Je, nimuache huyu msichana?

Kilichopon ni Kwamba wewe Humpendi tena huyu binti hivyo vyengine unavyoviongea ni visababu tu ili ujipe moyo kuona umefanya maamuzi sahiihi, Kwanza hujali hata kidogo na huyo ndugu yake alokwambia utumie akili alikuwa Sahihi kabsaa, kama ingekuwa unampenda na kumjali ni wewe ndo ungekuja na chakula mkakaa mkala na kuongea na sio kumuingiza mgonjwa jikoni, na bado huoni thamani yake??? Kama wewe unavyohisi maneno ya ndugu yamekutia hasira unadhani na yeye hasemwi na hao ndugu? WANAMPENDA NDO MANA WANAMSEMA YEYE NA WEWE, Na inaonekana una mambo mengi ya kijinga umemfanyia ndio maana ndugu zake hawakupendi.

Ila Ukimuacha huyo binti utarudi tena hapa kama sio kwa kutendwa na mwanamke mwengine basi kwa jambo lolote, ile Nuksi ulosema umetiwa na huyu dada sasa ndo unaibeba rasmi, na pia kama humpendi endelea na maisha yako huna haja ya kumuumiza, yeye atataumia kwa muda atasahau, ni wazi huna mapenzi kwa sasa.
 
UNA ROHO MBAYA SANA
UNA NUKSI WEWE
HUNA AIBU
UNA MOYO KAMA HITLER..
MTU ANAHAGAIKA UMEKAAUNASUBOIRIKUHUDUMIWA...
IPO SIKU UTAVUNA UNACHOPANDA..
MIZIGO GANI UNAMBEBESHA DADA WAWATU
UMENICHUKIZA SANA
MWANAUME UNAMTREAT HIVI HUYO..
ULIKUWANAE WANINI TANGU MWANZO SASA
LAANA HIYO
NDUGU ZAKEW WANA HAKI MAANA UNAMTESA NAKUMNAYAYSA
USHANICHEFUA
 
Lakini hata mm ningekwambia hutumii akili ilihali unajua mwenzako anateseka af we unafrai ukidhani ni upendo kua na roho ya huruma bhcii
 
Hujafa hujaumbika, mrudie dada wa watu. Achana na huyo ndg yake maana hawez hata kumuoa kama ukimuacha.
 
Wewe bado kavulana sana, muache huyo binti ateseke kwa muda mfupi baadae MOLA atampatia mme mwema amuoe ili wajenge familia nzuri, wewe baki na mishe zako, utashtuka siku ukikutana na asiye na NUKSI. Japo mimi mwanaumme lakini Umenikera sana kwa kukosa uvumilivu wa Kiume.
 
wewe ni wale sisi kwetu tunawapiga mawe....
 
Huwa nikikaa nafakari jambo moja linaloumiza sana kichwa changu siku zote. Sijui ya kesho juu yangu. Ukilitafakari jambo hili kwa umakini na utulivu wa hali ya juu~viburi, jeuri, sifa za kijinga, roho mbaya, fitina, unyanyasaji, unyanyapaa, uzinzi, uchoyo, ukatili na mambo yooote mabaya utajitahidi kuepukana nayo. Only God knows about our tomorrow
 
Wewe unatafuta sababu tu ya kumuacha hakuna la zaidi ni kwamba umemchoka..
 

Siku ukivuka stage uliyopo hivi sasa ya uvulana kuingia kwenye uanamme nadhani utakuwa na uwezo mzuri wa kufanya maamuzi yenye tija. Yaani wewe kuambiwa ukweli na kaka mtu unahamishia hasira kwa bint wa watu??!! Na walichokuambia ni ukweli mtupu! Kwa mujibu wa maelezo yako nasema wazi unamtesa bint wa watu kwa sababu unaona kama anakupenda sana na hana option nyingine! Ngoja nikuambie kitu mdogo wangu, siku mwanamke akichoka akasema basi na akaondoka, utalia na hatarudi tena na ndipo utakapotambua umempoteza mtu muhimu sana! Kaa chaka tafakari!
 
Nachokiona hapa ni mapenzi katika ubora wake,unampenda & u wish the whole world to know...mapenzi bhana yani utamtaja ata bila sababu.
 
Piga chini tuu mkuu unasubiri nini???

Umeshasema ana nuksi
 
Hivi wewe mtoa mada una akili nzuri kweli?Sio siri nimejikuta natoa machozi kwa jitihada za huyo binti juu yako.
Huna lolote unataka kumuacha sababu ya ulemavu wake,sio maneno ya ndugu zake.

Kwa jinsi anavyoonesha kukupenda maneno ya ndugu zake yanakwaza nini?
Jali na kuziheshimu hisia za huyo dada tafadhali,ukimuacha Mungu atakupiga pigo kali...hutokaa upate wa kukupenda kama huyo dada.
 
Kiukweli hutumii akili kabisa. Mgonjwa anajiburuta umejikalia tu killaza wewe.
Linaona sifa eti.
Badala anuambie apumzike na ampe maelekezo afanye yeye.
Kikubwa hapa ni hampendi huyo dada,angekuwa anampenda asingemuacha ateseke.
 
Kwa nilivyo soma huu uzi huyo mdogo wa huyo dada, hajakosea kukwambia unahitaji kutumia akili. Yaani umesaidiwa kiakili kifedha na kuwekewa chakula na huyo mdada akiwa bado anaumwa. Wakati wewe mzima huna msaada wowote juu yake, ama kweli huioni samani ya mtu mpaka yakukute. Mimi nasubiri mrejesho ukipata mwanamke mwengine halafu wewe uumwe akufanyie kama unavyo mfanyia huyo mdada.
 
Naomba nikuulize swali moja tu na unijibu ukweli. Ni hivi Katika kujiburuza buruza kwake wakati anapokuona kwa maana ya kukupokea au kukuandalia chakura wewe reaction yako ilikuwa inakuwaje na hasa mbele za nduguze.
 
Mimi Nadhani una hitaji msaada Wa kisaikolojia, hivi kweli mwenzio anakujali hadi kujiburuta umekaa tu uandaliwe chakula?? Hebu uwe na hoja za msingi labda Umepata mbadala huko
 
wakati huna kazi alikushauli alikua nawe karibu ulipopata kazi ukamwaga mungu anakupma akuone je ww waweza kumfalji m2 na kua furaha kwake kama yy alivyofanya mwanzo 2mia akili na kumbuka hujafa hujaumbka
 
Dah! Watu mnatafutaga laana wenyewe. Machozi ya huyo dada yatakurudia
Umemtumia wkt huna kazi, bado ukafukuzwa kazi ukamtumia, sasa hivi unamwona nuksi? Mbona hukuona pesa zake nuksi? Kuweni na huruma jamani mtu anapokupenda kwa dhati ridhikeni,
Huyo dada anakulilia sana leo ipo siku ata kubali matokeo, na ndipo utakapomjua Mungu ni mjombaako au shangazi yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…