Je, Prof. Assad alijifanya mhimili?

mafutamingi

JF-Expert Member
Feb 14, 2011
2,770
2,171
Jana wakati Rais Magufuli alipokuwa anamuapisha CAG mpya Ndg Charles Kichere, alisema kuwa Prof. Assad alijigeuza kuwa mhimili.

Nimejaribu kutafakari na kuibua kumbukumbu yangu kuhusu jambo lolote alilolifanya Prof. Assad ambalo lingebeba taswira ya kwamba anajigeuza mhimili lakini sijapata jibu.

Je, kuna yeyote mwenye jibu?
 
Ndio akaoneshwa mlango wa kutokea State agent



FB_IMG_1572959030873.jpeg
 
Achana na mawazo muflisi..Ibrahim Juma ni muislam, nani amemkomoa kwa sababu ya dini yake?.

Nahisi utakua haujamuelewa vzr huyo aliesema kua tatizo ni uislamu wake.

Ulipaswa kumuuliza huo uislamu wake kwa nini uwe ni tatizo?

Mimi nitakujibu kua uislamu wake unamtaka awe mkweli na muadilifu.

Umeelewa au bado unahitaji maelezo ya ziada?
 
Sio kweli tatizo ni kufanya kazi kwa weredi na uadilifu pia kukataa kutumika. Angekuwa mtu ambaye hana misimamo kama Lipumba amini angeongezewa muda mwingine
Uislamu wake unamtaka awe mkweli na afanye kazi kwa uweredi na uadilifu, hilo ndio tatizo ambalo jamaa amelihusisha na dini yake.
Una swali jingine?
 
Nahisi utakua haujamuelewa vzr huyo aliesema kua tatizo ni uislamu wake.
Ulipaswa kumuuliza huo uislamu wake kwa nini uwe ni tatizo?
Mimi nitakujibu kua uislamu wake unamtaka awe mkweli na muadilifu.
Umeelewa au bado unahitaji maelezo ya ziada?
Kwa hiyo wakristo sio wakweli na waadilifu?.

Kwa taarifa yako mmoja wa washauri wa karibu wa JPM ni muislam ni mtu mwenye umuhimu sana katika masuala ya hizi ndege zinazokuja na rada.

Mbarawa ni muislam na wapo wengine ambao ni muhimu sana awamu hii.

Kukimbilia uislam ni kuishiwa hoja.
 
Jana wakati Rais Magufuli alipokuwa anamuapisha CAG mpya Ndg Charles Kichere, alisema kuwa Prof Assad alijigeuza kuwa mhimili. Nimejaribu kutafakari na kuibua kumbukumbu yangu kuhusu jambo lolote alilolifanya Prof Assad ambalo lingebeba taswira ya kwamba anajigeuza mhimili lakini sijapata jibu. Je kuna yeyote mwenye jibu?
Tatizo Magufuri anajiamulia mambo bila kusoma Katiba, na bahati mbaya Mwanasheria Mkuu wake naye ni kilaza. Hakuna siku CAG amewahi kuwa mhimili, bali sheria inampa hadhi ya kuwa 'Independent'.

Ukishatoa hadhi ya Independence kwa CAG, hapo hapo anaacha kuwa CAG anakuwa examiner!!
Magufuri aheshimu fani za wengine, yeye kasoma chemistry tu. Anaharibu nchi vibaya sana.
 
Back
Top Bottom