Je ni uamuziii gani utachukua

KAJICHO KIVULI

JF-Expert Member
Jul 30, 2013
2,065
1,195
ukiwa huna hili wala lile unashtuka na kofi moja zito la uso linakupeleka kufumba macho, kabla huja kaa sawa inakuja ngumi ya uso halafu unasikia sauti ya anae kupiga ikisema NILIKWAMBIA IPO SIKU NITAKUKAMATA TU ile kuinua sura unakutana na sura usiyoifahamu kabisaaaaa!!! halafu na yeye anashtuka baada ya kukuona kisha anakwambia SAMAHANI NIMEKUFANANISHA

Je ni uamuziii gani utachukua....
 

Muwazi

JF-Expert Member
May 16, 2014
355
225
Upo sehemu unatembea kwa
miguu katikati ya safari yako ukiwa
huna hili wala lile unashtuliwa na
kofi moja zito la uso mpaka
unafumba macho ile hujakaa sawa
Inakuja ngumi ya pua,halafu
unasikia sauti ikisema ""NILIKWAMBIA IPO SIKU NTAKUKAMATA'' ile unainua sura unakutana na mtu
usiemjua kabisa halafu na yeye
baada ya kukuona vizuri
anasema"SAMAHANI
NIMEKUFANANISHA"" Swali :Sasa
hapo utafanyaje???
 

mende 2014

JF-Expert Member
Apr 13, 2014
765
225
Yaani jibu nitalipata siku hiyo ya tukio maana ndo nitajua kuwa ni kofi la aina gani maana duh!
 

Master plan

JF-Expert Member
Dec 24, 2012
3,665
2,000
Nampotezea aondoke kisha nakusanya nguvu halafu namfata kwa nyuma nampa bonge
la tama ile anafika chini namkanyaga buti la kichwa akinyanyuka namkung'uta ngumi ya roho halafu namuuliza kuna jipya?
 

charger

JF-Expert Member
Nov 21, 2010
2,322
1,225
Hapana huta mfaidi kama alivyokufaidi,chamsingi unamfuatilia mpaka ujue anapoishi then unajipanga kumteka.Hapo utamfaidi saaaafi.
 

kaka cliff

Member
May 18, 2014
45
0
Kama ni mimi kwanza nalia, alafu nitamparura, kisha namng'ata then namalizia na bonge la ngumi la shingo kudadeki
 

HARUFU

Platinum Member
Jan 21, 2014
28,330
2,000
ukiwa huna hili wala lile unashtuka na kofi moja zito la uso linakupeleka kufumba macho, kabla huja kaa sawa inakuja ngumi ya uso halafu unasikia sauti ya anae kupiga ikisema NILIKWAMBIA IPO SIKU NITAKUKAMATA TU ile kuinua sura unakutana na sura usiyoifahamu kabisaaaaa!!! halafu na yeye anashtuka baada ya kukuona kisha anakwambia SAMAHANI NIMEKUFANANISHA

Je ni uamuziii gani utachukua....
Yaani natabasamu kabla ya kukujibu, kwa kweli ....

Maana kitakachofuata hakitabiriki kwa wakati huo wa tukio litakapotokea

Ngoja niishie hapa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom