Je, niolewe naye? Baba yake alizaa na Mama yangu

Mama, kumbuka hapo nyuma umejitetea/jieleza kuwa hamchangii baba wala mama. Nami nimekujibu from the same angle. Sasa umekuja na hoja ya mahusiano ya damu. Ok!

Ikiwa A anamwita B, baba ni lazima atamwita mama yako mama. A na dada yako wanauhusiano wa damu wa moja kwa moja zaidi ya yale ya mtoto wa baba mkubwa. Then, jiweke wewe kwenye nafasi ya A. Je! Ni halali kwake kumwoa mtoto wa mama mkubwa (mke wa baba mkubwa) ambaye hakuzaa na baba mkubwa? Ndani ya mada, je ni halali A kumwoa mtoto wa mama wa kambo ambaye mama wa kambo hakuzaa na baba yako?


Du! LOL, nimeshindwa hata kuunganisha hata huo undugu unao ukokotoa lol
 
mmh hili suala linahitaji busara sana maana ukiangalia huyo ni kama kaka yako coz ni kaka wa dada yako.hata kama baba yake hakuoana na mama yako lakini mtoto waliezaa ndo alieleta undugu wenu.kwahiyo huyo ni kaka yako.ila jaribu kufuatilia kimila zaid na ww mwenyewe msimamo wako uko vp


Mie nampenda ila sijui kama ni sahihi kuolewa na yeye au hapana.
 
huyo ni ndugu yako usioe wala kuolewa naye

kuna madhara ya kiafya, kijamii na kiakili

kiafya kama kuna magonjwa ya kurithi yataendelea badala ya kukomeshwa

kijamii je unaendaje kutoa mahali kwa na nani atakukubali

kiakili, hamtafurahia maisha yenu ya ndoa kutokana na taarifa mchanganyiko mlizo naz

kidini, ka kuwa ni ndugu haikubaliki ninyi kuoana

tulia tafuta mwingine

Kiafya: magonjwa ya kurithi yanakuja vipi kama hakuna connection ya damu?

Kijamii: familia yangu na yake ni tofauti. Tumekutana ukubwani tu. 2 Months ago.

Kiakili: Sina uhakika.

Kidini: Unaweza ukanisaidia source? Kuna moja imetolewa hapa lakini haiendani na case hii.
 
Incest ni mpaka kuwe na blood relationship. Hawa wana relate vipi kwa damu hata iwe incest? Big lady olewa tu provided mnapendana

Ndugu yangu, we acha tu. nazidi kuchanganyikiwa hata sijui nifuate lipi.
 
mmeshamegana nyie!

Acha hizo bana. Hatujamegana. Kama tumemegana ningeshindwa nini kusema? Kwani mie mtoto mdogo!

Acha hisia mbaya! lol

Jinsia gani weye tukupake wanja? Haluuuuuuu!
 
Kimsingi huyo kijana si ndugu yako kwa damu ila ni ndugu ya huyo dada yeko mwingine kwa kuwa wanachangia baba. Nawe ndugu yako hi huyu dada ambaye mnachangia mama. Juu ya kuolewa ni ruksa kisheria, vinginevo mila na desturi (heshima na utu wema) unatumika kama kanuni nyingine ya kuwakataza kuoana. Ongea na mama yako mzazi usikie atakushauri vipi.

Asante sana nitaongea na mama!
 
Mamamia,watoto wa damu moja si wale tu waliozaliwa ndani ya ndoa. Hata wale waliozaliwanje ya ndoa kama wanachangia damu kwa njia ya wazazi au mzazi mmoja bado diniinatambua kwamba wako ndugu wa damu hata kama uhusiano wao hautokani na ndoahalali. Hivyo kama wako ndugu wa damu hata dini haikubali kufungisha ndoa hiyokwa sababu za kiroho na za kibaolojia. Tunapoongea mambo ya vizuizi vya ndoahasa cha undugu (consanguinity) hatuangalii uhalali wa mahusiano ya wazazi wawahusika bali uchangiaji wao wa damu.

Kwa kesi hii ya huyu dada, kimsingi hakuna uhusiano wa damu kati yao kwa vilewazazi wao wamewazaa na partners wengine. Pili, hao wazazi hawaishi pamoja kamamme na mke (walizaa kama marafiki tu na urafiki ukaisha). Kwa hivo huyu dadakwa mawazo yangu aweza olewa na yule kijana, vinginevo heshima za mila na ukoovinawashauri vinginevo.

Duh JF bana! Asante kwa mwongozo. Hoja kinzani umezisoma lakini?
 
Best ni kweli busara inahitajika ndo maana nakuja kwenu.

Kuhusu Mila ni mchanganyiko mtupu wa makabila na hata sijui ni mila ipi ya kufuata.

Huyu Mwanaume anayenipenda ni kabila XY. Baba wa Kumzaa kabila X. Baba aliyemlea toka mdogo kabila Y. Mwama yake ni kabila Z.

Mimi baba yangu ni kabila Q na ni mchanganyiko wa makabila mawili. Mama yangu kabila lake ni W.

Nimelewa na ndugu wengine so hata mila sizijui. Same kwa huyo Mwanaume A. labda nianze kuulizia. Ila kabla ya hapo ngoja nipate ushauri kwanza.

Wewe hii habari ya kutunga au?
Unatutajia kabila xy, y sijui nn huko ndio tueleweje?
Mm nataka kukushauri kwa kuangalia mila za makabila husika. Yataje.
 
Wewe hii habari ya kutunga au?
Unatutajia kabila xy, y sijui nn huko ndio tueleweje?
Mm nataka kukushauri kwa kuangalia mila za makabila husika. Yataje.

Haaaa haaaaa umenifurahisha. Hebu nieleze hapo mila za makabila yafuatayo zinasemaje?

Wabondei
Wanyakyusa
Waluguru
Wangoni
Wasukuma

Huo ndo m,changanyiko halisi. Please usiniulize zaidi.

Huyu Baba yake Mwanaume A ninayempenda, yaani Mzee B pia hakuwa ameonana na A miaka mingi pia. Ila alimweleza kwa sasa yeye amemwoa Binamu yake. Mzee B ni Christian. Ila sipendi kufuata mkumbo huo nahitaji kuwa na uhakika.

Lete nondo sasa . . . . lol
 
sasa hajakumega akutangazie ndoa! Umeona wapi hiyo?

We vipi jamani? Kipi cha ajabu? Si wote wako hivyo unavyofikiri. Watu wanasomana tabia kwanza na kuwa marafiki kabla ya kufikia uamuzi wa kuelezea nia. Wapo wanaoolwewa kabla ya mahusiano ya mwili.

Rudi kwenye mada bana!
 
Back
Top Bottom