daktari kitaaluma, na alizungumza kitaalamu. Hii ina maanisha kuwa Rais JPM hajashauriwa vizuri kuhusu hili suala la kujifukiza. Alipaswa "kuwaconsult" kwanza wataalamu kabla ya kuongea hadharani. Kupingana na Waziri wake hadharani ni kuleta mkanganyiko usiokuwa na lazima.

Malisa GJ
Mkuu hakuna "beberu" atakayekujali, hasa wakati huu wa Corona.
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom