Je, ni ruksa kwa Magari binafsi kupigwa label ya Jeshi?

Rufiji dam

JF-Expert Member
Feb 20, 2020
3,804
8,797
Kwa takribani mara tatu nikiwa Dar nimejionea mambo ya kushangaza. Kuna siku nimeona gari binafsi IST nyuma kwenye bumper kuna stika ama chata ya Jeshi.

Na kuna siku tena nikaona Subaru mbele pale kwenye boneti kuna pua napo kumepigwa chata ya jeshi.

Je, ni ruksa haya mambo magari ya binafsi kuwa na chata za jeshi?
 
Mbona siyo kitu cha kushangaa mzee, hata wewe unaweza tu kuweka chata hapo kwenye passo yako
 
Chap ngoja nikaweke chata ya jeshi kwenye jepp yangu fasta narudi kutoa comment 🏃🤦
 
Sasa wewe tafuta sare za jeshi kabisa weka kama cover kwenye Range Rover yako.. "Dawa ya kiburi ni jeuri"
 
Mkuu sijaelewa ulichouliza! Chata, chata gani ama unazungumzia namba za usajili(plate#)?

Hili utaendelea kuhojiwa sana na wadau, ungelifafanua vizuri basi ungelipata jibu mujarabu.
 
Mkuu sijaelewa ulichouliza! Chata, chata gani ama unazungumzia namba za usajili(plate#)?

Hili utaendelea kuhojiwa sana na wadau, ungelifafanua vizuri basi ungelipata jibu mujarabu.
Huyu mwenyewe ni mjeshi ila hajui kazi nyingine za jeshi tofauti.kazoea kuona madude makubwa makubwa tu.

Anaita chata badala ya plate number.
 
Back
Top Bottom