Kaka huo unasibu wa lugha! muktadha wa matumizi ya neno kama ulivyobainisha ni shahihi.Neno hofu kama lilivyotafsiriwa na mdau hapo juu lina maana ya kuwa katika hali woga, wasiwasi hatihati na hali nyingine zinazofanana na hizo! Kwa vyovyote vile hali ya watu kuumia katika ajli si ambo la heri. Kwa sababu hiyo mzungumzaji lazima aonyeshe hofu juu ya tukio hilo na mara nyingi neno hili hutumika pale ambapo hakuna uthibitisho wa idadi kamili ya majeruhi au vifo katika tukio husika. Vinginevyo lingeweza kutumika neno inasadikiwa/ taarifa za kusadikika n.k.Ni mtazamo tu![/QUOTE]
Pamoja na maelezo yako mazuri hapo juu, bado napatwa na sintofahamu kuhusu maneno niliyokoleza hapa. Kwamba, unakubali kuwa si sahihi kutumia "kuhofia" mahali pa "Kusasadikiwa/kukadiriwa"?