Ukitaka kujua kuwa wewe ni mwenye kijicho dhidi ya mafanikio au jitihada za wenzio, jiulize maswali machache yafuatayo:
Je unaposikia jirani kanunua gari, kajenga nyumba, kafungua biashara kubwa au mwanae kapata nafasi ya kusoma nje ya nchi na mengine mengi kama hayo maadamu yawe mafanikio, unajisikiaje moyoni?
Au jirani yako anapokuomba ushauri wa kuanzisha biashara, kununua shamba, gari au nyumba, unampa ushauri kwa moyo mweupe au unatoa ushauri usiofaa?
Kwa vyovyote vile, majibu ya maswali hayo hapo juu yanatosha kukujulisha iwapo una kijicho dhidi ya mafanikio ya mwenzio au la.
Hebu tusiwe wanafiki, tujifanyie tathmini ili tujijue tuko upande gani……………
Nani athubutu?
Nilijua tu kwamba huu uzi wadau wataukwepa maana umegonga ikulu..................
Kumbe wote tulio humu JF tuna KIJICHO eh.......................!
Heri wewe umekuwa mkweli wengine wenye kijicho nafsi zinawasuta, hawataweza kutia neno humu.............Sina wivu, sielewi even how it feels kumuonea mtu kijicho
Labda nikubali kutamani wakati mwingine na sijui kuyavuta matamanio yangu zaidi ya machoni na inaishia hapo.........
Kwani wanaJF wanajuana humu? wote si tunatumia majina na yasiyo yetu.......... sasa hofu ni ya nini? nyie fungukeni tu, wala hakuna atakeyewajua, baadae nitatoa darasa hapa namna ya kuondokana na kijicho..............stay tunelol... Jibu langu huwezi amni... hii tathmin unaweza pata majibu sahihi pale tu kama ni anonymous. sio kwa njia hii...
Yaani umesema sahihi kabisa..........Mtambuzi, uzi wako siyo watu wanakwepa ila mada uliyoiweka imekuwa na changamoto kwenye kuichangia. Kwa upande wangu mimi suala la kuwa na kijicho au kutokuwa na kijicho inategemea na ukaribu wa huyo mtu ambaye anamuonea kijicho/asiyemuonea kijicho mwenzie.
Kwa mfano si rahisi, mtu akigombana na mwenzake, kwa vyovyote vile, hatapenda kuona mwenzake (huyo mgomvi wake) anafanikiwa kwa yale atakayokuwa anayafanya. Hii ni nature ya binadamu na ndiyo maana kuna msemo unasema adui yako muombee njaa, na huwa hawasemi muombee mafanikio!!!
Lakini ktk hali ya kawaida, huwezi kuwa na kijicho kwa yule mtu ambaye una mahusiano naye mazuri. Kwa mfano rafiki zako, ndugu zako, jamaa zako wa karibu nk nk huwezi kuwaonea kijicho wanapofanikiwa na kama ikitokeo hivyo, basi wewe utakuwa na matatizo au una ile kitu inayoitwa ROHO MBAYA! :confused2:
BADILI TABIA nina waasiwasi na kauli yako, inamaana mimi Mtambuzi nikipata Ukuu wa Wilaya utakuwa na roho nyeupeeee kabisa.......................wenzangu wakifanikiwa nafurahia mafanikio yao
Heri wewe umekuwa mkweli wengine wenye kijicho nafsi zinawasuta, hawataweza kutia neno humu.............