Je, ni mapenzi au ana lake jambo?

Je, ni mapenzi au ana lake jambo?

Hakunaga kuachana Kwa wema Wala kuachana Kwa ubaya.. kama mmeachana mmeachana tu, mawasiliano ya nini Tena???. Ukiendelea kuwasiliana na ex ipo siku utamla tu. Songa mbele kijana
 
Uyo ushaachana nae fanya mambo yako unasema uwa anakutumia sms kwani lazima kujibu text zake kitendo cha ww kuwa positive kwake inaonesha apo kuna kitu mtakifanya soon
 
Hakunaga kuachana Kwa wema Wala kuachana Kwa ubaya.. kama mmeachana mmeachana tu, mawasiliano ya nini Tena???. Ukiendelea kuwasiliana na ex ipo siku utamla tu. Songa mbele kijana
Asante sana mkuu
 
Uyo ushaachana nae fanya mambo yako unasema uwa anakutumia sms kwani lazima kujibu text zake kitendo cha ww kuwa positive kwake inaonesha apo kuna kitu mtakifanya soon
Itabidi niache kujibu maana inakua too much..
 
Yeye ndo anaanzaga kunitafuta mkuu, alafu mimi sinaga muda wa kuwekeana vinyongo na mtu kwahiyo Huwa najibu tu text zake kama kawaida.

Basi hapo dalili ya kurudiana naye tu...
 
Tuliachana mwezi January mwaka 2018, kila mtu aka-move on na yakwake, binafsi niliumia sababu nilimpenda kweli na yeye alinipenda ila kama unavyojua sababu tu za kiufundi za hapa na pale zikatutenganisha.

Nikiri tu kuwa shinikizo kubwa la mimi na yeye kuachana ilikua ni rafiki zake. Rafiki zake walichangia pakubwa sana sisi kuachana na haikuishia hapo wakamjaza maneno akawa anatema shombo sana juu yangu, kama mwanaume wala siku-react, nikaona ni mambo ya kawaida tu yatapita.

As people say, time heals everything, with time I started getting better and I reached a point where I completely forgotten about her. Lakini pamoja na kuwa tulisha-move on karibia miaka 5 nyuma, yeye bado anaonyesha wivu sana juu yangu.

Bado anaonekana kuumia sana anionapo na mwanamke mwingine, na inapowezekana atatumia njia yeyote hata ya kusambaza sumu ili ahakikishe tumeachana, kuna muda tulikua tuki-chat Ile kishkaji tu ila through her conversations unaona kabisa kuna kitu ana push.

Kuhusu kimuonekano nisiwe muongo ni binti mzuri sana, ambaye almost kila mwanaume angependa kuwa naye, na ninawaona vijana wanavyopishana kwake. Ila ndo hivyo tu, sisi wengine tumejaaliwa mioyo migumu hatupelekeshwi na wanawake, ukileta miyeyusho unapita kushoto.

Basi ndo hivyo wakuu, najua humu kuna wakubwa zangu wenye experience kubwa kwenye hii sekta, naombeni ufafanuzi au ushauri wenu. He haya ni mapenzi au mchawi tu?

Naombeni kuwasilisha
hii tabia wanawake wanayo, mkiachana hawapendi kabisa upate pisi nyingine nzuri ufurahi na moyo wako. kwa kifupi hawapendi uwe na furaha ukiwaacha.
 
hii tabia wanawake wanayo, mkiachana hawapendi kabisa upate pisi nyingine nzuri ufurahi na moyo wako. kwa kifupi hawapendi na furaha ukiwaacha.
Umeongea fact sana mkuu, maana huyu anavyo ni-monitor kimya kimya mpaka imekua kero sasa..
 
Kiazi cha moto huyo achana naye, sasa wewe mbugie ujute. Kama alikuona mara ya kwanza hufai unafikiri atakuona unafaa tena?

Ukimrudia huyo utakuja kulia kabisa, kama mwanzo uliumia
 
Nadhani ni yeye ambaye angeulizwa, anachotaka kwangu ni nini sababu ananifuatilia sana mpaka anakua too much..
Umempa attention kwahiyo lazima ahisi unampenda, ukimkaushia kila anapotuma sms jibu atalipata kuwa humuhitaji na utamsaidia yeye ku mvoe on kiukweli na wewe ku move on pia
 
Ipo hivi huenda anataka kurudi kwasababu kweli kaumizwa na amejua thamani yako, anaweza akarudi kwako akatulia kabisa.
Sema shida inakujaga hapa wanaume kusahau ni changamoto, hivyo ugomvi utakuwa ni wa mara kwa mara , in short wewe ndio utapata shida kusihi naye kwasababu imani kwake huna, utahis mda wowote anaweza zingua tena.

Kuna sababu wanaitwaga ex, as long as amepita hata kama unamtamani vipi achana naye, mwisho wake huwa mbaya.
Futa mawasiliano sio kwa nia mbaya ila ili asiwepo akilini mwako na wewe usiwepo akilini mwake.
 
Nadhani ni yeye ambaye angeulizwa, anachotaka kwangu ni nini sababu ananifuatilia sana mpaka anakua too much..
Wewe ndio umempa nafasi ya yeye kukufuatilia,ungempotezea toka mwanzo asingekufuatilia,inaonekana una enjoy sana kuona anakufuatilia But kua muanfalifu sana.
 
Hutofautiani sana na kaka yangu mkubwa ninayefuatana naye kwa kuzaliwa. Huwa anahangaika sana uachana na chuda pindi wanapoachana matokeo yake anaonekana anakua miaka tu (umri) akili ipo palepale.

Ukishaachana na mwanamke futilia mbali kila kitu kisha songa mbele na yule uliyenaye kwa wakati huo inatosha.

Kua brother, miaka hairudi nyuma inasonga mbele
 
Back
Top Bottom