Je nimemjibu jamaa vibaya kuhusu mchumba wangu??

Yashanikuta mie kwa mademu wawili, mmoja wakati nimemaliza chuo natafuta kazi akafanya the same issue, ilinichanganya coz nilikuwa nimepanga nikipata kazi nianze mchakato wa ndoa, mungu akanisaidia nikamove on, akaja mwingine pasua kichwa, nikamlipia na ada ya chuo mzumbe maana mama yake alikosa pesa, akaja nikapigiwa simu na mtu akanambia the same story nikamtimua nae. Leo wote wanalalamika hawajapata mwanaume kama mie, kwa bahati nzuri mie nishaoa, nina kijana wa kiume though i cant say am happy with marriage but am satisfied.

Hongera sana kwa kuwa na family mkuu, yeah wa namna hiyo wengi wao wanakuwa hawafiki popote wanachezewa na kuachwa tu basi hamna mpya mkuu, ila hongera sana kaka kwa kujenga family na kuwa na mtoto.
 
Umemjibu vizuri kabisa ila kuhusu kuwasiliana na jamaa yake huyo nahisi kama utaonekana kuna jambo bado unalitaka kwao we wapotezee tu mkuu... those r gals mapenzi ni huku mnaonana daily mkikaaa miaka no kuonana baaasiiiii mtakua kila siku mnagombana bila sababu.......... ila nakupongeza sana kwa kuongea na mtwasi kiutu uzima me ningekata simu yenyewe na kubadili line 4rever
 
Duuuu wewe kweli noma aiseee sio mchezo kumbe ndio hivyo kwa hiyo naona kama haya mambo yangekukuta usingelaza damu si ndo??


nisingelaza damu, yaani wewe watu wengine kauzu kweli, hapo ningeuchuna angejifanya kurudi as if hakuna kitu kilichotokea, tena na malawana kibao
 
Mkuu wangu nashukuru sana kwa mawazo yako naona ni the same story,na jamaa alitumia tu kigezo cha kusema anamuowa ila siwezi juwa kwa kweli,na sikutaka kutafuta ugomvi kabisaaa zaidi ya kuongea kwa utaarabu zaidi,yeah mkuu me zaidi nawatakia maisha mema kama walivyopanga.

How is your baby boy mkuu,nifikishie salam zangu aisee

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums

Zimefika kaka. My baby boy is fine.
 
Mkuu Papizo pole sana kwa yaliyokukuta..I can imagine how you feel right now, be calm endelea na maisha yako vizuri.

Mie ilinikuta mpenzi wangu tuliyekuwa kwenye harakati za kuoana alinichenjia mbele ya mwanamke mwingine out of blue kwa ghadhabu za hali ya juu tena akitamka kitasha 'I don't love you, I love her and she's carrying my boy' . Niliduwaa kama shoti imenipiga, binti wa watu nikajikaza kisabuni. Halafu nilikuwa nchi ya watu, kila mtu mji wake na familia zetu zinafahamiana.
Mwanzo ilikuwa ngumu ila siku zilivyoenda uchungu ukapungua pole pole japo sitosahau...nilikaa mwaka na nusu bila relationship, nafurahi kuwa na mtu mwingine sasa hakika nashukuru kukutana na huyu kaka. I can't trade him for anything.

Ndiyo changamoto za mapenzi hizo mkuu!!
 
Last edited by a moderator:
Mbona mi na wewe kila siku mapanga shaaa?

@Bishanga kama unamaanisha kwa Lizzy nishaahirisha mipango ya kwenda kwenye pool yake coz kwa mujibu ya sredi moja ya juzijuzi nimegundua na yeye ni mpalestina, naogopa asije nikanumba bure! tena nackia kifo cha kwenye pool kibaya!
 
Mkuu ni hatari sana hawa watu asikuambie mtu kabisaaa, na omba hii kitu isikutokee kabisaaa....inauma sana. alafu bila aibu kabisa

Mkuu pole sana umenikumbusha mbali sana na mimi iliwahi kunitokea kama yako, nikawa mpole nikamalizana na huyo demu kishikaji na mpka leo ananimaindi lakini nilishamfungia vioo nafnya mabo mengine.

Hata kama ungemjibu vibaya hakuna shida ingekuwa ni provocation tu, na huyo malaya alikuwa anajiosha kwa basha wake tu. Hafai na wala usimsamehe hata iweje indapo kikiwaka huko.
 
Nashukuru sana kaka kwa ushauri wako mzuri na wa kutia moyo,ni kweli kabisa sielewi nini hasa kilikuwa kinaendelea I don't know serious,zaidi pamoja na hekima na vitu vyote nilivyofanya na kusema nafanya haya mambo coz nitakuwa nae for life then ndio nimeambulia haya yote,so zaidi me nawatakia mafanikio mema na yenye kheri, mkuu again thank u sana vile vile nikakaaa nikasema wanawake wapo wengi sana why niwe na kinyongo na mwanaume mwenzangu.



Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums

Okay hiyo ndo hekima....piga moyo konde mkuu maisha lazima yaendelee
 
Wakuu naomba msaada,maana leo nimepata drama ambayo sijawahi kuipata,nitaandika inshort tu,actual nilikuwa na mchumba niseme ambayo hivi mwezi wa saba narudi tuliplan maisha na kwenda kwa family,sasa kwa vile tupo mbali tukawa tunawasiliana sana na tukawa tuna share password zetu,basi ikafikia wakati nikaona mambo ya ajabu ajabu mara kachange password nikimuuliza hana sababu again ya kuniambia na attitude akawa anayo na dharau nyingi,hapo hapo tufahamu sijaanzana nae jana wala leo since nipo form 1 mda mrefu sana tupo wote.
Kama 2 months ilifikia akaniambia mimi na wewe basi eti nina wanawake wengi sana nikamuuliza ume prove ninao??akawa hana la kunijibu,nikamwambia ok fine hamna tatizo na maisha mema,sasa week kama 3 zilizopita akaja kuniomba msamaha na kusema nimsamehe me nikamuelewa nikamsamehe coz sikutaka relationship ife hivi hivi nikakaza moyo nikamsamehe.

Lakini tulivyokuwa tunawasiliana nikawa naona kuna somethin wrong sio normal nikamwambia akasema ananipenda sana hamna kitu. Na nimuamini nikamuuliza sasa mbona una tabia za ajabu ajabu anasema ndio nilivyo,basi me nikawa mpole sana na mvumilivu kwa kweli kwanza huwa sipendi kugombana kwa ajili ya vitu vidogo.

Sasa leo hii nimepigiwa simu mchana majira ya saa kumi namsikia mchumba wangu ananiambia kwamba ongea na bf wangu nikamuuliza unasemaje??na wewe ni nani??akanitajia jina lake coz sikuamini kama ni yeye,akasema ongea na bf wangu mwambie kwamba mimi na wewe tumeachana,me nilishasemaga sitokuja kugombana kisa mwanamke.akampa simu jamaaa akawa anawaka vibaya sana nikamwambia kaka calm down sawa wala usijali,akaniambia nimeona sehemu fulani umetumiana message za ajabu ajabu na huyo msichana wewe ni nani??Nikamjibu kwanza hajakuambia mimi ni nani??akasema wewe ndio niambie nikamwambia niulize swali lingine kipindi hicho kichwa hakifanyi kazi,akaniambia huyu ni gf wangu na next week naenda kutoa mahali kwao,nikasema ohhh ok sawa nikamuuliza umeanzana nae lini akasema miaka 2 iliyopita,me nikakauka kimya,akasema basi naomba mawasiliano yaishe na mke wangu nikamjibu wewe ni ndugu yangu na sisi wote ni wanaume so mkuu usijali zaidi tuzidi kuwasiliana sisi wote ni ndugu,nimemjibu kisomi na sikuonyesha kupanic,

Je wakuu wangu kuna mahali nimejibu vibaya??au yule alikuwa mchumba wangu kumbe mwanamke ana mwanaume mwingine kulikuwa na haja ya mimi kugombana na jamaa kwa ajili ya mwanamke??je majibu niliyomjibu kuepusha shari na kumuachia mwanamke nimefanya vizuri au nimekosea??

hujafanya vibaya.umejibu kistaarabu yamekishwa n then ucjute maana wewe sio ulosababisha hayo yote
 
Kumbe na nyie wanaume hua yanawakuta enh?pole sana take heart and move on!


Yeah yapo mbona sana tu sio mimi tu ukifatilia hii thread utaona kuna wengine pia yamewakuta ila me naona ni kutokujua tu nini unataka ndio maana inakuwa hivi but nimesha move on
 
Umemjibu vizuri kabisa ila kuhusu kuwasiliana na jamaa yake huyo nahisi kama utaonekana kuna jambo bado unalitaka kwao we wapotezee tu mkuu... those r gals mapenzi ni huku mnaonana daily mkikaaa miaka no kuonana baaasiiiii mtakua kila siku mnagombana bila sababu.......... ila nakupongeza sana kwa kuongea na mtwasi kiutu uzima me ningekata simu yenyewe na kubadili line 4rever

Yeah pale nilimjibu kisanii tu kumuonyesha as i dont care anything kimetokea kwangu me ni powa tu ndio maana,Nashukuru sana kwa mawazo yako ya kutia moyo. Mkuu ungekata simu na kubadili number ungeonekana as umekubali naunaogopa ndio maana
 
nisingelaza damu, yaani wewe watu wengine kauzu kweli, hapo ningeuchuna angejifanya kurudi as if hakuna kitu kilichotokea, tena na malawana kibao

Basi wewe kiboko daaaa, ila ndio hivyo sasa unajuwa ukilipiza basi itaonekana kama una kinyongo fulani na haupo happy ndio maana nikasema wacha nipotezee na niyamalize kiutu uzima na kutokuwa na chuki yoyote maana yametokea basi.
 
Kuna siku moja atajikuta amekuwa mpenzi wa ule wimbo wa R-Kelly unaoitwa "If I could turn back the hands of time"
 
Mkuu Papizo pole sana kwa yaliyokukuta..I can imagine how you feel right now, be calm endelea na maisha yako vizuri.

Mie ilinikuta mpenzi wangu tuliyekuwa kwenye harakati za kuoana alinichenjia mbele ya mwanamke mwingine out of blue kwa ghadhabu za hali ya juu tena akitamka kitasha 'I don't love you, I love her and she's carrying my boy' . Niliduwaa kama shoti imenipiga, binti wa watu nikajikaza kisabuni. Halafu nilikuwa nchi ya watu, kila mtu mji wake na familia zetu zinafahamiana.
Mwanzo ilikuwa ngumu ila siku zilivyoenda uchungu ukapungua pole pole japo sitosahau...nilikaa mwaka na nusu bila relationship, nafurahi kuwa na mtu mwingine sasa hakika nashukuru kukutana na huyu kaka. I can't trade him for anything.

Ndiyo changamoto za mapenzi hizo mkuu!!


Kwa kweli acha tu hii kitu ni ya kuisikia kwa wengine ni kama unaanza maisha moja, ila ndio hivyo now nipo normal nashukkuru munngu na nimesha move on tayari, ila siku zote shida zinampata binadamu, ila ndio hivyo now nimeplan kutulia kwa mda kwanza na kuangalia kwanza maisha yanaendaje maana ni hatari
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom