Je, Ni sahihi watoto wadogo kufundishwa 'Re-production?

Papushikashi

JF-Expert Member
Feb 28, 2016
10,913
13,232
Habari JF,

Kuna dogo mmoja wa darasa la sita kaja kuniuliza swali la sayansi kuhusu mfumo wa uzazi, sasa wakati mimi najifikiria nitamjibu vipi kutokana na swali lenyewe limekaa kiutu uzima (reproduction) na yeye umri wake ni mdogo miaka 11.

Akaniambia usione aibu wewe niambie hata wakati mwalimu anatufundisha alikuwa haoni aibu, nikamwambia nitakujibu baadae. Kwa mtazamo wako unaona ni sahihi kumwambia kila kitu maana enzi zetu kidogo tulikuwa tunasoma wakubwa tofauti na sasa.
 
Ni sahihi kwa sababu huo umri ndio wanabarehe na katika reproduction ndio hufundishwa juu ya mabadiriko ya miili yao, mfano ndoto nyevu, kuota nywele sehemu za siri, kuota matiti wasichana, sauti kuwa nyororo(ke), nzito(me) na hedhi, haya ni mambo ya muhimu wao kuyajua kwa sababu nyumbani inakuwa ngumu kufundishwa hayo kwa sababu kamaunazozifikiria wewe, kumbuka pia kwa sasa watoto wanabarehe mapema kuliko zamani i think vyakula vinachangia.
 
Inapaswa kufundishwa. Kama wizara imeliona ni vema. Pili,mjibu tu huyo dogo kwani usipomjibu ataenda kuulizia kwingine na baadae atakuona ww poporo kwa kutokujua (nadharia yake).
 
Ni sahihi kwa sababu huo umri ndio wanabarehe na katika reproduction ndio hufundishwa juu ya mabadiriko ya miili yao, mfano ndoto nyevu, kuota nywele sehemu za siri, kuota matiti wasichana, sauti kuwa nyororo(ke), nzito(me) na hedhi, haya ni mambo ya muhimu wao kuyajua kwa sababu nyumbani inakuwa ngumu kufundishwa hayo kwa sababu kamaunazozifikiria wewe, kumbuka pia kwa sasa watoto wanabarehe mapema kuliko zamani i think vyakula vinachangia.
Asante mkuu, ila huku uswahili wakikuta mtoto kama huyo nampa somo hilo si wanaweza kunichukulia tofauti?
 
Kama ni mtoto wako haina shida na umfundishe vitu basic kama nilivyotaja hapo kulingana na kipindi/umri aliopo, kushindwa kufanya hivyo kunawapa fursa watu wengine kumfundisha isivyosahihi, timiza wajibu wako.
 
Sio mtoto wangu, ni wa jirani
 
Mshauri aende akamuulize mwalimu wake wa somo maana wewe sio mwalimu na hujui mipaka ya mada hiyo
 
Back
Top Bottom