WomanOfSubstance
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 5,457
- 956
Waungwana,
Kuna kitu kimekuwa kinanitatiza kwa kipindi kirefu. Kitu hiki kinahusu kugeuza majina ya kikabila na kuyapa uzungu bila sababu za msingi.Labda kuna sababu ambayo siijui. Inakuwaje kwa mfano mmaasai anayeitwa Laiza kugeuza jina na kujiita " Laizer/Laiser", au mchaga anayeitwa Hoi-se na kujiita "Hoyce"..
wapo pia wale wanaoongeza "s" mwisho wa majina yao kama "Mnzavas", "Matingas" au kugeuza kabisa jina kama vile Juma kujiita " "Jimmy"
Inakuwaje hii? watu wanaonea aibu majina yao au wanafikiri kuyapa nakshi ya kizungu/kigeni ndio ujiko?Nahitaji somo hapa.