Je, petrol imeadimika soko la dunia?

Je, petrol imeadimika soko la dunia?

Umkonto

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2018
Posts
3,115
Reaction score
5,367
Naona uzi wa jamaa umefutwa unaohusu baadi ya maeneo nchini vituo vya mafuta kukosa mafuta hasa petrol.

Sasa nakazia, na huu uzi mods waufute tu kwa sababu hali halisi ndivyo ilivyo.

Baadhi ya maeneo nchini hasa wilayani huku mafuta hayapatikani hasa petrol.

Je, tatizo ni nini?

Mbona serikali haitolei ufafanuzi juu ya hili wakati wawakilishi wa serikali kila wilaya wapo ( Wakuu wa Wilaya)?

Kwani huko Dar petrol ipo?

Huku mikoani hasa wilayani hakuna petrol, na kama ipo inauzwa kwa maringo katika vituo vya mafuta. Ukweli ndio huo!
 
Njombe ola ni sheli za oryx tu ndo yalikuepo. nauli zinapanda holela distance ya jero utalipa alf 3
nimetembea gari imekata wese mpaka sasa iko pembeni ya road kwenda sheli lita moja 5k
 
Tangu mume wa sabufa ateuliwe ndio uhaba wa mafuta unprecedented umeanza kujitokeza.
Lazima Kuna uhusiano wa moja kwa moja Kati ya uongozi wa huyu mtu na huu upungufu.
Sijajua Kama anajua Kama Tabora mjini hakuna mafuta.
 
Duuh hii mbona kali sasa?
Bado ina nafuu. Sitii neno zaidi. Na hiyo shukuru hisani ya vijana wenye uthubutu kukimbia kusaka yanakopatikana kwa hatari ya kubeba madumu hadi 12 (lita 240) kwa pikipiki. Wanakimbia kilimita zaidi ya 300. Imewapa nafasi ya kuigeuza changamoto kuwa fursa kwa angalau muda kidogo. Sema tu, endesha ya bodaboda na hatari ya hicho kimiminika na mpangilio wa bodi ya pikipiki!!!
 
Naona uzi wa jamaa umefutwa unaohusu baadi ya maeneo nchini vituo vya mafuta kukosa mafuta hasa petrol.

Sasa nakazia, na huu uzi mods waufute tu kwa sababu hali halisi ndivyo ilivyo.

Baadhi ya maeneo nchini hasa wilayani huku mafuta hayapatikani hasa petrol.

Je, tatizo ni nini?

Mbona serikali haitolei ufafanuzi juu ya hili wakati wawakilishi wa serikali kila wilaya wapo ( Wakuu wa Wilaya)?

Kwani huko Dar petrol ipo?

Huku mikoani hasa wilayani hakuna petrol, na kama ipo inauzwa kwa maringo katika vituo vya mafuta. Ukweli ndio huo!
Jamii forums sijui wameanza kula rushwa nilipost kuhusu kuvuja kwa mitihani ya UTABIBU lakini wakafuta
IMG_20230904_054452.jpg
 
Tangu mume wa sabufa ateuliwe ndio uhaba wa mafuta unprecedented umeanza kujitokeza.
Lazima Kuna uhusiano wa moja kwa moja Kati ya uongozi wa huyu mtu na huu upungufu.
Sijajua Kama anajua Kama Tabora mjini hakuna mafuta.
Dollar zimeadimika duniani kwa sababu The Fed wamepandisha interest rate. Nadhani unajua madhara ya kupanda kwa interest rate ya dollar.

Pili, bidhaa kubwa itakayoathiriwa ni mafuta kwa sababu ndiyo yanayo kula dollars nyingi hasa kwa nchi kama Tanzania.

Tatu, ambalo ni la muhimu ili uondoe fikra ulizo nazo, Tanzanian Shilling kwa kipindi cha mwaka uliopita ndiyo iliyoonyesha more stability kuliko currency yeyote kwa nchi za Africka mashariki na kati.

Ikionyesha kuwa central bank ya Tanzania ndiyo angalau imechukua hatua bora zaidi, zenye matokeo chanya zaidi.

Shilingi ya Kenya sasa ni sawa na shilingi 17 za tanzania badala ya shilingi 21 za kitanzania., karibu ongezeko la thamani kwa 20%.
 
Back
Top Bottom