Je, ni wangapi wasiotamani kupata watoto?

Mie kinachonishangaza hapa kwenye hii thread ni wakaka kushangaa wadada wasiopenda watoto..ilhali wao wanakana mimba zao kila siku, mngekua wanaume mnapenda watoto kama mnavyojitabainisha humu...single mothers wasingekuwepo..
 
Kuna watoto ukiwauliza kama ingekua wanachagua wazazi kama wangekuchagua uwe mzazi wao hakika watakataa. Halafu unakuta mtu huyo nae yuko kifua mbele kumsimanga alosema haitaji kuwa na watoto[emoji134]
 
Linapokuja swala la sheria za Mungu hakuna excuse ya Nabii au mtu wa kawaida.

Wewe upewe mbegu, upewe uwezo wa kuzaa, upewe na muda bado usizae wewe huna maana.

Hata mti usiozaa matunda unapaswa kukatwa. Hauna maana
Haujajibu swali! Mitume na manabii ambao hawakuzaa nao hawakuwa na maana au unamaanisha mtu awe na maana mbele za nani?
 
Hahahaa! Leo mada mezani ni ulazima wa kuzaa. Usibadilishe mada
Teh unajitoa ufahamu eenh? We si tunakujua huchelewi sie tulikuwa tunatahadharishana tu kuwa muda wowote unaweza ukabadili gia angani ndege ikajikuta imetoka nje ya radar imeenda kusikojulikana!
 
Dunia ipi hiyo?

unajua dunia zaidi ya robo tabu bado haijakaliwa na watu?

Kama umewahi kuzunguka duniani, walau kwenda Ulaya huwezi ongea upuuzi kama huo. Dunia bado sana.
Nani aliyekuambia dunia inatakiwa ikaliwe na watu hadi ijae yote? Wewe kama ni msomi ilitakiwa ujue kuwa sehemu nyingine duniani zinatakiwa zibaki zikiwa na maliasili kwa ajili ya mzunguko wa hewa ya oskijeni!
 
Kuna watoto ukiwauliza kama ingekua wanachagua wazazi kama wangekuchagua uwe mzazi wao hakika watakataa. Halafu unakuta mtu huyo nae yuko kifua mbele kumsimanga alosema haitaji kuwa na watoto[emoji134]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Usijali mimi ningekuchagua wewe wewe
 
Huyo anajua alichokifanya. Hakuna mwanamke mwenye akili timamu na mkamilifu asitake mtoto, kuwa na watoto siyo lazima wakusaidie uzeeni na hili halija wahi kuwa lengo, bali watoto na mapambo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…