Je, nimuache huyu msichana?

Kweli mkuu huyu hana kabisa sababu ya msingi ya kumuacha huyu binti kwani amekiri mwenyewe huyu binti anampenda anamsaidia kwa hali na Mali sasa sijui anataka nini tena[emoji779] [emoji779] [emoji780] [emoji780]
 
Hapo ndipo ninapoona tofauti ya mapenzi ya wazungu na waafrika, ingetokea uzunguni hiyo huyo mzungu angemuoa huyo binti wakati huo kwa kuonesha upendo wake kwake na ndio maana wengi wanafunga ndoa na wapenzi wao waliopo kitandani ambao mara nyingine unakuta mwanamke ana stage 4 cancer, lakini kibongo bongo kuugua ndio kwanza inakuaga sababu ya kuachana, Tujifunze kupenda kutoka moyoni bila kuangalia uzima wa mtu, sisi ni wa mwenyezi mungu na kwake tutarejea tusiishi kama tutadumu milele, nakushauri hivi, usiende tu kwa huyo dada hiki ndio kipindi cha kupeleka posa, kwanza uzinzi ni zambi kwa dini zote
 
Well said.huyu jamaa ni shetani kabsa nazani.
 
Kwakweli hata mimi kaniudhi sana nabaki najiuliza sijui wanaume wanataka nini kwa wanawake!!?
 
Kwakweli hata mimi kaniudhi sana nabaki najiuliza sijui wanaume wanataka nini kwa wanawake!!?
Huyu anataka laana, furaha kubwa maishani ni kupendana na mpenzi/mke/mume wako katika shida na raha, upendo hufanya mtu hata akiumwa ajione mzima, hata awe katika matatizo makubwa vipi lakini ukipata upendo unaona kama tatizo dogo tu.
 
Huyu binti hana kazi. Kipindi hajaugua alikuwa akifanya kibarua tu. Pesa aliyojitolea kwangu si kubwa ila ukubwa wake ni kule kujinyima yeye na akanipa mimi. Msema ukweli ni mtu wa Mungu.
Sasa nikuulize wewe hasa unachotaka nini au unataka mwanamke gani? Kumbuka " UNACHOKITUPA KWA DHARAU WENZIO WATAKIOKOTA KWA FURAHA" na ukumbuke kuwa " NGUO YA ZAMANI NDIO DEKIO JIPYA" huna akili kabisa laana itakupata kwa hayo machozi ya huyo binti halafu utatafuta wachawi fyuuuuuuu [emoji57]
 
Sijaona sababu ya kumuacha,na kuhusu hao ndugu wameona dada yao anaumwa na anakuhudumia ww wanaona huruma kuwa anajiumiza kwa ajili yako na ww humkatazi
NB😀amu ni nzito kuliko maji
 
Punguza kuangalia tamthilia dada
 
Kwanza ungekua muungwana wala usingethubutu hata kuuliza ungeona aibu et "JE NIMUACHE HUYU MSICHANA? Huna haya wala huruma katili mkubwa wewe subiri laana zako.
 
Ndugu usifanye kosa kama hilo, unakili amekusaidia kwenye shida na raha hadi umepata kazi.
Mbona sasa wewe unashindwa kuwa imara kwenye shida inayomuhusu.
Usimuumize kwa sababu ya ndugu zake.
Tafadhali rudi kwake haraka ndugu huo ni ukatili kama ukatili mwingine.
 
Mbona yy alikusaport why u. hata utakayeoa hutapata aman inaonesha unapenda ukiwa na shida.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…