Je ni sahihi nilichofanyiwa?

Je ni sahihi nilichofanyiwa?

Kisampido

Senior Member
Joined
Jun 19, 2013
Posts
157
Reaction score
65
Naombeni ushauri wana Jamiiforums.

Kuna ofisa mmoja alinialika kwenye warsha nilikwenda na kushiriki siku kadhaa nikiwa huko akanitaka kimapenzi nikamweleza kuwa Niko kwenye ndoa niliporudi nyumbani akatuma meseji ya mapenzi kwangu kuwa nikimpa atanifanyia makubwa.

Hiyo meseji ikaonwa na Mme wangu ugomvi mkubwa ukatokea na nikamweleza Mme Wangu hali halisi, na kumtaarifu yule afisa kilichojili.

Sasa siku chache zijazo kuna semina nyingine, jana kanitumia ujumbe hawezi kuniita tena eidha nichague ndoa au pesa na kujiendeleza kielimu.

Naomba ushari kabla sijamuanika kwani Nina meseji zake nyingi za kijinga na nimeona kama unyanyasaji kwangu.
 
mripoti ngazi za juu yaweza kukuweka salama ukimchekea utavuna mabua
 
Unaomba ushauri kabla hujamuanika!!!!
Mumeo amekushauri nini?
 
Tumia hizo msgs kama ushahidi utakapokwenda kumshtaki ngazi za juu tofauti na hapo kuna mawili kupoteza kazi au kupoteza mume kazi kwako.

Sent from my iPhone using JamiiForums mobile app
 
Mlengeshe PCCB akanyee ndoo huyo team mafisi.Upo mkoa gani kwani?
 
Naombeni ushauri wana jf kuna ofisa mmoja alinialika kwenye warsha nilikwenda na kushiriki siku kadhaa nikiwa huko akanitaka kimapenzi nikamweleza kuwa Niko kwenye ndoa niliporudi nyumbani akatuma msg ya mapenzi kwangu kuwa nikimpa atanifanyia makubwa hiyo msg ikaonwa na Mme wangu ugomvi mkubwa ukatokea na nikamweleza Mme Wangu hali halisi,na kumtaarifu yule afisa kilichojili sasa siku chache zijazo kuna semina nyingine Jana kanitumia ujumbe hawezi kuniita tena eidha nichague ndoa au pesa na kujiendeleza kielimu naomba ushari kabla sijamuanika kwani Nina msg zake nyingi za kijinga na nimeona kama unyanyasaji kwangu.

Njoo ujibu hizi tuhuma zs tyta
 
naona hujaandika vizuri ikaeleweka. unasema kuna afisa mmoja alikualika, ofisi/ kampuni hiyo ni yake? ni bosi wako kazini? umuhimu wa warsha hizo nini? je ni pesa peke yake? wewe hupati pesa bila warsha? yeye ndiye kashika ajira yako? kwa nini akualike wewe tu? ameshakupa uchaguzi ndoa na pesa sasa umeshindwa chagua? kwani wewe ndo unahudumia mme wako? kwani hulipwi mshahara hadi uende warsha?
 
Kakaaa kimya! Na hivi cheti hunaaa usiwaamshe walio lala! Manake wakifata protocal kuna vigezo vingi vya kukutoa!
 
Ww unaona kipi bora kat ya semina au ndoa? Mikurumbembe utaijua tu staki nataka hili
 
Naombeni ushauri wana jf kuna ofisa mmoja alinialika kwenye warsha nilikwenda na kushiriki siku kadhaa nikiwa huko akanitaka kimapenzi nikamweleza kuwa Niko kwenye ndoa niliporudi nyumbani akatuma msg ya mapenzi kwangu kuwa nikimpa atanifanyia makubwa hiyo msg ikaonwa na Mme wangu ugomvi mkubwa ukatokea na nikamweleza Mme Wangu hali halisi,na kumtaarifu yule afisa kilichojili sasa siku chache zijazo kuna semina nyingine Jana kanitumia ujumbe hawezi kuniita tena eidha nichague ndoa au pesa na kujiendeleza kielimu naomba ushari kabla sijamuanika kwani Nina msg zake nyingi za kijinga na nimeona kama unyanyasaji kwangu.

Hiyo ni sexual harassment ya hali ya juu, nenda TAMWA, mfyatue tu.

Hana adabu hata chembe huyo, hiyo rushwa anayoitaka ni dhambi kuliko rushwa ya kuomba pesa. Maana ni dhambi (rushwa) juu ya dhambi (zinaa).
 
mwenzio anakutaka kweli.....njia kuu inamashimo kibao....chepuka upande ndege uende warshani....pole yako.....
 
Unahofia kutoitwa kwny.semina?!!
Au kutoa papuchi??

Sijaona kama amekutishia kukufukuza kazi, muhimu kusanya visibitisho vya kutosha kama ataendelea na tabia hio ndo uende kutoa taarifa kwa wahusika
 
buuull shi1t boss

kikubwa ni wewe na mumeo muwe kitu kimoja na muwe tayari kwa lolote litakalojitkeza

fight for ur right
 
Kwani amezuia mshahara wako.....au we unaishi kwa kutumia warsha?
Achana na warsha na ishi jama kawaida.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom