Je, ni vitu vingapi vilivyoibwa Afrika na sasa vipo katika makavazi tofauti duniani?

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
1575866855693.png

Ni jogoo mwenye historia yenye utata ambaye amesafiri mbali zaidi ya taifa la Nigeria anakotoka - na sasa anatarajiwa kurudishwa nyumbani.

Chuo kimoja kuu cha Cambridge kimetangaza kwamba kitarudisha mojawapo ya kile kilichotajwa kuwa shaba ya Benin , kilichoibwa kutoka mji mkuu wa Benin ambao ndio taifa la sasa la Nigeria , zaidi ya karne moja iliopita wakati wa uvamizi uliotekelezwa na Uingereza.
Jogoo huyo kwa jina 'okukor' alikuwa amewekwa katika maonyesho katika jumba la maankuli la chuo hicho hadi 2016 , wakati wanafunzi waliposhinikiza liondolewe na kurudishwa kutoka taifa lilikotoka.

Chuo cha Cambridge kilisema katika taarifa yake kwamba: Bila shaka sanamu hiyo ya jogoo iliibiwa kutoka mahakama ya Benin na kupewa chuo hicho 1905 na mwanafunzi wa chuo cha father of Jesus.

Kiliongezea kwamba saamu hiyo ni ya mahakama ya Benin- wanaokuza tamaduni ya watu wa Edo.

Kurudishwa kwa utamaduni uliotoweka
Tangazo hilo limechochea wito zaidi ya vito vya zamani vilivyopo katika majumba ya makumbusho ya Uingereza kurudishwa katika mataifa vinakotoka. Idadi kubwa ya vito hivyo viliibwa .

'Tunazungumzia kuhusu shaba ya Benin , maeneo kutoka Afrika na Asia. Viliibwa', Alisema Profesa Kehinde Andrews kutoka chuo kikuu cha Birmingham.
''Sababu ya pekee ya vito hivyo kuwa hapa ni ukoloni. Uingereza inahitaji kuelewa kwamba ukoloni ulimalizika zamani na sasa uwajibikaji uliosalia ni kurudisha vitu hivyo kule vinakotoka''.

Mjadala unaoendelea Uingereza uko sawa na wito unaoendelea kushika kasi katika maeneo mengine ya bara Ulaya , hususan nchini Ufaransa , ambapo rais Macron ameagiza kurudishwa kwa vito vya Afrika barani Afrika katika kipindi cha miaka michache ijayo.

Katika hafla moja iliofanyika mji mkuu wa Senegal Dakar, taifa hilo lilirudisha chombo kimoja- upanga uliokuwa ukimilikiwa na Omar Saidou Tall, ambaye alitawala maeneo ambayo yanajulikana kama Guinea , Senegal na Mali katika nusu ya pili ya karne ya 19.

'Nilidhani ni hadithi'
Kwa sasa upanga huo umewekwa katika jumba la makumbusho la ustaarabu wa watu weusi katika mji mkuu wa Senegal Dakar.
Rais Sall kulia akipokea upanga wa Omar saoidou Tall wakati wa Sherehe
Haki miliki ya pichaAFPImage captionRais Sall kulia akipokea upanga wa Omar saoidou Tall wakati wa Sherehe

Upanga huo wa chuma uliopinda una shaba nyeupe kutoka Ufaransa na eneo la kuushikia lililoshonwa kama mdomo wa ndege.

Umehifadhiwa kwenye shefu yake ya ngozi kwenye jumba la makumbusho kwa mkopo kutoka Ufaransa, lakini wabunge wa Ufaransa watapiga kura ya kuamua iwapo wataurudisha kabisa upanga huo pamoja na vito vingine.

Momodou Tall, mjukuu wa Omar tall aliambia BBC kwamba andhani kwamba upanga huo haukuwepo.
Ahmadou Sekou Tall, mwana waa Omar Tall


"Kuna picha zingine za yeye akiombea upanga kwa sababu amewashinda wakoloni," alisema Momodou .
Wakoloni wa Ufaransa waliiba hazina zilizokuwepo katika maadara ya Segou, Thiam amesema. "Ni matumaini yangu kwamba vitabu vyetu vilivyoko Ufaransa vitarejeshwa."
Shaba ya benini ikiwa katika maonyesho nchini Uingereza 2018

Hazina za taifa zilizoibwa
Wakati wa ukoloni huko Afrika, maelfu ya mabaki ya vitu vya kale vilivyoibwa kwa sasa vinaoneshwa katika makumbusho ya Ulaya.

Lakini kuna baadhi ya taasisi ambazo zimekubali kurejesha vitu hivyo vya kale. Vifuatavyo ni baadhi ya vitu hivyo vya zamani ambavyo ni tunu kwa mataifa yao.

Shaba za Benin
Shaba ya benin ikiwa katika maonyesho nchini Uingereza 2018
Shaba ya benin ikiwa katika maonyesho nchini Uingereza 2018
Shaba kutoka Benin zinajumuisha michongo na mabamba ya kale hasa yaliyotengezwa kwa shaba ambayo yalipamba jumba la kifalme la Oba, Ovonramwen Nogbaisi, kwenye ufalme wa Benin, ambao ulijumuishwa katika enzi za ukoloni wa Uingereza nchini Nigeria.
Wakati wa ukoloni wa Uingereza, inasemekana kwamba vitu vya kale 1,000 viliishia katika makumbusho mbalimbali kote duniani.
Mwaka jana, taasisi zilikubaliana kurejesha baadhi ya vitu hivyo kwa makumbusho mpya ya Kifalme huko Nigeria, inayotarajiwa kufunguliwa mwaka 2012.
Luteni kanali John Patterson

Wala-watu wa Tsavo
Kulikuwa na simba wawili eneo la Tsavo nchini Kenya, waliowaua na kuwala wafanyakazi kadhaa wa shirika la reli mwishoni mwa karne ya 19.
Mabaki ya watu hao, yalihifadhiwa na kupelekwa katika jumba la makumbusho la Chicago.
Mamlaka nchini Kenya inataka irejeshewe mabaki hayo ya binadamu.
Rosetta Stone
The Rosetta Stone on display at the British Museum in Bloomsbury on October 14, 2016 in London

Jiwe la Rosetta
Moja ya vitu muhimu vya kale vilivyopo kwenye makumbusho ya Uingereza, ni jiwe la zamani kama ubao lililochongwa ujumbe uliotoa taarifa muhimu kwa wataalam kufunza maandishi ya michoro ya Wamisri ya zamani.

Jiwe hilo lilichongwa mwaka 1801 baada ya jeshi ya Uingereza kushinda jeshi la Napoleon nchini Misri.
Kwa miaka na vikaka, makumbusho ya Misri yamekuwa yakitaka jiwe hilo lirejeshwe.

Malkia wa Bangwa
Mchoro wa malkia wa Bangwa uliokuwa ukimilikiwa na wakfu wa Dapper mjini Paris, Ufaransa
Malkia wa Bangwa ni mchongo wa mbao wenye urefu wa sentimita 81 kutoka Cameroon, unawakilisha nguvu na afya ya watu wa asili ya Bagwa.

Malkia wa Bangwa ni mchongo wa mbao wenye urefu wa sentimita 81 kutoka Cameroon, unawakilisha nguvu na afya ya watu wa asili ya Bagwa.
Wakoloni wa Ujerumani walipewa sanamu hiyo au waliiba mwishoni mwa karne ya 20.

Ni watu wengi waliokuwa nayo na hatimaye ikaishia katika makumbusho ya Dapper,Paris.
Ripoti rasmi ya Ufaransa imependekeza kwamba sanamu hiyo irejeshwe ilikochukuliwa nchini Cameroon.

Kurudisha urathi wa Afrika
Ripoti ilioendekezwa na rais wa Ufaransa inasema kwamba vitu vya kale vilivyoibwa kutoka mataifa mengine ni sharti virudishwe

Ripoti ilioendekezwa na rais wa Ufaransa inasema kwamba vitu vya kale vilivyoibwa kutoka mataifa mengine ni sharti virudishwe
Kati ya asilimia 80 na 90 ya vitu vya makumbusho ya Afrika vipo kwenye makumbusho za kigeni, kulingana na ripoti rasmi ya Ufaransa iliyotolewa mwaka jana.

Inakadiriwa kuwa angalau karibia vitu vya kale 90,000 vilivyochukuliwa katika nchi za Afrika, hususan, nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara, zipo kwenye makumbusho ya Ufaransa.

Makumbusho ya Quai Branly nchini Ufaransa pekee inasemekana kuwa na vitu vya kale 46,000 vilivyochukuliwa kimabavu.
Tangu ripoti hiyo ilipotolewa, baadhi ya vitu vya kale vilivyoibwa vinatarajiwa kurejeshwa kutoka nchi za Ulaya hadi vilikotolewa ikiwemo vitu vya kale 26 vilivyochukuliwa nchini Benin, magharibi mwa Afrika ezi za ukoloni na kupelekwa katika makumbusho ya Quai Branly.
Mei mwaka huu, Ujerumani ilitangaza kwamba itarejesha alama ya jiwe kama msakaba iliyokuwa ikitumiwa na mabaharia ambayo iliwekwa katika pwani ya Afrika na Wareno mwaka 1496 hadi Namibia.

Vitu vya kale vya jamii ya wenyeji wa asili wa Australia pia vimerejeshwa. Hivi karibuni makumbusho ya Manchester yalirudisha vitu 12 .
 
mobutu alishauri hivi vitu virudishwe wakati akihutubia umoja wa mataifa
 
Sijui kama ni vya kweli au tushaundiwa copy halafu tunaipokea kwa sherehe.. wazungu sio watu wazuri ..saa nyengine..
 
Back
Top Bottom