Je nirudi kuwa single.

Je nirudi kuwa single.

MAULA

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
1,056
Reaction score
170
Kumekua na tofauti kubwa nilivyo kuwa single na nlivyo sasa na mwanamke.
Na tifauti kubwa nimekua mtumiaji hela vibaya kiasi ambacho nashindwa kuzitunza kama ilivyokuwa hapo awali kiasi hata nguo mpya sijanunua kwa mda mrefu.
Najiuliza:nirudi kuwa Alon but Happy ingawaje tabia za mwanamke wangu ni nzur hana tatizo?
Tukiachana na mabadiliko mengine meng madogo madogo
Nisaidiwe ushauri hapa wadau
 
Sasa mkuu hata ukirudi kuwa alone, si ipo siku huko mbeleni utahitaji kuwa na mwanamke tena!

Jambo la muhimu kwa sasa ni kupaswa kutambua kuwa mpo wawili na kuna baadhi ya mahitaji yameongezeka.

Sasa kutokana na hilo yakupasa uwe mtu wa bajeti na hii itakujenga kuja kuwa mume mzuri huko mbele.

Hata sisi kaka zako tulipitia hiyo life lakini hatukukimbia bali tulipambana na hali kama hiyo kwa kuhakikisha tunafanya mambo ya ziada kuongeza ngawira.

NB:
Kanuni ndogo tu ya kimahesabu ya fedha, huwa wanasema matumizi mara zote hayapaswi kuzidi mapato...ukizingatia hili haijalishi we ni single, in relationship au married...financial status haitakusumbua.
Jikune hadi pale unapoweza...
 
Tatizo ni kutumia hela sana jirekebishe
halafu endelea kuishi na mkeo
 
Ndio ukubwa huo, majukumu lazima yaongozeke na akili ichemke zaidi. Hasa kama mpenzi wako hana kipato cha kutosha, inabidi tu uingie mfukoni. Wewe unataka awe anapendeza tu, hivo vipodozi kununua inakuwa tabu. Ila usiingie kwenye madeni kwa sababu yake, make sure you find the right balance kaka.
 
Hapana tafuta hela nyingi zaidi na hakikisha unapata hela nyingi kuliko anavyoweza kutumia mkeo.
 
Pole sana!
Ila kama mkeo hana tatizo kurudi kuwa single ni sawa nakutaka urudi tumboni kwa mama yako ili iwe mimba! nacho maanisha labda ukafanyiwe operation ya kutofeel kufanya tendo la 6x6 kama hutaki kutoa matumizi!
Hapa Duniani ukisha zaliwa mwanaume utakula kwa jasho lako na familia mtu wa kwanza kum-exploit ni wewe!
ushauri wangu kwako:
1. Kuwa na nidhamu ya Fedha = sio kila kitu unacho kipenda lazima ukinunue ili mradi fedha iko mfukoni la hasha unapaswa kupangilia vitu vya kununua ukiwa nyumbani chochote utakacho kikuta njiani kama hakiko kwenye orodha yako hata kama unakipenda achana nacho.
2.Badilika = unapooa hupaswi kuishi maisha ya usingle at the same time ya ndoa, unapaswa kuhama hiyo stage ya usingle mfano Chakula ni lazima kula nyumbani labda kama inapotokea kuna ulazima wa kula nje na nyumbani mfano mchana uwapo kazini, sio uko mtaani tu unanunua chakula,unanunua vinywaji ovyo, ukiona kitumbua huyo, ukiona mwanamke huyo! kila kitu ikiwemo papuch jijengee utaratibu wa kula home hata ukinunua mtaani basi kilike home!
3. Kuwa Transparent kwa mkeo hasa swala la kipato ikiwezekana mshahara ukitoka mkabidhi yeye alafu pangeni matumizi kwa pamoja yeye awe mhasibu wa nyumbani alafu wewe ni m/kiti wa nyumbani. Hivyo nyote wawili mtaishi mkiwa mnajua uhalisia wa mfuko na hautapata shida lakini kama matumizi unakabwa shati ahsubuhi mzee unahesabia mfukoni lazima maisha yawe magumu.
4.Kama ulioa mke wa level ya juu ya maisha zaidi yako mdrag down to your level alafu use your exprience in your level ili aweze kuishi kama wewe ulivyokuwa unaishi!

Be smart kijana! mimi sijaoa lakini nilikuwa naona matumizi yote tunatoa kwa mama na hakuwa na kazi, ukimuomba baba hela anasema muone mama yako kiasi anacho kupa shangaa ukimuomba tena baba next time utasikia situlikupa kiasi kadhaa siku fulani anamwambia mama usimpe kweli mama hatoi kama shida ni mhimu mama anamshawishi baba unasikia haya mpe! maana yangu hapa nikuwa umechukua majukumu yote kuanzia kufikiri,kuhifadhi fedha,kutafuta,kutumia hata kujishauri unapaswa kugawana na mkeo majukumu.
Nikioa ntaishi kwa gharama nafuu sana kuliko nilivyo single naamini hivyo na itakuwa hivyo!!!!!!!!!!!
 
Kumekua na tofauti kubwa nilivyo kuwa single na nlivyo sasa na mwanamke.
Na tifauti kubwa nimekua mtumiaji hela vibaya kiasi ambacho nashindwa kuzitunza kama ilivyokuwa hapo awali kiasi hata nguo mpya sijanunua kwa mda mrefu.
Najiuliza:nirudi kuwa Alon but Happy ingawaje tabia za mwanamke wangu ni nzur hana tatizo?
Tukiachana na mabadiliko mengine meng madogo madogo
Nisaidiwe ushauri hapa wadau

Moja:Umesema kuwa mkeo "hana tatizo",wewe unadhani ni kipi ni tatizo na kipi sio tatizo?
Kama mkeo "hana tatizo" kwanini unafikiria kumuacha?

Pili:Kwa mujibu wa maelezo yako inaonekana unakubali kuwa mkeo sio chanzo cha wewe kutumia hela,ila unadhani ndoa ndio chanzo ndio maana unafikiria kurudi kuwa single,inamaana hujaona upofu ulioko kwenye namna yako ya kulitazama tatizo?
Nimesoma kidogo tu maelezo yako nikaona kuwa mwenye matatizo ni wewe
Hebu jikague kuhusiana na matumizi uliyoyaongeza baada ya kuoa ili ujiangalie upya kama unaweza kuyaondoa

Acha kuoilaumu ndoa yako!
 
Namuunga mkono shemeji watu8...:amen:
 
Last edited by a moderator:
Nafurahi nimapata mawazo mapya sio na yale mhando nlokua nayo mwanza
 
Naxhukulun kwa mchango wenu mzur yamenfungua akil
 
Kumekua na tofauti kubwa nilivyo kuwa single na nlivyo sasa na mwanamke.
Na tifauti kubwa nimekua mtumiaji hela vibaya kiasi ambacho nashindwa kuzitunza kama ilivyokuwa hapo awali kiasi hata nguo mpya sijanunua kwa mda mrefu.
Najiuliza:nirudi kuwa Alon but Happy ingawaje tabia za mwanamke wangu ni nzur hana tatizo?
Tukiachana na mabadiliko mengine meng madogo madogo
Nisaidiwe ushauri hapa wadau

Kukimbia tatizo si njia sahihi ya kutatua tatizo, dawa ya kutatua tatizo ni kukabiliana nalo! Kaa chini na tafakari nini chanzo cha matumizi yako ya pesa kuongezeka. Ni kweli mpenzi wako ndo kachangia au kuna tatizo kwenye upangaji wa budget? Nini kinasababisha matumizi yawe makubwa? Na vipi vi element vya uchoyo, Samahani lakini!
 
Back
Top Bottom