Je, ni ustarabu au ni ujinga?

The patriot man

JF-Expert Member
Aug 16, 2015
968
1,064
Kwema wakuu

Mimi na wewe huwa tunanuka jasho au baadhi yetu midomo lakini ni mara chache saana kukuta mtu anamuambia mwenzake kuwa unanuka jasho au mdomo sijui kwa nini?

Badala yake tunakaa kimya tukivumilia harufu kali pasipo kumuambia mhusika lakini cha ajabu mtu anatoka hapo ataenda kumuambia mtu flani ananuka sana jasho au mdomo. Hii tuniitaje?
 
Sent from my SOV42 using JamiiForums mobile app
Pole mkuu.
naona wewe unanuka jasho
 
Watanzania wengi hatuna ustaarabu wa kutoa na kupokea feedback, mtu anaweza kukwambia kwa nia ya kukusaidia ukachukulia visivyo na kuanza kumtukana au kupelekea kukosana, hivyo hivyo kwa anayemwambia, anatumia lugha gani kufikisha ujumbe kwa muhusika.
 
Kila binadamu kaumbika akiwa na aibu,staha na kikubwa kiasi.Hata kama ni rafiki yako ni vema kujipa muda na kujiridhisha ili uweze kumwambia huyo ndugu/rafiki yako kwamba ana changamoto ya kutoa "kijiharufu" kisichopendeza cha jasho au mdomoni.Ukijifanya unaongea tu ukweli bila staha na kiasi ni kutafuta mivutano isiyokuwa ya lazima.Staha na kiasi kuzingatiwa.
 
Watanzania wengi hatuna ustaarabu wa kutoa na kupokea feedback, mtu anaweza kukwambia kwa nia ya kukusaidia ukachukulia visivyo na kuanza kumtukana au kupelekea kukosana, hivyo hivyo kwa anayemwambia, anatumia lugha gani kufikisha ujumbe kwa muhusika.
Hii imekaa vizuri saafi

Back
Top Bottom