Je Papa anakufuru?

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Jul 24, 2014
24,504
28,691
Kukufuru ni kujiweka ktk nafasi ya Mungu ingawa wewe ni mwanadamu Yohana 10:33 Wayahudi wakamjibu, kwa ajiri ya kazi njema hatukupigi kwa mawe; bali kwa kukufuru, na kwa sababu wewe ulie mwanadamu wajifanya mwenyewe u Mungu. ---->hiyo ndo maana ya kukufuru. Kudai kuwa sawa na Mungu.
==>Isaya 14:13,14 Shetani alitamani kupaa juu kupita nyota za mbinguni ili afanane na Mungu, yaani akakae ktk nafasi ya Mungu.
==>Mwanzo Mwanzo 3:5 Shetani aliuingiza ulimwengu dhambini kwa kosa la kufuru yaani alimshawishi Eva akaidi agizo la Mungu amwahidi kuwa "atakuwa kama Mungu"-->hii ni kufuru!
WAKATOLIKI wana mwanadamu waliempa jina lenye wadhifa na wasifu wa Mungu peke yake, yaani " Baba Mtakatifu" Soma: Yohana 17:11Wala mimi simo tena ulimwenguni, lakini hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba Mtakatifu, kwa jina lako ulilonipa uwalinde hawa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo.
Umeona hiyo aya inavobainisha kuwa "Baba Mtakatifu" ni jina la Mungu? Lakini Wakatoliki wana babao mtakatifu mwingine!!!!!? KUFURU!.


Mathayo 23:9 Wala msimwite mtu baba duniani; maana Baba yenu ni mmoja, aliye wa mbinguni. 10. Wala msiitwe viongozi; maana kiongozi wenu ni mmoja, naye ndiye Kristo.
a1c24a7039696fc400f2495b14f81a4b.jpg

Ndugu zangu aya hii ya 9, Mungu kakataa kuwa na ubia ktk jina lake la mamlaka linalobeba wadhifa wake. Kumwita mtu baba Mtakatifu na kiongozi mkuu wa dini ni KUFURU.
Mwenye masikio na asikie ambayo roho awaambia Wakatoliki. Mimi ni mjumbe tu kuwakumbusha yaliyokwisha bainishwa
6c9ad4bf3f1a83fb90dfe2d0b6c7f9d9.jpg
 
mkuu naona ule uzi umekutia mzuka ukaanzisha mwingine wa kufanana na ule ili mzuka wako upande zaidi.
Nakushauri tu unapoandika uzi wowote tulia andika vizuri utaeleweka!
Km utaamua kusoma biblia kwa matakwa yako hakika umepotea.

Rudia vzuri nukuu yako hapo juu hyo ya Mathayo 23:9,
hapa duniani baba aliyekuzaa /kiongoz wako wa dini mfano mchungaji unamuitaje?.Ukisoma mstari mmoja bila kuomba kibali cha roho mtakatifu uweze japo kuelewa aya moja tu katika biblia nzima hakika utakuwa unafanya KUFURU.

Na nimuhimu kwako ukatambua pia kila dhehebu,dini zinataratibu zake ili kuendelea kuleta amani na upendo katika jamii.
Mfano,Wakatoliki wana taratibu zao za kuabudu,za kulinda jamii inayowazunguka,za kusali!
Swala la kumuita kiongozi wao wa dhehebu Baba mtakatifu ni utaratibu wao hauna budi kuheshimu taratibu za wenzio ili kupata jamii inayoheshimiana.

Je unafahamu utaratibu wanaotumia kumtafuta baba mtakatifu?

Je unafahamu pia kwa kupitia utaratibu huo huo ndiyo kati ya dhehebu linaongoza katika kutoa huduma mbali mbali za kijamii kama elimu,afya,maji na chakula?

Mkuu ni bora ukatulia,ukaja na mada iliyoshiba na ushawishi wakutosha na siyo kunukuu mistari 2 ama 4 katika Biblia Takatifu ukaweka hapa kwa tafsiri ya matakwa yako!

Huyo roho anaesema na wakatoliki tu ni wawapi na ni roho gani huyo? mbona hujaweka mstari ktk Biblia kuonesha hilo?
 
Quran ni kitabu cha shetan alichompa jamaa mmoja anaitwa muddy miaka ya 600s
Majibu yako si yahekima hata kidogo! Inaonesha huwez kuishi na watu tofauti na dhehebu/dini yako.
Heshimu imani za wenzio.

Katika Biblia unayosoma ni wapi wameandika kuwa unaruhusiwa kukashifu ama kujibu kwa jeuri kuhusu imani ya jirani yako?

Rejea amri za Mungu zishike vyema na kuzielewa hakika utabarikiwa na Mungu aliyehai,Mungu asiyebagua dini,rangi wala kabila.
 
Here we go again. Seventh Adventists (Wasabato) at work. Yaani bila Papa na ukatoliki hamna dini. Hata hiyo misingi ya dini yenu huwa mnaihubiri saa ngapi kama kazi yenu kuu ni kupambana na Papa na ukatoliki 24/7? Nyinyi mnaamini nini? Wokovu unapatikanaje? Kwa kusoma na kufuata mafundisho ya Bibi Ellen G. White? Kwa kutokula samaki wenye magamba, wanyama wasio na kwato zilizogawanyika na wale wasiocheua? Ni kwa kuabudu Jumamosi? Ni kwa kutokunywa chai, kahawa na soft drinks? Ni kwa kukurupuka na kuwa na kiherehere cha kuhusisha kila tukio na unabii wa vitabu vya Daniel na Ufunuo? Usabato ni nini? Mtu atakwenda mbinguni kwa sababu ni Msabato?

Inawezekana kweli Papa ni ajenti wa shetani lakini je, hili linawasaidiaje nyinyi kama Wasabato? Mbona mko so obsessed na Papa na Wakatoliki? Dini na madhehebu mengine yote yako sawa isipokuwa Wakatoliki? Au mna bifu la kihistoria na Papa na ukatoliki?

Samahani kwa maswali mengi na natumaini kwamba hutatoa povu na badala yake utajaribu kutuelimisha kuhusu kikundi hiki cha kifarisayo (washika sheria za Musa) kiitwacho Seventh Adventists. Ajabu ni kwamba kikundi hiki kina mauzauza mengi yasiyofungamana na mafundisho ya Biblia na badala ya kukazania kuondoa kwanza mabolti katika macho ya wafuasi wake kimekazania mabolti ya Wakatoliki.

Anyway, Happy New Year mkuu (kama mnaamini/mnasherehekea mwaka mpya)!
 
Yani humu jf nimeshakutana na uzi kama tano hivi zote ni kuhusu papa na ukatoliki. Mpaka napata kinyaa juu ya hii kampeni yao. Nadhani wanavyoona krismasi ikipata waumini washerehekeaji wengi wamepagawa. Watakua wameambiwa waanze kusambaza upuuzi wao kwenye mitandao ya kijamii!
 
Yani humu jf nimeshakutana na uzi kama tano hivi zote ni kuhusu papa na ukatoliki. Mpaka napata kinyaa juu ya hii kampeni yao. Nadhani wanavyoona krismasi ikipata waumini washerehekeaji wengi wamepagawa. Watakua wameambiwa waanze kusambaza upuuzi wao kwenye mitandao ya kijamii!
Tatizo unataka usionywe kuhusu huu upagani

7ea70d08a3aa6a6ffd2bdf1884998df4.jpg
 
Kwa taarifa yako, kanisa la kweli ni moja tu lenye alama/nguzo kuu nne...!!
 
ha ha! bado mnanifanya nijichekee!
mwenye siraha ndio hudhuru why hadhuru adui mwenye hatari..?
 
Back
Top Bottom