Je, nini Siri ya Waarabu, Wasomali, Wahindi kuishi ukoo mzima nyumba moja kwa upendo?

MURUSI

JF-Expert Member
Jun 25, 2013
4,496
8,731
Hawa watu unaweza kuta kuanzia Babu, Bibi, wajomba, Mama wadogo, watoto, Wajukuuu, wote wanaishi nyumba moja na kwa upendo mkubwa mno.

Wabongo hii haiwezekani kabisa, make kusengenyana, kudharauliana na kadhalika kutakuwepo tu tena kwa wingi sana.

Na ndio basi hata hawa watu kwa kupigana tafu wako vizuri sana, wanainuana wao kwa wao.

Wabongo mtu kumpiga tafu tu kaka yake au Mdogo wake anaona hapa, hata saa zingine wazazi wake kabida.

Nini siri ya hawa watu kuishi pamoja kwa upendo mkubwa sana na kwa nini sisi tunashindwa?
 
Wanakua wakiona hayo

Sasa sisi tunakua unaambiwa hamna hata kukanyaga kwa aunt. Mara sijui mjomba wako ana roho mbaya, mara mama yako mdogo ni mchawi ukienda kwake usile chochote, unafikiri tunakuza kizazi cha aina gani!

Wao wanarithishana upendo, sisi tunarithishana chuki.
 
Wengi wao ni wabaguzi tu hawataki kuhama Posta na Upanga na kujichanganya Uswazi. Wengi wanaishi kifamilia baba analala na watoto wa kiume, mama na watoto wa kike. Mambo ya kujamiana mchana wakati wengine wapo kwenye mishe maisha gani hayo?
 
Nimewahi kujiuliza hilo swali miaka mingi nyuma na niliwahi kuwauliza wahusika. Wenzetu toka kuzaliwa uwa wanakubaliana na kuwekeana malengo ya pamoja kama familia. Hata biashara zao ni za pamoja. Wanaendesha familia zao kama kampuni na hilo upandikizwa toka mtoto anazaliwa.

Kuna mikutano na hata mipango ya kurithishana uongozi (succession plan). Sisi ngozi nyeusi tunaishi tu baba hajui anaipeleka familia wapi, mama na baba hawaelewani, michepuko inavuruga familia, majungu ndio mtaji, watoto hawajui wanasoma ili iweje yaani ngozi nyeusi ni full changamoto.

Hata tukienda ulaya na marekani hatuigi mema bali ni majungu na fitina ndio utawala. TUBADILIKE WATANZANIA.
 
Ni undezi tu

Na ndio maana unakuta hao waarabu kumuoa shangazi yake ni kitu cha kawaida. Halafu hii tabia nimeiona hadi kwa wapemba nao wame copy kwa Waarab.

Unakuta kibopa ana miaka 30 yuko kwao halafu geto lake linaangaliana na mlango wa dada zake halafu muda wote unakuta yupo ndani hajichanganyi na watu wengine tofauti na kabila lake.
 
Nilidhani kwakuwa labda wengi wao wana uchumi mzuri lakini mbona hata weusi kuna familia zenye uchumi mzuri lakini kuishi kama wahindi na waarabu ni ngumu?

Waafrika hatuwezi chokochoko za mawifi, mara ma mkwe, mara shemeji kafanyaje, mara binam kaja kusomea pale, mara bibi kaja kuugulia pale, mara shangazi kaachana na mmewe naye kaja pale. Mara mwali anashindwa kuenjoy mapenzi na mumewe kisa watu wamejaa nyumba hajiachii (kutoa sauti chumbani)😂 vita ya huu mkusanyiko Mungu ndo anaweza iamua.
 
Hawa watu unaweza kuta kuanzia Babu, Bibi, wajomba, Mama wadogo, watoto, Wajukuuu, wote wanaishi nyumba moja na kwa upendo mkubwa mno...
Siri Unayo hapo juu wote wanaishi nyumba moja na kwa upendo mkubwa mno.
 
Hawa watu unaweza kuta kuanzia Babu, Bibi, wajomba, Mama wadogo, watoto, Wajukuuu, wote wanaishi nyumba moja na kwa upendo mkubwa mno...
Hao watu tangu utotoni wanakuzwa hivyo, na mwisho wa siku nao wanaendeleza huo utamaduni. Unakuta watoto wao wanapopelekwa shule hawaendi kusoma ili waje kuajiriwa, maono yao mengi ni kupata maarifa tu ya kuendesha biashara zao na vitega uchumi mbalimbali walivyonavyo.

Ndiyo maana hata MO aliachia Ubunge Singida kurudi kusimamia Biashara za Familia. Sisi wengine tunagombania Ubunge tukiamini ndio njia ya mafanikio. Lakini bottom line, nadhani UTAMADUNI wetu ndio umetuponza. Tujifunze sasa, na tusiishie kupiga porojo humu.
 
Ni undezi tu

Na ndio maana unakuta hao waarabu kumuoa shangazi yake ni kitu cha kawaida. Halafu hii tabia nimeiona hadi kwa wapemba nao wame copy kwa Waarab.

Unakuta kibopa ana miaka 30 yuko kwao halafu geto lake linaangaliana na mlango wa dada zake halafu muda wote unakuta yupo ndani hajichanganyi na watu wengine tofauti na kabila lake.
Kama hiyo tabia inamfanya afanikiwe kiuchumi, wewe unaumia wapi!?

Punguza chuki uongeze siku za kuishi, wewe jichanganye achana na Mpemba..
 
Hata mm hili jambo nimeliona na kulipenda sana yaan hawa watu wanakua na umoja wa hali ya juu sana wanakaa sehem moja tena km wana uwezo ndo wanajenga nyumba kubwaaa hapo unakuta familia nzima wapo hapo.Pia hii inawasaidia sana hata kibiashara yaan kama ni kampuni ama biashara familia yote inajua kila kitu cha kampuni.

Sasa kwetu bongo mzee anaweza kua na hela ama kampuni ila hujui hata benki ana kiasi gani na akifa kampuni linakufa ama wanafaidika watu wa pembeni ambao alikua nao karibu nao.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom