Je, ni umbali gani unatakiwa kupandwa miti ifuatayo pembeni ya fensi ili mizizi isipasue msingi, mwisho ukuta?

Asante upo vizuri mkuu
 
Inafikirisha sana. Nje ukipiga michongoma bila ukuta halafu ndani ukaweka miti, na hiyo miti matawi yawe juu ninadhani itapunguza hii risk
Michongoma ina mizizi yenye nguvu inapasua hadi mawe mkuu. Panda michungwa limao komamanga curry tree hui haiharibu mizizi yake inakwenda chini kutafuta maji haisambai juu
 
Kama hakuna Muarubaini hapo basi nyumba yako iko salama
Muarobaini ninadhani ni management tu.

Kawaida mti ukiucha matawi yakawa makubwa basi na mizizi inatanuka zaidi ili kuweza kubeba uzito wake
Ila ukiupruni ukawa wa kivuli kidogo basi mizizi haiwezi kusumbua.

Muarobini ni dawa kwa mimea na binadamu kwa hiyo kwangu siwezi kuuondoa.
 
Michongoma ina mizizi yenye nguvu inapasua hadi mawe mkuu. Panda michungwa limao komamanga curry tree hui haiharibu mizizi yake inakwenda chini kutafuta maji haisambai juu
Michongoma hapa nimemaanisha ya fensi.

Ni kweli michongoma ni hatari iwapo ukiiacha ikawa miti, ila ukiifanya fensi wala mti wake hauzidi fimbo ya kuwachapia watoto.

Ni uzoefu wa muda mrefu sana na miti
 
Naomba kuuliza wataalamu wa miti;

Je, ni umbali gani unatakiwa kupandwa miti ifuatayo pembeni ya fensi ili mizizi isipasue msingi, mwisho ukuta?

1. Michungwa na milimao

2. Miparachichi

3. Miembe

4. Mipera

Natanguliza shukrani!
Inategemea ni miti hiyo uliyotaja haina effect kubwa nyumba nauoishi ina miembe mkubwa nusu mita kutoka kwenye msingi hatuoni nyufa sakafuni wala ukutani tunakula maembe tu
 
Naomba kuuliza wataalamu wa miti;

Je, ni umbali gani unatakiwa kupandwa miti ifuatayo pembeni ya fensi ili mizizi isipasue msingi, mwisho ukuta?

1. Michungwa na milimao

2. Miparachichi

3. Miembe

4. Mipera

Natanguliza shukrani!
well, hakikisha unachimba shimo kubwa liende chini ya msingi, na hata kama ni kumwagilia hakikisha unachimbia PVC ikute ile roots weka kokoto ukifanya hivyo roots will go down na msingi wako utakuw a salama kabisa
 
Naomba kuuliza wataalamu wa miti;

Je, ni umbali gani unatakiwa kupandwa miti ifuatayo pembeni ya fensi ili mizizi isipasue msingi, mwisho ukuta?

1. Michungwa na milimao

2. Miparachichi

3. Miembe

4. Mipera

Natanguliza shukrani!
Nilikata kwa 'uchungu' miembe dodo miwili baada ya kujishauri kwa miaka kadhaa kutokana na kuwa naziba nyufa kila baada ya meizi michache.. Mafundi walikuwa wanakula hela zangu tu.. Ila embe nazikumbuka hata leo zilivyokuwaga nyingi na tamu dah...
 
Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…