mshamba_hachekwi
JF-Expert Member
- Mar 3, 2023
- 24,944
- 81,593
Unapenda vitu vingi hujui ufanye kipi....hasa kuhusu passion
Tatizo linaweza kuwa kwamba unapenda vitu kwa nje. Yaani labda ukisikia fani flani inalipa sana unaitamani, hivyo....
Sasa unatakiwa uamue kufanya kitu kimoja kati ya hivyo, kwa nguvu zako zote, hivyo vingine fanya kama burudani(hobbies) ikiwezekana.
Fanya kimoja kwanza, kwa ufanisi, ili uone matokeo.
Lakini sikushauri uachane na 'passions' zako zote, nimesema vingine unaweza fanya kama hobbies au ukawa unavifanya kwa juhudi ndogo. Lazima vitakusaidia mbeleni....
Kwasababu wazungu wanasema 'Jack of all trades, master of none, but still better than a master of one'