Je, ni sahihi Kanisa Katoliki kuzuia Waumini wake kwenda kuombewa kwa Mtume Mwamposya?

Kama wana Katiba yao inayowaongoza kufanya hivyo..., To each their Own..., Ila wenye tatizo ni wale wanaonganganiza kwenda sehemu wanayotengwa

Anyway Imani yoyote inayotenga watu kwangu mimi ni Cult.., Binafsi ningependa kundi ambalo lipo milango wazi linakaribisha kila atakaye karibia hata kama jana alikuwa pengine na kesho ataondoka... zaidi ya hapo naona kama ni kuwa enslaved mentally
 
Bora waamke sasa maana kuna uzi mwembamba kati ya waganga wa kienyeji na yanayoendelea kwenye baadhi ya makanisa. Hii ilipaswa kuwa nchi nzima. Haiwezekani mtu anaibuka tu na kuanza kupaka watu mafuta ya "upako" alafu usionye kondoo zako. Watapakwa hadi mafuta ya kipepo huku jina la Yesu likisingiziwa!

Akina mama ndio mabingwa kutwa kutafuta mafuta ya " upako" mengine wanachanganyia waume zao kwa siri na kunuiza ili aache pombe n.k purely uchawi uliopakwa rangi ya Ukristo.
 
padri hivi anaweza kumuombea mtu akapona? maana sijawahi kuwaona wakitumia jina la Yesu kuombea
Ukatoliki ni imani kamili isiyohitaji kukopa chochote. Hakuna haja ya malumbano, kama huko ni bora si wabakie huko? Kanisa halilazimishi ila halitaki kujichanganya kama mtu usiyeelewa unataka nini. Wito ndio huo waliopewa otherwise waache imani!
 
Kama wana Katiba yao inayowaongoza kufanya hivyo..., To each their Own..., Ila wenye tatizo ni wale wanaonganganiza kwenda sehemu wanayotengwa

Anyway Imani yoyote inayotenga watu kwangu mimi ni Cult.., Binafsi ningependa kundi ambalo lipo milango wazi linakaribisha kila atakaye karibia hata kama jana alikuwa pengine na kesho ataondoka... zaidi ya hapo naona kama ni kuwa enslaved mentally
Kwamba Mkristo awe anakuja anapokea Ekaristi alafu baadae yupo msikitini aachwe? Wengi shida mnayopata ni vile zaidi ya kusoma biblia Ukristo hamuujui! Historia ya Kanisa hamjui, imani tumeipokeaje na kuilinda hata leo hamjui!

Mnafikiri Ukristo umefika hapa kiholela kila mtu anaibuka na kufanya yake! Ukristo sio kokoro la kubeba kila kitu! Hata Uislamu huwezi kuibuka na mambo ambayo hawajawahi kuyapokea! Imani ikiwa holela itapotea tu.

Ndio maana Yesu alipoondoka alituachia vitu viwili tu, Kanisa ( Mitume) na Roho Mtakatifu! Hivi viwili ndio vilivyotupa hii bible tunayotumia na mafundisho mbalimbali nje ya hayo maandiko. Hivyo wajibu wetu ni kutojiongoza kama vipofu bali kusikiliza Kanisa.
 
Inasemekana baada ya Kanisa Katoliki Iringa kuwataka Waumimi wake walioombewa na Mtume Mwamposya kutubu sasa katazo hilo ni kwa nchi nzima.

Je, ni sahihi Kanisa Katoliki kuzuia Waumini wake kuombewa kwa Mtume Mwamposya?
Huu mjadala ulishajadiliwa humu kitambo! Cha kushangaza unauleta tena! Mbaya zaidi na mods nao wanauacha kwa makusudi, badala ya kuufuta au kuunganidha na ule mwingine.
 
Kwamba Mkristo awe anakuja anapokea Ekaristi alafu baadae yupo msikitini aachwe? Wengi shida mnayopata ni vile zaidi ya kusoma biblia Ukristo hamuujui! Historia ya Kanisa hamjui, imani tumeipokeaje na kuilinda hata leo hamjui!

Mnafikiri Ukristo umefika hapa kiholela kila mtu anaibuka na kufanya yake! Ukristo sio kokoro la kubeba kila kitu! Hata Uislamu huwezi kuibuka na mambo ambayo hawajawahi kuyapokea! Imani ikiwa holela itapotea tu.

Ndio maana Yesu alipoondoka alituachia vitu viwili tu, Kanisa ( Mitume) na Roho Mtakatifu! Hivi viwili ndio vilivyotupa hii bible tunayotumia na mafundisho mbalimbali nje ya hayo maandiko. Hivyo wajibu wetu ni kutojiongoza kama vipofu bali kusikiliza Kanisa.
Kwamba hata leo Shetani angemrudia huyo Yesu anayesamehe sabini mara saba angemfukuza ?

Au story za prodigal son zimetokea wapi ?

Na kama ungenielewa nimesema kila watu na katiba yao hata wakisema wanapokea wanywa damu ya kunguru ni sawa kulingana na misimamo yao..., tatizo ni wale wanaongangania kujiunga na wasiowataka wakati wanaweza kuondoka...
 
Ki - imani hawapo sahihi

Ila

Ki - Biashara wapo sahihi

Moja ya misingi ya biashara ni kulinda wateja wako kwa kadri unavyoweza...
 
80.jpg
 
Huu mjadala ulishajadiliwa humu kitambo! Cha kushangaza unauleta tena! Mbaya zaidi na mods nao wanauacha kwa makusudi, badala ya kuufuta au kuunganidha na ule mwingine.
Kanisa Katoliki limetoa waraka wa katazo

Uko.nyuma sana bwashee
 
Roman wako sawa, ukiona mtu anasali makanisa matatu matatu maana yake hana imani kanisa lake.
 
Wanaosali kwa mwamposa na Manabii dizain hiyo ,wengi Wana matatizo ya Akili

Huwez kuuziwa maji ,mafuta UNADANGANYWA yana Upako

Inaonesha jins gan husomi maandiko

BIBLIA inasema Mmepewa bure toen bure

Wewe unauziwa

Biblia inasema OMBENI NANYI MTAPEWA

wewe unakwenda kwa kina mwamposa unatoa pesa uponywe, Ni UZWAZWA
 
Unaweza kwenda na hirizi kanisani katoliki,he!!!???unaweza kwendanayo kwenye viwanja vya kawe muda ule wa maombi?jiangalie wewe...
 
Back
Top Bottom