msabillah
JF-Expert Member
- Dec 5, 2011
- 4,764
- 3,189
Ahsante sana kwa kutupamba mkuuJibu watakuwanalo Wazaramo.
Miaka ya90 nilifika Dar kwa ajili ya kutafuta kazi, sikuwa peke yangu, tulikuwa kundi vijana ka'5'ivi.
Kati yetu mmoja alikuwepo mnyamwezi, na msukuma pia alikuwepo.
Kilichokuja kunishangaza, yule mnyamwezi aligombaniwa na wanawake kama mpira wa kona, hasa majimama yenye hela zao ili wamlee kwa gharama zozote zile.
Nikijua wanyamwezi na wasukuma ndiyo walewale, nikataka nitembekee nyota ya msukuma, nikajiita nami msukuma.
Wote siye wasukuma na wengine tukawa tunaswagwa shambani, kwamba siye ni mijitu tu yanayostahili kazi ngumu, lakini si kwa mwenzetu mnyamwezi.
Sasa nikaja kuuliza wenyeji nini maana ya jambo hilo!
Nikaambiwa kuwa wanyamwezi huku pwani wanapendwa na kuheshimika sana na wazaramo, hawana lolote la kusema wakiona mnyamwezi awe wa kike ama wa kiume, wote ni mali adimu.
yaani ni kama mbwa aonavyo chatu na kujisogeza bila shurti mzaramo akiona myamwezi!
Nikasema sawa, lakini nini sababu?
Nikaambiwa ni wazuri sana kwenye mambo yetu yalee!
Kama ni dozi, basi wao hutoa full package!
Nipe namba yako nikutumie salio.