Nahisi nina matatizo au sielewi ni mgeni sana wa haya mambo. Iko hivi, mwanamke nikimsaundisha ikizidi wiki mbili sioni muelekeo namkaushia.
Mimi ni wale wanaume ninaeamini katika "love at first sight". Yani ninakua na upendo mwingi sana kwa mwanamke anaenikubali mapema. Ule wimbo wa fid q sijui usinikubali haraka naonaga hau-apply ktk feelings zangu.
Kwanza mwanamke nikiona ananizungusha zungusha hua nahisi hajanipenda mimi kama mimi, Yani muonekano wangu haujamvutia kuniweka ktk hisia zake. Hua naona kunizungusha zungusha anajipa mda wa kunifanya niongeze vitu vya ziada tofauti na mm nilivyo naturally ili niweze kumvutia kwa mfano nianze kumuhonga vijisenti, au nibadili mfumo wangu wa maisha uendane na anavyotaka yeye na mwisho wa siku aje kunipenda kwa vitu ambavyo vikija kuisha na yeye upendo utaisha au ntajikuta naishi maisha ya kuigiza tofauti na mm nilivyo ili nimridhishe yeye tu.
Sijui imekaaje hii...
Sent using
Jamii Forums mobile app