happy amos
JF-Expert Member
- Feb 23, 2012
- 251
- 434
Natumain mu wazima
Samahan kwa kuwachosha na hii mada yangu ya kila siku imekosa ufumbuzi ndio maana huwa nairudia sana humu.
Naomben ushauri kwa hili. Mara nyingi tumekuwa tukikwazana na mwenzangu(mume) sababu ya mambo mbalimbali. Tuna mwaka na zaidi sasa lakini binafsi nimefika kwa shida sana. Mwanzo tulikuwa tunaishi pamoja ila kwa sasa kahamishwa kikazi nami najipanga.
Binafsi moyo wangu hauna amani kabisa kwa sababu jamaa familia yake 100% inamtegemea yeye. Sio baba, sio mama sio wajomba sio shangazi sio kaka zake mpaka inafikia hata shida za wake wa ndugu zake kama wakiugua yeye ndio anagharamia.
Mimi sijakataa lakini maendeleo ya familia hakuna. Alidai nimpe muda amalizie maendeleo ya kwao lakini hayaishi sababu
akitaka kupiga hatu mjomba anashida anapewa, akitaka kupiga hatua shangazi anatoa tatizo anapewa.
Kinachoniuma nilishamwambia anapata karibia milioni 2 kwa mwezi hivyo mimi kwa mwez anipe laki 3 tu nami niongezee laki 1 za maendeleo ya ndani maana na sisi tuna maisha yetu. Anakubal lakini mwisho wa mwezi ukifika chenga nyingi.
Mwezi uliopita alitoka semina alipata karibia mil 3 nje ya mshahara lakini mimi nilipewa elfu 30 tu za matumizi. Waliitana na ndugu zake mjini walichonunua sijui ila naambiwa hela imeisha hata kununua sufuria hapana. Nikimwambia ananiambia nitulie kwanza akimaliza kwao ataanza maendeleo na kwetu.
Mimi nina biashara zangu, hapa ninapofanyia kuna changamoto za huduma ya M-PESA tukapanga na mume wangu nikaanza kufatilia leseni na TIN namba kwa gharama zangu. Nikapata nikafuatilia TIL ya M-PESA. Nimepewa namuomba anichangie hea ya kununua simu akacheka nikanunua mwenyewe.
Nikamuomba aniongezee mtaji laki 2 kakataa anadai ana ujenzi kwao nikamuomba basi anikopee nitakua narejesha 50 kwa mwezi kakataa. Ikabidi nikamkope mama nifanye kazi. Ajabu nikipata faida naambiwa ninunue vitu kidogo kidogo vya ndani.
Serious napenda kuolewa lakini huyu mwanaume hapana bora nikae mwenyewe ijulikane moja.
Nikamwambia tuachane kabembeleza ndio anakuja baba yake mdogo kutukalisha. Sasa nieleze ukweli wote au nitaeleweka vibaya? Maana mimi nimechoka na nimewaambia nyumbani warudishe tu mahari yake
maana mwenzangu hanithamini kama mke!