Je, nimuache huyu msichana?

Utakuwa shetani binaadam
 
Povu
 
Dada wa watu hana kosa lolote. Kilichotokea ni kuwa ndugu zake wana uchungu kuona dada yao anakuonyesha upendo wa dhati lakini ww ndio haueleweki.
Embu jirekebishe mfariji, muonyeshe upendo wa dhati..
 
Aaaaah umenidhalilisha sana.... Huna utu na hufai kuwa Mume wa uyo binti. Muache atampata mume mwenye hekima..... Tafuta mwingine msumbuane
 
We ndo una nuksi sasa, hilo gubu la kuwaza mtoto wa mwenzio ana nuksi linatoka wapi. Na unapata wapi ujasiri wa kusema ana nuksi we kama humpendi mwambie sio kusema ana nuksi bwana
 
Mapenzi ni vita pambana ndugu kama kweli unampenda usimwache aumie kwa ajili yako kisa ndugu zake wanakutolea maneno makali ...je dada zako wakikwambia umwache huyo mpenzi wako kwa sababu hawampendi utafanyaje?
 
Mi nakushauri umuache kabsa tena mapema ili umpunguzie matatizo, halafu ktk kipindi hiki atapata mtu ambaye anampenda kwa dhati coz atamkubali hivyo hivyo na ulemavu wake
 
Nipigie taka kukupa tusi ila nimeogopa hapa kuna watu tunaheshimiana.

hivi just ndugu ndo kumwacha binti kwa kosa lipi? wacha kupotezea watu bahati kuna watu wanataka upendo wa binti huyo. acha kuchezea akiri za watu.
 
Mkiwekwa kwenye mizani, maamuzi yako yatakuwa mepesi kuliko umri wako. Jitahidi ubalance mizani. Ni hayo tu...
 
kama hii sio hadithi kama zilivyo hadithi zingine za kutunga...inawezekana wewe una matatizo tena makubwa pengine umri wako ni mdogo teena sana...umejuaje kama mtu ni chanzo cha wewe kufukuzwa kazi? hizo ni imani za kitoto...but uamuzi ni wako hapo kwangu mimi imenigusa tena ndani kabisa uvunguni mwa moyo wangu na roho ya huruma imeniingia..kwakweli kwa karne ya leo kumpata msichana ambaye anaweza kukuvumilia kwa hali yoyote ya kimaisha huyo ni wa kumshika bila kumuachia....ila hayo ni yangu...kama unaona inafaa unaweza ukamuacha kwani tumetofautiana wengine tunahuruma wengine wamepewa huruma machini ila ndani ya mioyo yao ni makatiri zaidi ya simba mwenye njaa
 
The world is not fair.... Pole sana uyo dada kwa kukutana na mpenzi hewa
 
Huna mapenzi ya dhati kwa huyo dada kwa swala kama hilo wala hukuhitaji kuja hapa kuomba ushauri wa kumwacha.....umegundua anakupenda kwa dhati unalipa kwa kumwacha wapo wanaotafuta wenye upendo wa kweli wamewakosa wewe unajifanya huelewi ipo siku utaelewa lakini utakuwa umechelewa
 
Hukua unampenda huyu dada,kama unampenda kaka zake hata wakufanyie visa,huwezi kumuacha tena ukizingatia,huyo mpenzi wako sasaivi ni mgonjwa,tumia akili kijana kupenda sio mchezo,inahitaji kujitoa kwa shida na raha.
 
Kiukweli hutumii akili kabisa. Mgonjwa anajiburuta umejikalia tu killaza wewe.
 
Kwani wewe unampango wa kumuoa huyo binti au hao ndugu zao..???...Tafakari imeandikwa utawaacha wazazi wako utaungana na mkeo siyo ndugu zake...
 
Huyo ndio mwanamke wa kua nae utakua juta kama utamtosa hutopata tena mwanamke kama huyo ushauri wangu kua nae
 
Kama nikutie kibao cha kihindi kwanza
 
Huwa wanasema wanawake hawajui wanachokitaka naanza kuwa na hisia kuwa baadhi ya wanaume hawajui wakitakacho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…